Wanabodi,
Moja ya topic ngumu sana humu JF, ni topic za kitu kinachoitwa Trends Readings za psychoanalysis trends, kinacho tokana na ku psychanalyse Trends kisaikolojia kwa kutumia tabia za mtu za nyuma, tabia za sasa kuweza ku détermine tabia kitakachokuja kutokea baadae in near future kwa short term, médium term na long term.
Trends Reading ni Nini, na Zina Kazi Gani, na Zina Faida Gani?.
Kwa kifupi, trends ni mielekeo, hivyo trends readings ni kusoma mielekeo, faida ya kusoma mielekeo, au direction, na kuangalia kule mliko toka, hapo mlipo mlipo, ili kujua kule mnakokwenda. Ni kama somo la Historia, ni kujifunza mambo ya zamani, kule tulikotoka, kulinganisha ya sasa hapa tulipo, hivyo kuweza kujua kule tuendako. History is the study of the past in relation to the present, to determine the future. Hivyo faida kubwa kabisa ya trends reading is the determination of the future. The future haijiji tuu kama kudra ya Mwenyezi Mungu, inakuwa determined na matendo yako ya nyuma, matendo yako ya sasa, hivyo kuipanga kesho yako iweje.
Trends Reading Sio Utabiri, Sio Ubashishiri, Ni Usomaji wa Mienendo na Mielekeo, Matokeo ya Trends ni Uhakika Zaidi Kuliko Utabiri na Ubashiri.
Kuna watu wanachanganya ubashiri, utabiri na trends readings. Japo yote matatu, yanaweza kusema kitatokea nini in future, mtabiri yeye anatumia mizimu kuuliza na kuona kitatokea nini, hawa wanaitwa scorchers, kuna wasoma nyota wanaoweza kukuambia yajayo kwa kusoma nyota yako, hawa wanaitwa astrongers, kama Sheikh Yahaya Hussen. Kuna wabashiri, hawa ni watu wa kubahatisha tuu kama bahati nasibu, Simba na Yanga zikicheza, kuna matokeo matatu tuu, au kushinda, kushindwa na sare. Wabashiri wanabahatisha lolote likitokea, wanakula bingo kwenye betting. Trends Readers, sio wanajimu, sio wabashiri ni watu wa kawaida tuu ambao ni wasoma mielekeo, trends na kuweza kusema kitatokea nini in future kutokan na matendo au matukio ya nyuma, matukio ya sasa na hivyo kujua matukio yajayo.
Trends Readers Humu JF ni Kina Nani na Jee Hizo Trends Zao, Zilikuja Kutokea?
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kwa wapenda mastori, sasa kwa faida ya wenzetu wasio penda long stories, mnaweza kuishia hapa, na kwenda kusoma conclusion
Tuanze na Psychoanalysis ni nini na ya kazi gani au inasaidia nini?.
Conclusion
Trends za Samia, zinaonyesha tunaelekea kwenye Tanzania njema yenye rais humber, mpole, nyenyekevu, mstahimilivu, na hata kule UN, tumemshuhudia katika hotuba yake, amehutubia UN akiwa humble vile vile. Once humble, always humble.
Mungu ambariki sana, Mama Samia aendelee na hii humbleness yake asibadilike.
Mtu mcha Mungu, mpole, mnyenyekevu wa type ya Mama Samia, akitibuliwa na akatibuka... JPM atakuwa ni mtakatifu!.
Kama alivyo sema mwenyewe kuhusu uwezo wa macho yake yale, yanaona hayo!, na akasema wazi yeye sio mtu wa kufoka foka na akatoa onyo tusimzengue "mkinizengua, tuta zenguana"
Natoa wito kwa sisi wana Jf, la Watanzania kwa ujumla lets give her time, tumpe muda wa kutosha kuisuka nchi. Lets not take upole wake, unyenyekevu wake na humbleness yake for granted tukaanza kumzengua...
She will be....
Naomba nisimalizie
Nakutakia Jumapili Njema.
Paskali