Propaganda za kukuza uwezo wa Rwanda kijeshi zinahatarisha usalama wa nchi yetu hapo baadaye

Mkuu kwani Tanzania iko vitani na Rwanda?
Kama ni swala la kijeshi kwa nini tusijilinganishe na Kenya,Uganda,Misri,Nigeria,Morocco,South Africa,nk
Kwa nini tuone kipimo cha ubora wa jeshi letu ni kuishinda Rwanda?
Misri inapokea misaada ya kijeshi kutoka Marekani na inasemekana ndiyo ni moja ya nchi bora kijeshi Africa! Kwa nini tusijilinganishe na nchi hiyo kijeshi?
 
Sasa kama jeshi linachukua magari yake na kuipa CCM ili ibebe wajumbe wa mkutano mkuu na kuwapeleka DODOMA kwenda kumpitisha mtu kinyume cha taratibu hata za CCM yenyewe, hapo kuna kitu hapo?
Jeshi linategemea mtu kama lugumi ndio akalichagulie silaha za kununua kwa kweli tunasafari ndefu sana
 
Tumelala sana na kujisahau
Tushakuwa wakata mauno kama wakongo

Ova
 
Tumelala sana na kujisahau
Tushakuwa wakata mauno kama wakongo

Ova
Na kibaya zaidi vijana wengi wanaoajiriwa Leo wamekua legelege sana inawezekana ndio hao wajomba maana tunakunywa nao pombe bar unajiuliza hawa nafasi wamepataje? Maana unaweza piga kibao asiamke
 
Maswala ya jeshi ni complex kidogo, Wenyewe wanajua wanachofanya hata hivyo suala la jeshi la rwanda kukuzwa kwa propaganda ni la kuangalia sasa si la kupuuzwa.
Nauhakika wazee wa MI wanalifanyia kazi
VIVA TANZANIA.

Naam Mkuu
 
Na kibaya zaidi vijana wengi wanaoajiriwa Leo wamekua legelege sana inawezekana ndio hao wajomba maana tunakunywa nao pombe bar unajiuliza hawa nafasi wamepataje? Maana unaweza piga kibao asiamke
Kutwa kukatika maunooo

Ova
 
Hivi Rwanda ina ukubwa kama wilaya moja ya korogwe tu au imezidi? Yaani siku Rwanda au M23 wakijichanganya wakavamia bongo jina lao litabadilika
Haya ya kuchukulia poa eneo ndio ujinga wenyewe ambao unatupumbaza.. embu angalia israel ina eneo na population gan tofauti na zile nchi za kiarabu zinazoizunguka halafu angalia zinavyoendeshwa na israel pale
 
Umeshakuwa mwanajeshi? Vinginevyo hizi ni sawa na porojo za kijiweni. Hata hivyo huo ni ushabiki wa kijiweni km wa simba na yanga. Watanzania wa leo wanashabikia kila kitu kinachokuja mbele yao. Vita vya Israel na Hamas wapo, vita vya Russia na Ukraine wapo n.k.
 

Hiyo inamaana gani?
 
Naam uko vizuri mno kwa kuujali UKWELI huu wa hakika.
 
ila Rais Kagane msimchukulie wa kawaida!

Uwezi fahamu yuko na mataifa gani yenye nguvu kijeshi na kiuchumi.
 
Acha ujinga Hilo ni jeshi la ccm sio wananchi
Haukuwa na haja ya kuniita mjinga; hata hivyo kudharau jeshi letu sio sawa. Tuna nchi moja tu na hiyo ni Tanzania. Jeshi letu ni moja tu, wana kazi ngumu ya kulinda mipaka yetu. Wakati sisi tunakula na kulala kuna ndugu zetu wengine hawalali kutuhakikishia ulinzi. Respect our men in Uniform
 
Wewe jeshi linakusaidia nini wakati huna ajira?
 
Unakosea!

Hili suala linahitaji utaifa. Unaweza ukaichukia serikali lakini si taifa.

Siasa za upinzani ziishie kwenye serikali na mambo ya siasa. Lakini taifa linapokuwa hatarini utaifa unapaswa kuwekwa mbele.
Shida yake anafikiri nchi ikiingia vitani sasa, wapinzani hawatashambuliwa, au anadhani upinzani ukichukua nchi sera za Jeshi zitabadilika. Jeshi litabaki kuwa lile lile. Ukiona mtu yeyote anabeza jeshi la nchi yake hajui maana ya utaifa wake. Kwake siasa ni bora kuliko taifa lake. So sad
 
Wew unapata faida gani kupitia jeshi lako
 
wa tanzania tatizo sijui hawajui maana uoga sio ila ruanda anamuogopa sanaa mtanzania sababu anatujua moto wetu ila hajui tutamfanyaje wanyaruanda wote waliopo tanzania wanajulikana wakibisha tu tokomeza ujangili inarudi kwa mtindo mwingine
 
Wewe jeshi linakusaidia nini wakati huna ajira?
Hii ndiyo changamoto nyingine wapinzani Africa bado tunayo; tunadhani kazi ya serikali ni kufanya kila kitu kwa ajili ya wananchi huku wananchi wamelala.

This is why nchi nyingi upinzani ukichukua nchi, baada yq muda fulani mambo huwa worse na baadaye huondolewa madarakani; why? Kwa sababu wapinzani huoverpromise ama huchukilia mambo poa, running a country is never easy (Muulize Ruto, Mnangagwa, Chakwera, na wengine)

Wenzetu walifanikiwa kuwaambia wananchi ukweli; mfano JF Kennedy qliwaambia “Kabla hujajiuliza serikali imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini serikali”. Unategema serikali inipe ajira???? No way ni kazi yangu kupambana kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…