Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Habari wakuu, uzi ni mzuri ila naomba kuuliza maswali juu ya huu uzi.

1. Ikiwa ukawa na hizo power zote zinajibu kusudi la binadamu hapa duniani au ni ajili ya kucontrol nature basi?
2. Hizo nguvu zina majibu ya life after death? ikiwa hazina majibu naona zina limitation.
3. zina leta majibu juu ya ulimwengu na uumbaji? au bado hazina majibu hayo
4. Lucid Dreams ni nini?
5. kwanini njia hizo zinabaki kuwa siri, kwann zisifundishwe kila mmoja akazijua
6. ikiwa power ipo within, je unaweza kujitibu magonjwa kama figo, tb,kisukari, ukimwi kwa kutumia nguvu hizo?

Maswali mengineyo yatakuja na majibu ya wadau hapa jukwaani, asanteni
 
Ila Mimi nina nguvu zaidi na huwa ninapokuwa nasoma sana biblia na kusikiliza nyimbo za dini na kuzama kwenye maombi ,nakuwa na nguvu kubwa sana,naweza kumtazama mtu na kumwambia mambo anayopitia na kumwambia hivi na huwa natabiri mambo mengi na huwa ni ya kweli maana Huwa nafuatilia na kupata majibu

Na uwezo wa kuona kitu mbele na kufika nakuta ni kweli ,na naweza kupita sehemu mbaya zaidi na nisipatwe na kitu maana nguvu nilizonazo Huwa kubwa zaidi.

Kipindi nikiwa mdogo nilikuwa naona mambo makubwa sana

Nilishawahi kupanda gari na watu wabaya baada ya kuamka mapema kwenda kazini na baada ya kuja kushtuka na kuangalia saa vzr ilikuwa ni saa 7 usiku na nilipoingia kwenye Ile daladala wote waliinama chini wote na hata niliposhuka nilimpa dereva ela alikataa kupokea na konda hakwepo kwenye Ile daladala.walikwepo wanawake na akina baba na Mimi tu ndo sikupata Siti mle na mda wote mpaka nashuka walinamisha vichwa chini mwisho nikashuka na wao wakaendelea na safari zao,na baada ya kushuka nikajua hawakuwa watu wazuri,

Kwa hiyo Kuna mengi sana na Mimi kujihisi na kuelewa kuwa nina kitu Fulani kikubwa sana
 
Binafsi nimekuwa nikikutana na namba inayojirudiarudia mara kwa mara. Mfano naweza nikawa nipo mahali nimetulia nikisema nitoe simu mfukoni jicho likienda kwenye saa hukutana na Dakika 11 yaani kama ni saa 5 basi dk 11 km saa 9 Dk 11

Hii imekaaje?
Universe inajiendesha yenyewe. Najua huez rudisha majibu ila iyo ni message labda" Hi " kujibu ndo hatujui
 
Ila Mimi nina nguvu zaidi na huwa ninapokuwa nasoma sana biblia na kusikiliza nyimbo za dini na kuzama kwenye maombi ,nakuwa na nguvu kubwa sana,naweza kumtazama mtu na kumwambia mambo anayopitia na kumwambia hivi na huwa natabiri mambo mengi na huwa ni ya kweli maana Huwa nafuatilia na kupata majibu

Na uwezo wa kuona kitu mbele na kufika nakuta ni kweli ,na naweza kupita sehemu mbaya zaidi na nisipatwe na kitu maana nguvu nilizonazo Huwa kubwa zaidi.

Kipindi nikiwa mdogo nilikuwa naona mambo makubwa sana

Nilishawahi kupanda gari na watu wabaya baada ya kuamka mapema kwenda kazini na baada ya kuja kushtuka na kuangalia saa vzr ilikuwa ni saa 7 usiku na nilipoingia kwenye Ile daladala wote waliinama chini wote na hata niliposhuka nilimpa dereva ela alikataa kupokea na konda hakwepo kwenye Ile daladala.walikwepo wanawake na akina baba na Mimi tu ndo sikupata Siti mle na mda wote mpaka nashuka walinamisha vichwa chini mwisho nikashuka na wao wakaendelea na safari zao,na baada ya kushuka nikajua hawakuwa watu wazuri,

Kwa hiyo Kuna mengi sana na Mimi kujihisi na kuelewa kuwa nina kitu Fulani kikubwa sana
😂😂😂😂😂
 
Mkuu Utali, you have the powers!. Amini usiamini, anapogeuka na kukutazama, powers zako zinamconquer, ukimtuma mhudumu na kumpa number yako ampe wakati akienda washroom, anaweza kukupigia pale pale na kama yuko na mtu mtu tuu asiyenampango, huo mzigo unajibebea siku hiyo hiyo na unaliza kila kitu!.

Hizo powers za kupata kila unachokitaka ni "will powers" na hiyo ndio siri ya mafanikio ya karibu matajiri wote!, inaitwa "uthubutu wa kuamini unaweza!'. Utaweza vipi, au utapata vipi sio issue, ukishaamini, powers zina open up njia zote!. Wakati powers hizo zikifanya kazi kukuletea mafanikio, shetani naye na nguvu zake za giza hachelewi kukupa majaribu, watu wenye kijicho, husda na wivu, watatataka kukukwamisha hata ikibidi kufifisha nyota yako, ili wao ndio waisafirie!, kamwe hawawezi kuzuia rizki, bali wanaweza tuu kuichelewesha!.
Pasco.
Najiona Mimi kabisa kwenye hii statement, sema kwakuwa nilikuwa sijafahamu lolote hapo mwanzo nilikuwa najishangaa sana inawezekana vp hii? Ilikuwa kila jambo nikili-wish tu lazima litokee kama nilivyolitarajia pasipo kujali mazingira. Nilipoanza kuwasimulia watu tu, mambo yangu yalianza kuniharibikia nikapigwa vichomi vya kutosha. Kupitia jukwaa hili nimepanua sana ufahamu wangu. Pascal Mayalla Mshana Jr Rakims Thread zenu mbalimbali zimekuwa baraka sana kwangu. Baada ya kuanza kuzifatilia nimeanza kuona matokeo CHANYA na kujitambua. Mungu awabariki sana[emoji120] kwa moyo wa kutoa mlicho nacho bila kujali kuwa ninyi mlitumia pesa na muda wenu mwingi kupata haya mnayoyafundisha kwenye jukwaa hili.
 
Interesting.

Ngoja na mimi niendelee kusoma vitabu. nilishaanza na teaching of Buddha kina mafundisho mazuri kuhusu "enlightment"
soon nitanunua hicho The power of your subconscious Mind, infact a few months ago kuna rafikiangu tulienda pamoja bookshop akanunua akaniambia ni kizuri
Kusoma tu bila practice mkuu haitisaidia kitu. Nisawa sawa na aliyesomea (VETA) ufundi makanika bila practice huwezi mfananisha na makanika wa mtaani ambae hajaingia darasani. Ni vizuri kusoma lakini na kufanya practical ni bora zaid.
 
Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen.
Energy medicine
- Healing by channeling a form of energy.
Psychic surgery - Removal of diseased body tissue via an incision that heals immediately afterwards
Divination - Gaining insight into a situation via a ritual.[SUP][7]
[/SUP]Clairaudience - receiving messages in thought form from another frequency or realm. It is considered a form.

Baadhi ya waganga ni kweli wananguvu hizi, ila wengi zaidi ni wasanii, wameishajua the powers anazo mgojwa, anachofanya ni make belive kuwa kaoteshwa, anachokupa is nothing, wala hakitibu!, kinachotibu ni imani yako!, kama kikombe cha Babu!. Anayeponyesha sio mganga, bali mwili unajitibu na kujiponya kwa nguvu zako mwenyewe, anachofanya yeye ni kukusaidia tuu wewe kufungua milango ya nguvu zako kufanya mambo!.
Pasco.
Hii mkuu Mimi niliwahi kuishuhudia bila kusimuliwa. Kipindi cha nyuma tulikuwa tumepanga nyumba moja mitaa ya uswazi. Kuna jamaa mmoja baada ya kuona mambo kiuchumi kwake yamekuwa tight akaanza kusaga majani ya mpapai na kuponda ponda mikaa hadi inakuwa unga. Then akaongea na marafiki zake ambao walikuwa ni madalali wa vyumba kuwa wamtafutie wateja kwa kuwaambia na wao atakuwa akiwagawia fungo kidogo. Jamaa alianza kama utani tu, watu wakaanza kuja lakini pamoja na kuwapa majani ya mipapai na unga wa mkaa watu walikuwa wanapona. Walichokua wanakifanya wale makuwadi wake wa kumletea wateja ni ku make believe tu Kwa wale wateja ambao walikuwa wakimletea. Wanajifanya kuwa wao walikuwa na hali mbaya jamaa huyo akawaokoa. Mteja anapopigwa Testimony yakutosha wanakuja wameiva kiimani. Menginge sitaki kumuongelea sana. Haya mambo ya Imani ni ya kuacha tu
 

"Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?"​

Kama mtu anakuwa na hizo nguvu na hajitambui, atatambuaje kama hafanyi miujiza? Pia, atatambuaje kama anazo?
 
Mkuu Nyenyere, kiukweli naunga mkono hatua ya mode kuingilia kati kwa sababu ukifika mahali pabaya pa kukashifu dini na imani za Wengine.

Mfano wewe ukiwa Mkiristu unaamini Yesu ni Mungu, its not fair kwa asiyeamini kuwa Yesu ni Mungu aje humu na kusema Yesu sii Mungu!. Kama wewe ni muumini wa imani fulani, itoshe kuishikilia imani yako bila kushambulia imani za wengine!.

Kwenye uzi huu mimi nafundisha watu kuhusu powers from within bila kulazimisha watu wa dini yoyote. Wewe kila ukija humu unanishupalia mimi ni mpinga Kristo, ninacho kueleza wewe na waumini wengine kama wewe, hizi powers zimekuweko tangu kabla ya Ukristu. Hindu wanazifundisha kiaka 300,000 kabla ya Kritu, its not fair kulazimisha hizi powers ni za Kristu pekee aliyekuja miaka 2013 tuu iliyopita!. Kama meditation imekuwepo miaka 300,000 kabla ya Kristu, Kristu nae kaja kaikuta na ukitumia sana tuu, nakuuliza jee unajua Kristu alikuwa wapi na alifanya nini kati ya miaka 12 hadi 30?, hujui unalazimisha kile tuu ukijuacho!. Nimekuwekea vitabu pale juu husomi unang'ang'ana na kitabu kimoja tuu cha Biblia, unakuwa huwatendei haki wengine wote wasioamini katika Kristu.

Nakuhakikishia hizi powers zipo indeoendent ya dini yoyote, zile secret society zote wanazijua ila wanafanya siri ili wafaidike wenyewe pekee!.

Nakushauri stick to unachoamini bila kuwaingilia wengine na kulazimisha unachoamini wewe!.
Please!.
Very Strength Intelligent
 
Mkuu Manning, you have the powers to make things happen!.Hizi powers ziko za aina mbili , positive na negative , ingekuwa ingekuwa zinafuata principle ya nature,positive na negative ingeattract!, powers hizi ni contrary to nature, positive na negative zina repeal Positive powers ni nguvu za kutenda mema na negative ni nguvu za kutenda maovu. Kinachowafanya hao watu wakuogope ni kuwa mwili wako una radiate powers mbao wanakuogopa nao wana opposite powers!.


Hiyo ya kuwapata kila wasichana utakao watokea, ni nguvu hizo will powers za lolote utakalo linakuwa!.Wowote utaawasaidia wanafanikiwa!. Unachopaswa kufanya sasa, kwanza ni kujitambua kuwa you have the powers za kufanya kill kitu!, Kwa vile umekuwa na hizo powers kwa muda mrefu bila kujitambua , matokeo yake zimekuwa wasted na under utilized!.Kutoka sasa zitawale nguvu hizo, ukizielekeza direction mfano kama unatumia coralla huku unapeda Benz au Vogue na unajiona huna uwezo wa Benz au Vogue, then weka nia ya dhati kwa kudhamiria kuwa utendesha Benz au Vogue na utajenga ghorofa, umekuwa boss, utaishi top life, vyote vitakuja!,

Hilo la kutokewa na baba , death is not a big deal, it's only a change of life form physical to spiritual yaani amehama toka ulimwengu wa mwili sasa anaishi ulimwengu wa roho the spiritual world ambako ndiko mbinguni au peponi kwenye ulimwengu wa pepo. Anapokutokea, anakutokea kweli hivyo msikilize kwa makini na zingatia sana maelekezo yake !.

Angalizo: Kwenye ulimwengu wa pepo, zile positive na negatives zipo, yaani kuna good spirits na bad spirits.
Nitaendeea, na take break follow Isidingo ikiisha narudi kumalizia.
Pasco
Asante Sana mkuu @pasical mayala, ushauri wako nitaufanyia kazi naona umelenga mulemule
 
Wanabodi,

"Powers" ndicho kitu kikubwa kabisa duniani kuliko kitu kingine chochote! . God is Power, yaani Mungu ni nguvu, hakuna kitu chochote kinachoonekana kwa macho kumhusu Mungu, bali ni powers zake tuu za mambo Mungu anayoyafanya ndizo zinazoonekana.

Powers ndio kila kitu. Watu wote wenye nguvu ni powers, spiritual powers kwa watu wa imani, political powers kwa wanasiasa, economical powers kwa matajiri, social powers kwa wenye vipaji mbalimbali. Everything thing is about powers na mafanikio yoyote katika kila kitu ni jinsi watu wanavyo master hizi powers.

Kitu chenye nguvu kabisa katika mwili wa binadamu ni power ambayo ni nguvu inayoitwa "Will Powers" ambayo kila binadamu, anazaliwa nayo, ila wengine wanabahatika kwa nguvu hizo kujionyesha bayana, huku wengine wengi wakiwa nazo zikiwa zimejificha bila kujijua kuwa wanazo hizo nguvu. hutumia.

Hatua ya kwanza ya kufungua nguvu hizi ni "imani" kuamini kuwa "you have the powers" and that "you can do anything!", or "you can be anybody". Kuamini Mungu, Yesu, Mtume, Allah, Roho Mtakatifu, Bikira Maria, Watakatifu, Wachungaji, Wahubiri, Baba Mtakatifu, Sangoma, Sheriffu, Mlingotini, Chini ya Mti, Chini ya Mbuyu, Mlimani, Pangoni, Kisimani, Mtoni, Ziwani, Kwa Mganga, Vitabu Vitakatifu etc, ni njia rahisi ya kuanzia kufungua milango ya "higher power" to open up your doors for powers from within!" to act on you for you!.

"I know I can, be what I wanna be!"

Hii ni fursa kwa wewe kujitambua, kuzitumia powers ulizo nazo, kubadili maisha yako!,
NB. Hili ni muhimu sana kuzingatia, mzingi mkuu wa mada hii ni kujitambua, self awareness, kwa vile nimesema Mungu ni Nguvu za kutenda mema, God is Powers of Lightness, na Shetani ni nguvu za kutenda maovu, is powers of darkness, the dividing line between hizi powers ni very thin. Shetani is very clever, ni imposter, ana penda kuji disguise as Mungu, hivyo kuna mambo mengi ikiwemo miujiza ya uponyaji inayofanyika kwenye dunia hii, huku watu wakidhani ni kazi ya Mungu, kumbe sio kazi ya Mungu, ni kazi ya shetani. Hivyo be very careful.

Karibu tujadiliane!.

Paskali
Na mbaya zaidi kaanza kuwa "prophet of doom" he always wishes doomsday to come in Tanzania for his devilish foresight about someone the "damned"

Na wote tuseme Amina ,
Mkuu The imp, kuna kitu umekisema hapa, Pascal Mayala kazeeka haoni mbele tarehe 25 mwezi 9, mwaka 2019 kunihisu mimi, halafu kilikuja kutokea kweli!. Nikisoma hapa ulisema nini kunihusu na nikipima na kilichokuja kutokea, kiukweli, naanza kujiogopa!.
Nakupitisha kwenye baadhi ya mabandiko yangu uangalie tarehe ya mabandiko hayo, nilisema nini lini na nini kimekuja kutokea kuhusu hicho nilicho kisema!.

The most powerful thing in this world is the power of will!.
Japo kuna msemo kuwa kauli huumba, kumbe kiukweli, kinachoumba sio kauli, bali the will ikiyoko ndani ya hiyo kauli.
If the will is strong enough, you can wish anything and it will happen or materialize!

P
 
'the will ikiyoko ndani ya hiyo kauli.
If the will is strong enough, you can wish anything and it will happen or materialize!' naendelea kufuatailia taratiiibu...
 
Ngoja niongelee kitu kimoja km mfano...

kuna kitu kimoja kinashangaza inatokea sana mashuleni na vyuoni.
Unakuta mtu anasoma sana halafu kwenye mitihani anafeli halafu kuna huyu yeye hashiki kitabu mpaka siku za mitihani alafu anakuja kufaulu masomo vzr tu. Hapa huwa inanishangaza sana
 
Nakubaliana kabisa na wewe Mkuu Pasco, kipindi fulani katika maisha yangu nilitamani sana kujifunza uchawi mwenye tija, nikajikuta nimeangukia kwenye temple moja south Africa iliyokuwa inafundisha Buddhism Yoga meditation na supernatural powers

Yalikuwa ni masomo magumu ya ajabu na yenye kushangaza kwa jinsi yake, kwa ufupi ni kwamba hakuna chenye nguvu duniani kama bongo(mind) ya binadamu, na tunachokitumia katika mind zetu ni theluthi tu ya kile chote kilichopo

Tunafundishwa kuwa kuna 5senses, lakini Zipo 8 ambapo mtu ukiweza kuzifanyia kazi utafanya maajabu mengi , mind ya mwanadamu imejazwa takataka nyingi mno, illusions na dillusions ukiweza kuziondoa kwenye bongo yako ukabaki na pure and stable mind unakuwa mtu mwingine kabisa mwenye maono na nguvu za ajabu mno

Medition ni kitu cha Mwanzo kabisa kuendea kwenye kudevelop supernatural powers, nilifanya meditation zote, chanting, yoga nikiwa vegitarian kwa miaka mitano nikajikuta nabadilika nikaogopa nikaacha , kwakuwa niliona wazimu kuna mafundisho yanapingana waziwazi na imani yangu

Nimeipenda mada yako sana. Nakaribisha maswali na ufafanuzi nimeisoma sana Buddhism, Taiosm, Satanism na Kshna consciousness

Mwenye kupenda hii mambo atafute kitabu kiitwacho Analects: Way and Its Power.
Mshana kama Mshana.
 
Mkuu mayenga, mimi nina
Telepathy
- Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.

Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.

Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!.

Matumizi ya nguvu hizi yalikuwa ni kwa "kata funua tuu!, mpaka nilipokutana na dada mmoja aliyekuakisoma Jangwani, ndipo akanieleza kuhusu uwezo huo, na ninachokifanya ni abuse of power! akanionya nikiendelea hivyo matokeo yake yatakuwa nini, ndipo nikabadilika!.

Ila mpaka leo, kuna mtu nikimfikiria tuu, anatoke, au nafika mahali na kuambiwa, una maisha marefu, sasa hivi tulikuwa tunakuzungumza!. Au uko mahali unatembea, njia nyembamba, unataka kupishana na mtu, ukienda upende ule naye anakuja huko, ukirudi huku naye anarudi huku hadi mnataka kugongana unaamua kusimama mpishane!.

Pia nina Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen. kidogo. Kuna mambo huwa naota yanakuja kutokea!. Nina kitu kinaitwa "intuition!" yaani kabla sijafanya jambo, unapata hisia this is not gona work!, au unakutana na mtu anakuzimikia sana for real, wewe unaona its not for real!. Au ndani ya ndoa, ikitokea wife ame cheat, utajua!, huwezi kuuliza kwa sababu huna ushahidi, ili mtu akicheat, ujue atacheat tena!, nilianza kufanya kazi ya kukusanya ushahidi nikathibitisha!, na nilisamehe kwa kujifikiria ni mara ngapi nilipitia wake za watu!, wengine wakiwa ni wake wa marafiki zangu kabisa!.

Pia naweza kufanya Aura reading - Perception of the energy fields surrounding people, places, and things kwa kiwango kidogo!, nikikutana na mtu for the first time, I can tell huyu ni mtu mwema au ni mtu mbaya!. Hii nimeiwea kwa practice kutoka kwenye net.
Retrocognition - Perception of past events imeishanitokea mara kadhaa, naweza kufika mahali for the first time, na kujiona I have seen this place before ila sikumbuki ni wapi!, au nimekutana na mtu for the first time, na kujiona I've seen him before sijui ni wapi!, hii inaitwa De-ja-vu kwa Kifaransa!.

Nimesoma sana vitabu vingi vya mambo haya, hivyo naangalia uwezekano wa kufungua more evenues kwa meditation ila kwa njia ya natural sio kupitia secret societies kama Freemasons, Illuminati au Rosecrusians. Hawa jamaa ndio ma master wa haya mambo ila wanafanya siri!. Matajiri wengi wanatumia powers hizi kupata utajiri iwe ni kwa njia za sala kupitia makanisa ya wokovu, waganga wa kienyeji, kujiunga na vikundi kama freemasons etc, all and all its works of powers!.
Pasco.
So mkuu Pascal, unamaanisha hawa secret societies wanajua siri zote za Ulimwengu huu?
 
Back
Top Bottom