Ndugu Pasco, Kutojua muujiza behind yule bibi haina maana kuwa hizo hearsay zinazosemwa juu yake ni za ukweli. Hapo kuna siri. Mbona wewe hukuenda huyo bibi akakutengenezea na wewe mambo yako yakawa sawa? Mhhhh, story kama hizo ziko nyingi sana sana lakini zote ukiuliza maswali mawili matatu tu, zinaisha mwisho. Ndugu yangu, hapo kwenye simulizi yako kuhusu huyo bibi hakuna chochote cha kuthibitisha miujiza, telephathy, au nguvu ya psychic powers au paranomal. Je wataka tuamini kuwa bibi huyo anatumia nguvu hizo kuwasaidia hao wanasiasa au huyo tajiri wa uarabuni unayesema alimjengea ghorofa? Mhhh, hapo ndo unapoona kuwa hii si kweli; kwanza bibi mwenye hizo nguvu hadi aletewe hela na hao wanaonufaika nazo, pili hao wanaonufaika na hizo nguvu hawajipambanui kunufaika nazo. Lakini vile vile wewe mwenyewe hukujiridhisha ni kwa jinsi gani huyo bibi anatumia hizo nguvu, sana sana na wewe umeangukia kwenye kusikia hearsay halafu unasimulia wengine, na wengine wanasimulia wengine, n.k. Hivyo ndivyo uchawi, ushirikina, n.k. unavyofanya kazi. Ukichimba undani wake hutaona jipya, sana sana utakutana na mitandao ya uhalifu.
Usemayo yanaweza kuwa na ukweli ndani yake!.
Mimi sikwenda kwa sababu I don't believe mambo hayo!.
Nikiwa kijana mdogo nikifanya kazi RTD miaka ile ya 90s, nimemaliza form 6, nina diploma ya Journalism, niliposema nataka utangazaji, walishangaa!, by that time watangazaji wengi walikuwa form four, kama hawakuzungusha, then, wameponea chupu chupu!. Nikatishiwa kulogwa!. Sikutishika!.
Baada ya mwaka mmoja kazini, nikiwa ndani ya basi la dala dala natoka Kariakoo kuelekea Mwenge, huku nimeshika bomba baada ya kukosa siti, tulipokuwa tunakaribia eneo la Magomeni Mapipa, babu mmoja emevaa kibalaghashia na ndevu kama za Osama, akasimama akijiandaa kushuka aliponifikia nimpishe, akanisalimia kwa majina yangu yote mawili!, akaniambia nina kufahamu, wewe si ni fulani ndio maana nimekuita kwa jina lako, tena una matatizo makubwa kazini!, nikazidi kushangaa, ila kiukweli kazini sikuwa na matatizo yoyote!, akaniuliza kwani unakwenda wapi?!, nikamjibu nyumbani, akanishauri nishukie hapo kituo cha mapipa, anieleze matatizo yangu ya kazini na jinsi atakavyo nisaidia!. Du kusema ukweli, kama nimelogwa, nikajikuta huyo nashuka nae Mapipa!.
Pale kituoni tukasimama pembeni, babu akafunguka, yeye anauwezo wa kuona matatizo ya watu na nimewasidia wengi tuu, tatizo langu kazini ni eti sauti yangu haina ladha!, eti nikitangaza watu wanazima redio!, enzi hizo redio moja tuu RTD!, hivyo malalamiko hayo yameishafikishwa kwa Mkurugenzi, David Wakati, ninachosubiri ni taratibu tuu za kufukuzwa kazi!. Kiukweli nilistuka!. Ila kimoyo moyo najiuliza mbona sikuwahi kusikia malalamiko yoyote ya hivyo!. Akaniambia nitakusaidia ila kwanza tufike nyumbani kwake! ni karibu tuu hapo mtaa wa pili wa Idirisa na Mikumi!. Nikamwambia tutapanga nije siku nyingine!, akasisitiza twende ukapaone ili ukija usipate taabu kupatafuta!, nikasita kidogo, nikajikuta nimekubali, mimi huyoo, babu mbele mimi nyuma!.
Kufika kwake sebuleni, kuna sebule kubwa haina kiti hata kimoja, kuna zulia jekundu tuu kuu kuu na kabati moja la kioo!. Karibu.. hukae chini, au hujazoea tukakuletee kit!?, kiukweli kukaa chini ni issue kidogo, akanipa mto nikajiegemeza ukutani!, akaniagizia chai, au kahawa nikamjibu asante, basi maji, nikasema asante!. Mazungumzo yakaanza!.
Yeye ni mtaalamu wa nyota, ameona nyota yangu inangaa sana, hivyo kwa elimu yangu, nitafika mbali na RTD, hivyo watangazaji wenzako wanakuonea kijicho, hivyo wamekuendea kinyume!, wameitia kiza nyota yako!. Akauliza wewe una gari ya kutembelea?, nikamjibu hapana, una nyumba yako, nikamjibu hapana bado naishi home!, unaona?!, wameamua kukukwamisha kabisa!, saa hizi ulipaswa uwe una gari na nyumba nzuri!. Nikawaza kidogo, mishahara ya serikali enzi hizo, nimefanya kazi mwaka mmoja niwe na gari na nyumba!, enzi hizo, mtangazaji mwenye gari, ni wale tuu waliotoka kwenye exchange program za redio za nje, BBC, Ujerumani, VOA, Japan etc. Nikajifanya kukubaliana nae.
Akaniambia kazi ya kwanza ni kusafisha nyota yangu ingare!, sauti yangu iwe tamu kama asali kuisikiliza!, du!, nikasita kidogo kumkubalia!, nikamuuliza umawahi kuwasaidia kina nani?!, he came out with a long list of names za watangazaji!, aliwataja karibu wote waliokwenda ulaya!. Almanusura nikubali!, wakati akiendelea kuongea, kikachomosa kipanya kidogo nyuma ya kabati, kinakuja usawa wake!, amini usiamini, mimi siogopi nyoka!, ila panya!. Nikataka kuamka akasema usiope, hawa ni panya wangu tuu hawana madhara, hata wakija kukupandia, usiwaogope!, akanyoosha mkono kama kukiita kile kipanya kije, kikaja kaja kisha kikakimbia!.
Ule uoga wa panya, ukanifanya nijisikie sitaki tena hata kusaidiwa nikaaga kuondoka na kuahidi nitakuja siku nyingine!, jamaa anashangaa vipi, mimi naamka!, akaamka kunitoa huku akiendelea kutaja majina ya wakubwa aliowasaidia kunyoosha mambo yao!, nikiiangalia hali yake na hapo kwake!, mimi nyota iliyotiwa kiza ni afadhali!.
Sikurudi tena, na kazini hakukuwa na tatizo lolote!, ila ile listi alionitajia amewasafishia nyota zao, kiukweli walikuwa wanapisha ulaya!, mtu anatoka BBC anatulia kidogo anapelekwa Ujerumani, akirudi hajakaa sawa huyo Japan!, sisi wengine ni Tandahimba na Kimanzichana na Chole Samvula!, ila nilikubali kuna watu na bahati zao!.
Mafundi wa kusafisha yota mambo yako yakunyookee wapo!, ila nguvu za kweli za kunyoosha mambo yako, ziko ndani yako mwenyewe, ukiamini yatanyooka, yananyooka yenyewe na sio lazima kwenda kwa wasafisha nyota kuyanyoosha!. Mafundi safisha nyota, wanatumia nguvu za giza kusafishia, hivyo hata mambo yakikunyookea, ni kwa muda tuu!, lakini yakikunyookea kwa nguvu za Mungu zilizo ndani yako, ni yamenyooka jumla!.
Pasco