Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #1,361
Sorry Mate Sio Nakupinga Ila UKWELI Ni Kwamba Lucifer Hakuwa Malaika Alikuwa Ni Jini.. Malaika Wa Mungu Hawapingi Kile Anachosema Mungu Hawakupewa FREE WILLS wao asemacho mungu ndio hicho hicho kwa.. Lucifer Ana Material Ya Moto Ndio Maana Aliweza Kupinga Maana Alipewa FREE WILLS....
Source Ya Mungu Ni Nyingine na anaijua yeye tu Mkuu..
Lucifer Hakujiumba Aliumbwa na mungu kwa hiyo usiseme mwanzo wa mungu ndio wa lucifer....
kwamba wanazidiana nguvu hiyo haipo mungu ni alpha na omega kama ulivyonena sasa kama ni alpha na omega means vingine vyote vipo chini yake tena havimkaribii hata robo.....
"Rakims"
Mkuu Rakims,tunazo ulimwengu mbili, ulimwengu wa mwili, physical world, na ulimwengu wa roho, spiritual word. Kwenye ulimwengu wa mwili, ndiko hapa tulipo, tunapoonana physically na kugusana etc, mwili ukishakufa ndipo unahamia katika ulimwengu wa roho.
Kama ulivyo ulimwengu, miili yetu nayo inazo sehemu mbili kuu, the physical body, ambao ndio mwili huu wa nyama, na the spiritual body ambao ni mwili wa roho, astral body.
God, devil, malaika, majini, wanga, mashetani, ni spirits hivyo they act on spiritual bodies. Lucifer ndie alikuwa malaika mkuu, anaitwa malaika pale tuu anapotenda mema, lakini anapotenda maovu ndio huitwa shetani, majini pia ni hao hao malaika na ndio hao hao mashetani, jini la ulinzi au la mafanikio ndio malaika wema na jini la maangamizi ndio mashetani, the dividing line between malaika na jini ni very thin so does the dividing line between Mungu na shetani, na nguvu za Mwanga na nguvu za giza.
Nguvu za mwanga ni wale wote wanaotumia nguvu za Mungu kutenda mema, sala, maombezi, uponyaji, mafanikio, etc, ila pia shetani nae ana nguvu na ana penda sana kuji disguise kama ndie Mungu, hivyo wapo wanaotumia nguvu za giza kufanya maombezi, uponyaji au kupata mafanikio huku wakilitaja jina la Mungu jut to make believe kuwa ni Mungu, lakini kiukweli ni shetani!.
Utawatambuaje hawa kama ni miujiza ya nguvu za Mungu au ni miujiza ya nguvu za giza au za shetani, utawatambua kwa namna mbili tuu.
1. Matendo yao: Ukiwafuatilia utawakuta wanahubiri Neno la Mungu madhabahuni, tuu, lakini nje ya madhabahu, wanatafuta utajiri, ni wazinzi na waasherati wakiendekeza ngono, utawaona wakivaa mawazi nadhifu ya kuonekanika, wakitembelea magazi ya kifahari, wakimiliki utajiri mkubwa majumba, madhahabu, fedha na vitu vingine vya kuonekanika, huku wakilipia airtime mahubiri yao yaonekane kwenye ma TV huku kistari ya mbele wakiwapanga matajiri etc!. Wahubiri wanaotumia nguvu za giza wako arrogant na huhubiri kwa ku shout!, Wahubiri wa kweli wanaotumia nguvu za mwanga wako humble and down to earth!, huomba kwa kuzungumza na Mungu, very sofltly and humbly!.
2. Mafanikio, miujiza, uponyaji toka kwa Mungu ni unconditional! tunaokolewa kwa neema tuu na sio matendo, ukipona utaambia imani yako ndio imekuponya na credits zote za uponyaji zsiende kwa Mungu, lakini uponyaji, au mafanikio ya nguvu za giza ni conditioner!, utaambiwa ili upone lazima ufanye abcd!, lazima usali kanisa fulani, mhubiri yule hujifanya yeye ndio mwenye hizo nguvu za uponyaji hivyo wewe umtegemee yeye, na sometimes huandamana na material things, maji ya baraka, mara leta nguo,mara jishike hapa ili mradi lazima utawekewa conditions na the bottom line ni sadaka!, makusanyo!.
Mungu alipotuumba ulitupa Umungu hivyo yupo ndani yetu spiritually na kila muujiza wa kweli wa Mungu, comes from within!. Shetani nae ni spiriti ila yuko without, anajitahidi sana akuingie ili Roho wa Mungu akutoke!, Mungu na shetani hawakai pamoja, hivyo ukimpokea shetani, umempoteza Mungu!, kuna wengi wetu wanamtumikia shetani bila kujijua wakiamini kuwa wanamtumikia Mungu!.
Pasco.