Wanabodi,
Conclusion
Trends za Samia, zinaonyesha tunaelekea kwenye Tanzania njema yenye rais humble, mpole, mnyenyekevu, mstahimilivu
Paskali
Wanabodi,
Hii humbleness ya huyu Mama, na being down to earth, nimeiona tena jana, kwenye kuhitimisha Nane Nane Mbeya.
Baada ya kukamilisha kuhutubia, wakati anaondoka, badala ya kuelekea direct kwenye gari, akatuzungukia wananchi huku tukipo, mimi nikamwamkia kwa sauti, akageuka, akanitazama, akaijibu shikamoo yangu, tena I think...naomba nisimalizie maana...
Na wakati anahitimisha hotuba yake kuhitimisha Maonyesho ya Nane Nane Viwanja vya John Mwakangale, Mbeya kuna kitu sio cha kawaida, Rais Samia amekifanya, hakijawahi kufanywa na rais wetu mwingine yoyote, ukimuondoa Nyerere.
Siku zote kwenye matukio rasmi, viongozi wanatayarishiwa hotuba kwa kuandikiwa na Viongozi huhutubia ama kwa kusoma hotuba alioandikiwa, ama kwa kutumia talking points.
Lakini licha ya rais kuandikiwa hotuba, kuna baadhi ya vitu huwa anavisema kwenye hotuba ni vyake mwenyewe kutoka moyoni na sio kuandikiwa,
Wengi wa wenye uwezo wa to read in between the lines, pia wana uwezo to listen in between the world's hivyo Mama anapohutubia, ma psychoanalysits wenye uwezo wa kubaini hili ni ameandikiwa na hili ni lake kutoka moyoni.
Kwenye hotuba ya jana kule mwisho, aliwashukuru madereva.
Ukimuondoa Nyerere na hotuba zake za kulihutubia taifa kwa njia ya redio, hii ndio mara yangu ya kwanza kumsikia rais wetu yoyote akiwashukuru publically madereva!.
Wasio na jicho la roho, jicho la ndani, wanaweza kuona this is a small thing!. It's not!.
Hii shukrani kwa madereva kila mtu huwa anaitoa kwa dereva wake akifika salama, lakini ile shukrani kuwashukuru madereva publically for the first time, japo inaonekana ni shukrani tuu, kwa sisi ma psychoanalysits, sio shukrani tuu, ile ni shukrani ya appreciation ya being arrived safely out of ...
Kwenye shukrani hizi, kuna kitu hapa Rais Samia amekisema bila kukitamka, uwezo wa kumwelewa rais wetu bila hata kutamka kitu ni plus kwenye utawala wa nchi.
Katika shukrani hizi za rais, Rais Samia kawasifu na kuwapongeza madereva wa msafara kwa umahiri wao na car control.
Sijui ni wangapi kati yetu wana uwezo wa kusoma facial expressions wakati mtu akiongea!, Rais Samia amewashukuru madereva kwa kuwafikisha salama na kushukuru Mungu kufika salama.
Kitu ambacho Mama Samia hakukisema ni the speed of msafara was very high, mnamuweka Mama Roho Juu!.
Kwa vile tumetawaliwa na wazungu, watu wetu wa usalama wanafunzwa msafara kwenda kwa kasi ya ajabu hivyo hivyo na wao kuiapply hivyo hivyo hata kama in reality Tanzania haina security threat kwa rais wetu kivile!.
Kwenye msafara wa rais kuna rake 3, kabla ya msafara, hivyo madereva wanakimbiza msafara kwa speed ya ajabu for what?!.
Halafu unaambiwa eti wanakijiji au wananchi wa eneo fulani wamezuia msafara!.
All and all, asante sana Mama kuonyesha concern for this.
Hata hii democrasia tunayoitumia ni imposed democracy, kama sasa tunaotumia the African Democracy ambapo nchi ya vyama vingi vya siasa, vinaweza kufanya uchaguzi Mkuu na chama kimoja kikashinda Kwa 99% na uchaguzi huo ukawa huru wa haki na wa kidemocrasia, tuachane na imposed security protocols, to embrace African security protocols, viongozi wetu wakimaliza wanasalimia na kujichanganya kidogo na watu.
P