Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?

Mkuu Schiendler, sii kweli kuwa "psychic powers" ni nguvu za giza!, hizi ni nguvu za Mungu na alitupa ile siku anatuumba!, ila zinaweza kutumika vizuri kwa kumtumika Mungu kufanya wema, uponyaji, na kuleta mafanikio, au zikatumika vibaya kama kufanya uchawi na kuleta maangamizi, hivyo kumtumikia shetani!.
Pasco.

Ndugu Pasco:

Biblia inakataza kabisa mambo yafuatayo spiritism, mediums, the occult, and psychics (Leviticus 20:27;Deuteronomy 18:10-13)., Zaidi ya hapo, vile vile Mungu anakataza yafuatayo Horoscopes, tarot cards, astrology, fortune tellers, palm readings, and séances.

Pasco, please be informed that these diabolical practices are based on the concept that there are
gods, spirits, or deceased loved ones that can give advice and guidance. These "gods" or "spirits" are demons (2 Corinthians 11:14-15). The Bible gives us no reason to believe that deceased loved ones can contact us. If they were believers, they are in heaven enjoying the most wonderful place imaginable in fellowship with a loving God. If they were not believers, they are in hell, suffering the un-ending torment for rejecting God's love and rebelling against Him.

You must be careful. The difference between Godly and Satanic is more subtle. For example:

Divination- Bad
Prophesy- Good

Mediumship- Bad
Receiving messages from angels- Good

Speaking with the dead- Bad
Praying to the (dead) saints- good

Spirit guides- Bad
Guardian angels- Good

Do you see the distinct between God and Satanic Power? It is conspicuous and vivacity to those who comprehend God.

 
Hivi mkuu Pasco, unywaji wa pombe ni kizuizi cha hizi nguvu kuprevail? Vingi nilishasema tangia kurasa za mwanzo, ila nikinywa pombe hata kuota sioti nashtukia asubuhi hiyo au kushtuka tu usiku kama nina kiu au haja ndogo imenibana.
 
Mkuu Pasco,unafahamu nini kuhusu "holographic healing"?
Mkuu Juve, nimeisoma kidogo hiyo "holographic healing", haswa ile inayofanywa na yule mdada Kara!, inatumia the "inner power", tatizo kwangu ni kitendo cha huyo dada kutumia "claivoyance "talking to the dead" ili kujua chanzo cha tatizo, na pia anatumia "hypnotisim" kutibu, kama reiki, hivyo naihesabu kama yoga, meditation, dianetics, etc, hoja yangu ya msingi bado inasimama kwenye tiba zote za imani, kuwa nguvu za uponyaji, zinatoka ndani yako, ndio maana ukizungumza tuu na huyo muombaji kwenye simu, kwa kumsikiliza kwenye redio au hata kwa kumuona tuu kwenye TV.

Yesu alipofanya muujiza, hakuhitaji kulipwa hata senti tano!, sasa hawa wafanya miujiza wa kulipwa, wananitatiza kidogo, wanawaibia watu pesa zao, kwa kujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za uponyaji, badala ya kuwaeleza ukweli watu kuwa nguvu za uponyaji zimo ndani yao!.
Pasco.
 
Mkuu Juve, nimeisoma kidogo hiyo "holographic healing", haswa ile inayofanywa na yule mdada Kara!, inatumia the "inner power", tatizo kwangu ni kitendo cha huyo dada kutumia "claivoyance "talking to the dead" ili kujua chanzo cha tatizo, na pia anatumia "hypnotisim" kutibu, kama reiki, hivyo naihesabu kama yoga, meditation, dianetics, etc, hoja yangu ya msingi bado inasimama kwenye tiba zote za imani, kuwa nguvu za uponyaji, zinatoka ndani yako, ndio maana ukizungumza tuu na huyo muombaji kwenye simu, kwa kumsikiliza kwenye redio au hata kwa kumuona tuu kwenye TV.

Yesu alipofanya muujiza, hakuhitaji kulipwa hata senti tano!, sasa hawa wafanya miujiza wa kulipwa, wananitatiza kidogo, wanawaibia watu pesa zao, kwa kujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za uponyaji, badala ya kuwaeleza ukweli watu kuwa nguvu za uponyaji zimo ndani yao!.
Pasco.

nimekusoma vizuri kaka.Hapo kwa kweli hata mie huwa napata wakati mgumu.Nilichotaka kujua haswa ni ile dhana nzima ya sayansi ya holographic healing.Kwamba miili yetu inabeba continuous energy patterns ambazo zina information kuhusu jinsi mwili ulivyokuwa na ulivyo at the moment of diagnosis.Kwa hiyo kama kuna tofauti kati ya ulivyokuwa nyuma na ulivyo sasa,hapo kuna defect,kwa hiyo wanatumia chombo maalum chenye uwezo wa kuingilia zile waves za energy patterns ili zijipange kama mwanzo na hivyo kuufanya mwili kujitibu wenyewe.Kila sehemu ya mwili ina energy patterns zake ambazo zinabeba informations za kiungo husika.Kwa hiyo ukizisoma patterns hizo(Quantum hologram) unapata information za kiungo kilivyokuwa mwanzo hadi kilivyobadilika(defect ya ugonjwa),na kuziamuru patterns zirudi kama mwanzo na hivyo nazo zikikaa sawa kiungo kinapona ugonjwa wake hata kama ni cancer.Kwamba maana yake ni kwamba mwili wa binadamu una uwezo wa kujitibu wenyewe ila tu uwezo wa kiakili kucontrol hizo patterns zetu(meditation) umepungua kiasi kwamba tunahitaji hiyo external power kwa kutumia vifaa maalum kama hivyo kustimulate patterns.This is what is all about holographic healing kwa kutumia scientific quantum theories ambazo principle yake kubwa ni kwamba ulimwengu na yote yaliyomo ni holistic,yaani muunganiko wa vitu kimoja kimoja ambavyo vinategemeana na umoja wao ndio unaleta nguvu kuu,na kila kitu kimoja kimoja ukikichunguza ndani yake utakuta nacho kimeumbwa kwa muunganiko wa aina hiyo,kila kiungo kikiwa related na kingine,muunganiko huo ukiwa chini ya principles zinazoleta uwiano sawia(uniformity),umoja na utulivu katika utendaji ili kufikia malengo yake ambayo ndio consciousnes.Energy patterns ndio zinacoordinate hizi individual bodies zote according to principles.Hivyo kukiwa na ukiukwaji wa principles zinatoa information.Hapo ndipo tunapopata majibu ya maswali magumu kama kufanana kwa sayansi ya ukuaji wa mimea,binadamu,tabia kufanana,instincts,yaani ukichunguza universe yote imejaa viumbe vyenye uniformity na relativity ya ajabu ambayo inaonyesha kuwa kuna sababu ya uwepo wake na ni blueprint ya aliyeumba!kwa hiyo unapotaka kujua sababu ya jambo fulani ni lazima ujue mtandao mzima ambamo jambo au kitu kile kimo,how it relates to it's surroundings and "how it should relate".Ni kwa njia hii hizi holographic treatment zinafanya kazi,mwili mzima unakuwa diagnosed energy patterns,halafu tatizo linaonekana na kutatuliwa kwa kuziamrisha zirudi katika hali yake ya mwanzo na kiungo kinajiponya chenyewe.Kila kiumbe kina energy ndani yake sawa na kiwango cha mada iliyobebwa na kiumbe huyo na kuna very special relativity kati ya energy hizo na maumbile ya kiumbe hicho.Kujua base ya energy hizo(sijui ndio mnaita chakra) inasaidia kupata information zote juu ya maumbile yake na utendaji wake.Hii ndio Holographic healing nilikuwa nazungumzia.Sasa shida ipo kwa who possess this kind of technology?tunarudi kulee usikokupenda,teh teh,pole kaka usinung'unike sana ndio dunia ya ujasiriamali hii!You know what am i thinking mkuu Pasco,napata picha kwamba hizi ni ancient science and technologies ambazo kuna watu so powerful in this world walizificha for a special purpose na sasa wanarelease huku waki-dictate mambo ziwaletee desired outcomes.Huenda vilikuwa vitu vya kawaida enzi za akina Musa na Abraham,lakini somewhere along the road kuna powers zilivuruga wavelength yote na sisi tunapokea frequencies tusizozielewa teh teh!dunia ina mambo hii!bora ukae nyumbani ujilie bada lako kwa mlenda..ptuu!
 
Kuna jambo moja muhimu sana kulifanyia uchunguzi kuhusu elimu hizi hasa kwa wale wenye dini.Kujua lipi ni jema na lipi ni dhambi!kuna suala la kujua hizi nguvu,kuna suala la kumanipulate hizi nguvu,na kuna suala la kutumia hizi nguvu.Kinachoniumiza kichwa ni kwamba kwa mafundisho yetu ya dini,elimu kuhusu psychic powers ni dhambi kama mheshimiwa mmoja alivyonukuu kifungu hapo juu.Swali langu ni je,every kind of psychic powers ni evil au kuna aina fulani biblia inalenga?je,tafsiri ya biblia kama tunavyotafsiri ni sahihi?kama ni sahihi,my main question comes,kwa nini tumeumbwa na hizi powers?kuna mtu alinijibu kwamba hizi powers za shetani,does it mean shetani hukaa ndani yetu?manake kuna watu decent wanaexperience hizi nguvu ndani yao,how?kuna maswali magumu yalikuwa hayajibiki but since the introduction of this knowledge at least kuna vitu mtu unapata platform ya kuanza kuvijibu mfano miujiza ya Yesu na mitume wa zamani,"nataka pona",mtu anaamka tayari amepona,is it a new power from Jesus imemwangukia mtu ikarekebisha kasoro za mwili wake,au tayari kuna scientific base Mungu aliweka ndani yetu,kutokana na dhambi zinavurugika,and all Jesus(creator) did ni ku-send again sound wavelength zake(neno) kwenda kupangilia tuu energy patterns zikae sawa na command ya kwanza ya neno wakati uumbaji unafanyika in the beginning?unajua sibishi lakini nataka tuwe na reasoning kwa kila jambo as long as lipo kweli,..sijui naeleweka jamani?aargh!
 
( 1 TIMOTHEO 4:1 ).
"Basu Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani". Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.
( 2 TIMOTHEO 4:3-5 )
"Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo".
( 2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.

Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni" wapandisha pepo". Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani iwe dhahiri kwa mfano wetu tunavyofanya katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.


Kazi tuliyoitiwa ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo". MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza," je, wana wenu huwatoa kwa nani?". Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?
Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.
 
Haya mambo tangu niyaone kwa mara ya kwanza...nimekuwa nikiendelea na kutafuta ukweli wake na hatimaye nimepata picha na video nyingi juu ya hili.

Check na hii picha hapa.
 

Attachments

  • 1393644804637.jpg
    1393644804637.jpg
    34.1 KB · Views: 255
Dah mambo mengi sana huwa yananipita jamani

nimeipenda hii mada nimeishia page 5 nitahakikisha naisoma yooote thank you Pasco

unaelezea vituhadi raha yaani U can feel au ndio nimeanza kumeditate lol unavuta pic ya jinsi mambo yalivyo.

Natamani nikufaham zaid nahisi unajua mambo mengi saaaaaana
 
( 1 TIMOTHEO 4:1 ).
“Basu Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.
( 2 TIMOTHEO 4:3-5 )
“Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.
( 2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.

Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani iwe dhahiri kwa mfano wetu tunavyofanya katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.


Kazi tuliyoitiwa ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?
Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.
Mkuu Schiendler, haya yote usemayo, ni ukweli mtupu!, japo pia nimekushtukia kiana, una "il motive" ndani yako, kutaka kuonyesha hata haya mafundisho mimi ninayoyaweka humu, ndio mafundisho haya ya kupoteza!.
Ukweli ni kuwa, mimi nafundisha watu wajititambue, wajijue, wana Mungu ndani yao!, hivyo hawawezi kupotea!.

Dini nyingine zinawazuia waumini wake wasiijue kweli hii, ili waendelee kuwapoteza na kuwapotezea!.

Wako baadhi ya wahubiri wenye nguvu, wanaotumia nguvu za giza kufanya ishara, uponyaji na upungaji mapepo! lakini sio wa Bwana!.

Yesu aliishawataja watu hawa kuwa "Watakuja watu, watatoa mapepo kwa jina langu "Kwa Jina la Yesu!" lakini sio wangu!".
Pia Bwana wetu Yesu Kristo, alitufundisha namna ya kuwatambua kuwa "utawatambua kwa matendo yao!"
Pasco
 
Hivi mkuu Pasco, unywaji wa pombe ni kizuizi cha hizi nguvu kuprevail? Vingi nilishasema tangia kurasa za mwanzo, ila nikinywa pombe hata kuota sioti nashtukia asubuhi hiyo au kushtuka tu usiku kama nina kiu au haja ndogo imenibana.
Mkuu Pasco mimi swali langu lina fanana na la ndugu fyddell ,tafadhali tunaomba majibu yako.
Wakuu fyddell na stephot, jibu ni straight forward, jiulize function ya pombe kwenye mwili wetu ni nini?, kazi ya pombe katika mwili wa binadamu ni moja tuu, nayo ni kupumbaza akili!. Kwa hapa naomba ku declare interest mimi Pasco wa jf, ni mnywaji mzuri wa pombe za aina zote, ukiondoa bia!, kwa sababu huu ndio muujiza wa kwanza wa Yesu pale kwenye harusi ya Kana!.

Naamini kunywa pombe kwa kiasi sio mbaya, kunauuburudisha mwili, kukupatia relaxation na uwezo wa kuufurahisha mwili ila kunapumbaza akili. Hzi powers ziko stored kwenye subconscious mind, hivyo kitendo cha kuupumbaza ubongo kwa kitu chochote, kunazifungia kabisa hizi nguvu na kuzifanya au zilale zaidi, au body iki relax, hizi nguvu huweza kuamka zaidi!, ndio maana kuna baadhi ya watu, akivuta kidogo bangi, au kupata kidogo (pombe), ndipo huweza kuongea mambo makubwa au kufanya makubwa!. Au baadhi ya madaktari wenye powers kama Prof. Shaba, "The Pathologist" ilikuwa kwanza lazima "apate" ndipo akafanya "pathology!".

The biggest power practice inafanya na mafundisho ya Eastern Sciences ambayo yote kwa pombe ni marufuku!. Hindu na Budhism pombe kwao ni mwiko, hivyo yoga za aina zote zinapinga matumizi ya kilevi, sambamba na Uislamu. Hata baadhi ya dini za Kikristo wenye imani kali wakiwemo Wasabato na madhehebu yote ya Pentekoste pombe ni marufuku, tumebaki sisi Wakatoliki, Anglikana na Walutheri ambao pombe ni rukhsa ila kwa kiasi!.

Mimi kuna wakati niliweza kuacha pombe, baadaye nikaamua kuendeleza kunywa kwa raha zangu. Nikinywa na kulewa, naweza kufanya lolote ikiwemo "kuchepuka" kidogo kutoka kwenye "njia kuu", fahamu zangu zikinirudia, najusfy matendo yangu hayo kuwa "it was not me" ni "pombe" hivyo kujiplease kuwa sijafanya kosa lolote, na ninakuwa huru kabisa bila any guilt consciousness!.

Ushauri kwenu, if you can do without alcohol, una chances za kuishi vizuri zaidi kuliko kuendelea kunywa pombe!. Kwa vile the deviding line between nguvu za Mungu na nguvu za shetani ni very thin!, ukiwa kwenye influence ya pombe, you are more likeli kutenda ya shetani zaidi kuliko kutenda ya Mungu ndio maana maana wenye imani kali wanaamini pombe ni shetani!, hata ngono ni shetani!, kwa sisi wengine pombe kwetu ni starehe so do sex!.

Uamuzi ni wako!.

Pasco.
 
Pasco: What is a Psychic Attack?
Mkuu Schiendler, kwa mujibu wa michango yako humu, unaonyesha wazi uko deep, na hiyo psychic attack unaijua fika!.

Kama ulinisoma vizuri mule mwanzo, nimesema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na tumepewa "powers" za Uuungu zimo ndani yetu!. Tukizitumia hizi powers kufanya mema, tunakuwa tunampendeza Mungu. shetani naye pia yupo, na yeye ana powers, kazi yake ni kutughilibu sisi, ili hizi powers tulizopewa na Mungu, tuzitumie kutenda mao, tumtumikie yeye badala ya Mungu, hivyo matumizi ya hizi nguvu, kufanyia uovu wowote, ni kumtumikia shetani!. Nilisema wachawi, waganga, waongea na mizimu, wanga, na wengine wote wenye nguvu, huzitumia nguvu hizi kufanyia mambo!. Hvyo psychic attack ni matumizi ya nguvu hizi kufanyia shambulio la kichawi kwa mtu mwingine kwa lengo la kufanya maangamizi!.

Hata hivyo, maangamizi haya yanaweza kukupata tuu endapo wewe utakubali yakupate kwa kuamini, au ukiwa weak in spirit!, yaani ukiamini uchawi upo, na unaweza kulogeka, ukilogwa, uchawi unakupata!, kama ukiamini kuwa tes uchawi upo, ila huamini kuwa unaweza kulogeka, unakuwa tayari ume invoke hizi nguvu kukupa shield, hivyo unakuwa haulogeki hata waloge vipi!. Shield hii sio kwenye kuzuia kulogeka tuu, hata kuzuia maradhi, mfano ukijiaminisha huwezi tena kuugua malaria!, huugui tena malaria!. Mimi mwenzenu huu ni mwaka wa 20! malaria no!, na sio malaria tuu!,ukijiaminisha hata ukikanyaga umeme, huwezi kunaswa!,aminiusiamini, katika pita pita yako, unaweza kabisa kukanyaga miwaya yenye umeme live na usinaswe na umeme!, NB. Natoa onyo!, pamoja na uwezo wa kuzui kunaza na umeme kuwa nao, sishauri kabisa, wewe kujiachia na kupunyanga peku peku bila kinga yoyote katika mtandao wa hatari ambao nyanya za umeme zimetapakaa, eti kwa kisingizio tuu kuwa "I have the powers!, ziwezi kunaswa!, hii itakuwa ni abuse ya hizo powers, unaweza kuchapwa bakora kama adhabu, na moja ya bakora hizo inaweza kabisa kuwa ni kunaswa na umeme!.

Kwa uelewa zaidi karibu hapa

Psychic Attacks,
na hapa What is a Psychic Attack?
Pasco
 
Nimekukubali mkuu, ni kweli hizo issue karibu kila mtu anazo sema unakuwa unapuuzia tu, nahisi nahitaji kusoma vitabu zaidi ili kujua nguvu yangu niliyonayo,
mkuu kwa uzoefu wako naweza tafuta kitabu gani ambacho kitanisaidia kujua nguvu zangu.
 
Mkuu Schiendler, kwa mujibu wa michango yako humu, unaonyesha wazi uko deep, na hiyo psychic attack unaijua fika!.

Psychic Attacks,
na hapa What is a Psychic Attack?
Pasco
Manangwa Pasco:

Kabla sijaweka majibu au nyongeza ya posti/majibu yako, ngoja niongezee maswali haya kwanza.

Mtabiri wa nyota na kusoma viganja vya watu vya mikono na kuwaeleza hivyo wanavyosema ameona, huyu mtu ana tofauti gani na MPIGA RAMLI?

Je, unajimu unahusiana na majini au ni nguvu ya Mungu aliyo wapa viumbe vyake?
 
Manangwa Pasco:

Kabla sijaweka majibu au nyongeza ya posti/majibu yako, ngoja niongezee maswali haya kwanza.

Mtabiri wa nyota na kusoma viganja vya watu vya mikono na kuwaeleza hivyo wanavyosema ameona, huyu mtu ana tofauti gani na MPIGA RAMLI?

Je, unajimu unahusiana na majini au ni nguvu ya Mungu aliyo wapa viumbe vyake?
Utabiri wa nyota unaitwa astrology na kusoma viganya kunaitwa palmistry, hizi ndizo silaha mbili kuu zinazotumiwa na wanajimu na wapiga ramli!. Kwa mujibu wa imani ya Kikristu, kufanya hayo ni dhambi!. Kama nilivyoeleza tangu mwanzo wa uzi huu, matumizi ya hizi powers ni over and above Christianity. Bible imepiga marufuku mambo haya!. Mimi nimeishi kidogo India nimesoma kidogo maandiko ya dini ya Hindu na Budhiism, kiukweli ukizama humo ndani, unakuta Christianity ni almost nothing!, na Bible ni cha mtoto, ulifanya comparison, unajikuta ukistick na knowlege kutoka Bible pekee, then utajiona you know so much, ila in reality kwa kuitegemea bible pekee, kiukweli kabisa unakuwa you know so little!.

Kwenye uzi huu, kuna ile list ndefu ya vitabu vya elimu adimu, vingi sio vya dini, kuna mpaka vitabu vya elimu ya shetani, satanic, kuna mpaka vitabu vya kufundisha uchawi, kufundisha kupaa hewani etc.

Kwa opinion yangu, mimi nimeisoma astrology as a hobby na siifuati ila siipuuzi! kwa sababu unajibu ni pure mathematical!. Hata Yesu kabla hajazaliwa watabiri waliishatabiri kabla!. Alopozaliwa wale mamajuzi walimfuata hadi alipo kwa kuongozwa na nyota!. Sehemu kubwa isemayo "yanenavyo maandiko", ni kazi za unajimu!. Yusuph tangu akiwa mdogo alikuwa ni bwana wa ndoto!.

The dividing line between utabiri na unabii is very thin!. Mpaka kati ya kufunuliwa maono, na kuonyeshwa future kupitia psychic pia ni very thin!.

Wakati wote nawashauri wasomaji wangu, kujisikilizia "listening from your self", "the voices from within" ndio itakayokuambia what is real right and what is really wrong. Mfano mimi ni Mkristu, nimeoa Kanisani, nina mke mmoja, ila pia nina watoto kadhaa kwa wamama wengine kadhaa, mpaka kesho nikisafiri safari ya muda mrefu, huwa napata "usaidizi" huko niliko, nikihesabu I'm doing nothing wrong!, pombe nakunywa, sigara navuta hadi ile kubwa, starehe nafanya, Bibilia nasoma, kusali nasali na kanisani nakwenda!. Nimeicondition conscious yangu kukubali baadhi ya vitu ambavyo vinakatazwa na dini, mimi nimejiruhusu kuvifanya na kujiaminisha ita right kwa sababu mitume na manabii wengi ndani ya Bibilia walivifanya kama hiyo ya kuwa na mke zaidi ya mmoja na kujisaidia niwapo safari ya mbali kwa muda mrefu!. Vivyo hivyo japo ni Mkatoliki, kuna vitu tunavifanya, kupitia kuisoma sana Biblia na kuupata uelewa fulani kivyangu, kuna vitu sivifanyi!.

Dhamira ndio inayoniambia kweli kuwa hiki nitafanya, na hiki sifanyi!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom