Imani yao hawa Monks inapingana au inashabihiana vp na imani ya kikristo na/au uislam?
Mkuu Sabayi, hawa monks wamevuka stage ya imani!, they are powers!. Kama hukujua unajua baada ya kukufuka Yesu iliishi wapi?. Alitembeaje?!. Alikulaje?, hayo ndio maisha ya hawa monks!, Yesu alitembea juu ya maji!, hawa jamaa wanatembea juu ya maji!. Yesu alikuwa akiibuka na kupotea, hawa jamaa wanatokea na kupotea!. Yesu alikuwa akitembea kwa kupaa!, hawa jamaa wanatembea kwa kupaa!. Ukristo ni wa juzi tuu! na Uislamu ni wa jana tuu, dini ya hawa jamaa ilikuwepo kitambo sana!.
Kwa hizi dini za zamani Hinduism, Buddhiism na Taoism, kuzilinganisha na Ukristu, ni kama mlima na kichuguu!.
Wewe ambaye umezaliwa kwenye kichuguu, umekulia kwenye kichuguu, na unaishi humo humo ndani ya kichuguu, nyie humo ndani ndio mmeambiwa hicho kichuguu chenu, ndio mlima mkubwa kabisa kuliko yote!. Kwa sababu unachikijya ndio hicho hicho kichuguu, hivyo kinakuwa ndio mlima mkubwa wako!.
Ili kuweza kulinganisha, inakubidi wewe sikumoja utoke humo ndani ya kichuguu itembee tembee huko nje, utakaouna mlima mkubwa, uuliza hilo dubwana ni nini?, utaambiwa huo ndio mlima mkubwa!, utashangaa na kuuliza huo utakuwa ndio mlima wakati umeelezwa mlima mkubwa ni ule wewnu wewe ulimotoka!. Ndipo utakapoambiwa mlima mkubwa ni huo unauona!, mule wewe ulimotoka sio kwenye mlima mkubwa, bali umetoka kwenye kichuguu tuu!. Ukilinganisha huo mlima na kile kichuguu sasa ndio utajua ulima ni upi na kichuguu ni kipi!.
Hivi ndivyo ulivyo Ukristu na hizi dini!. Nimekaa kidogo India, nimezisoma kidogo, ndipo nikagundua kumbe Ukristu ni kichuguu tuu!. Pamoja na ukichuguu wa Ukristo, ninaendelea kushikamana nao, ila when it comes to powers, powers zote ziko ndani yetu!.
Pasco.