Mkuu mayenga, mimi nina
Telepathy - Transfer of thoughts or emotions, kwa kiasi kidogo!. Zamani nikiwa kijana mdogo nikisoma sekendari ya Tambaza na baadae Ilboru, ilitokea kuna vibinti fulani vya Kisutu na Jangwani, nilivitazama kwa kuvihitaji tuu, nikaja kuvipata!.
Ikawa nikienda kwenye party, nikimsimikia binti, nikimtazama kwa concentration huku nikisema kimoyo moyo, nakuhitaji!, yule binti, atageuka na macho yakigona tuu, nitatoka nje, atanifuata!, tutazunguka tuu mahali popote penye faragha!, nitamaliza shida zangu na kurudi kwenye party!.
Nilipomaliza na kujiunga JKT, kule ikawa balaa!, kila macho yanapoona, moyo ukipenda, napita na sikosi!.
Nilipoanza kazi, nikajikuwa huwa nakuwa MC, nikawa nikienda kwenye sherehe mbalimbali, naondoka na mtu!. Hata nikiwa kwenye Daladala, nikizimika mahali, natazama tuu, nikishuka naye anashuka!.
Matumizi ya nguvu hizi yalikuwa ni kwa "kata funua tuu!, mpaka nilipokutana na dada mmoja aliyekuakisoma Jangwani, ndipo akanieleza kuhusu uwezo huo, na ninachokifanya ni abuse of power! akanionya nikiendelea hivyo matokeo yake yatakuwa nini, ndipo nikabadilika!.
Ila mpaka leo, kuna mtu nikimfikiria tuu, anatoke, au nafika mahali na kuambiwa, una maisha marefu, sasa hivi tulikuwa tunakuzungumza!. Au uko mahali unatembea, njia nyembamba, unataka kupishana na mtu, ukienda upende ule naye anakuja huko, ukirudi huku naye anarudi huku hadi mnataka kugongana unaamua kusimama mpishane!.
Pia nina Precognition,
premonition and
precognitive dreams - Perception of events before they happen. kidogo. Kuna mambo huwa naota yanakuja kutokea!. Nina kitu kinaitwa "intuition!" yaani kabla sijafanya jambo, unapata hisia this is not gona work!, au unakutana na mtu anakuzimikia sana for real, wewe unaona its not for real!. Au ndani ya ndoa, ikitokea wife ame cheat, utajua!, huwezi kuuliza kwa sababu huna ushahidi, ili mtu akicheat, ujue atacheat tena!, nilianza kufanya kazi ya kukusanya ushahidi nikathibitisha!, na nilisamehe kwa kujifikiria ni mara ngapi nilipitia wake za watu!, wengine wakiwa ni wake wa marafiki zangu kabisa!.
Pia naweza kufanya Aura reading - Perception of the energy fields surrounding people, places, and things kwa kiwango kidogo!, nikikutana na mtu for the first time, I can tell huyu ni mtu mwema au ni mtu mbaya!. Hii nimeiwea kwa practice kutoka kwenye net.
Retrocognition - Perception of past events imeishanitokea mara kadhaa, naweza kufika mahali for the first time, na kujiona I have seen this place before ila sikumbuki ni wapi!, au nimekutana na mtu for the first time, na kujiona I've seen him before sijui ni wapi!, hii inaitwa De-ja-vu kwa Kifaransa!.
Nimesoma sana vitabu vingi vya mambo haya, hivyo naangalia uwezekano wa kufungua more evenues kwa meditation ila kwa njia ya natural sio kupitia secret societies kama Freemasons, Illuminati au Rosecrusians. Hawa jamaa ndio ma master wa haya mambo ila wanafanya siri!. Matajiri wengi wanatumia powers hizi kupata utajiri iwe ni kwa njia za sala kupitia makanisa ya wokovu, waganga wa kienyeji, kujiunga na vikundi kama freemasons etc, all and all its works of powers!.
Pasco.