Asante Lady, kunijulisha, nilikuwa sijui, ila sasa kupitia wewe nimejua!.
Pasco.
Mkuu Schiendler, sii kweli kuwa "psychic powers" ni nguvu za giza!, hizi ni nguvu za Mungu na alitupa ile siku anatuumba!, ila zinaweza kutumika vizuri kwa kumtumika Mungu kufanya wema, uponyaji, na kuleta mafanikio, au zikatumika vibaya kama kufanya uchawi na kuleta maangamizi, hivyo kumtumikia shetani!.
Pasco.
Mkuu Juve, nimeisoma kidogo hiyo "holographic healing", haswa ile inayofanywa na yule mdada Kara!, inatumia the "inner power", tatizo kwangu ni kitendo cha huyo dada kutumia "claivoyance "talking to the dead" ili kujua chanzo cha tatizo, na pia anatumia "hypnotisim" kutibu, kama reiki, hivyo naihesabu kama yoga, meditation, dianetics, etc, hoja yangu ya msingi bado inasimama kwenye tiba zote za imani, kuwa nguvu za uponyaji, zinatoka ndani yako, ndio maana ukizungumza tuu na huyo muombaji kwenye simu, kwa kumsikiliza kwenye redio au hata kwa kumuona tuu kwenye TV.Mkuu Pasco,unafahamu nini kuhusu "holographic healing"?
Mkuu Juve, nimeisoma kidogo hiyo "holographic healing", haswa ile inayofanywa na yule mdada Kara!, inatumia the "inner power", tatizo kwangu ni kitendo cha huyo dada kutumia "claivoyance "talking to the dead" ili kujua chanzo cha tatizo, na pia anatumia "hypnotisim" kutibu, kama reiki, hivyo naihesabu kama yoga, meditation, dianetics, etc, hoja yangu ya msingi bado inasimama kwenye tiba zote za imani, kuwa nguvu za uponyaji, zinatoka ndani yako, ndio maana ukizungumza tuu na huyo muombaji kwenye simu, kwa kumsikiliza kwenye redio au hata kwa kumuona tuu kwenye TV.
Yesu alipofanya muujiza, hakuhitaji kulipwa hata senti tano!, sasa hawa wafanya miujiza wa kulipwa, wananitatiza kidogo, wanawaibia watu pesa zao, kwa kujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za uponyaji, badala ya kuwaeleza ukweli watu kuwa nguvu za uponyaji zimo ndani yao!.
Pasco.
Mkuu Schiendler, haya yote usemayo, ni ukweli mtupu!, japo pia nimekushtukia kiana, una "il motive" ndani yako, kutaka kuonyesha hata haya mafundisho mimi ninayoyaweka humu, ndio mafundisho haya ya kupoteza!.( 1 TIMOTHEO 4:1 ).
Basu Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.
( 2 TIMOTHEO 4:3-5 )
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
( 2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.
Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni wapandisha pepo. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani iwe dhahiri kwa mfano wetu tunavyofanya katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.
Kazi tuliyoitiwa ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza, je, wana wenu huwatoa kwa nani?. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?
Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.
Hivi mkuu Pasco, unywaji wa pombe ni kizuizi cha hizi nguvu kuprevail? Vingi nilishasema tangia kurasa za mwanzo, ila nikinywa pombe hata kuota sioti nashtukia asubuhi hiyo au kushtuka tu usiku kama nina kiu au haja ndogo imenibana.
Wakuu fyddell na stephot, jibu ni straight forward, jiulize function ya pombe kwenye mwili wetu ni nini?, kazi ya pombe katika mwili wa binadamu ni moja tuu, nayo ni kupumbaza akili!. Kwa hapa naomba ku declare interest mimi Pasco wa jf, ni mnywaji mzuri wa pombe za aina zote, ukiondoa bia!, kwa sababu huu ndio muujiza wa kwanza wa Yesu pale kwenye harusi ya Kana!.
Mkuu Schiendler, kwa mujibu wa michango yako humu, unaonyesha wazi uko deep, na hiyo psychic attack unaijua fika!.Pasco: What is a Psychic Attack?
Manangwa Pasco:Mkuu Schiendler, kwa mujibu wa michango yako humu, unaonyesha wazi uko deep, na hiyo psychic attack unaijua fika!.
Psychic Attacks, na hapa What is a Psychic Attack?
Pasco
Utabiri wa nyota unaitwa astrology na kusoma viganya kunaitwa palmistry, hizi ndizo silaha mbili kuu zinazotumiwa na wanajimu na wapiga ramli!. Kwa mujibu wa imani ya Kikristu, kufanya hayo ni dhambi!. Kama nilivyoeleza tangu mwanzo wa uzi huu, matumizi ya hizi powers ni over and above Christianity. Bible imepiga marufuku mambo haya!. Mimi nimeishi kidogo India nimesoma kidogo maandiko ya dini ya Hindu na Budhiism, kiukweli ukizama humo ndani, unakuta Christianity ni almost nothing!, na Bible ni cha mtoto, ulifanya comparison, unajikuta ukistick na knowlege kutoka Bible pekee, then utajiona you know so much, ila in reality kwa kuitegemea bible pekee, kiukweli kabisa unakuwa you know so little!.Manangwa Pasco:
Kabla sijaweka majibu au nyongeza ya posti/majibu yako, ngoja niongezee maswali haya kwanza.
Mtabiri wa nyota na kusoma viganja vya watu vya mikono na kuwaeleza hivyo wanavyosema ameona, huyu mtu ana tofauti gani na MPIGA RAMLI?
Je, unajimu unahusiana na majini au ni nguvu ya Mungu aliyo wapa viumbe vyake?