PUBLIC RELATIONS: Rais Samia anaweza kutumia busara tu. Ijumaa (December 27, 2024) iwe siku ya mapumziko.

Sijaweka Udini Nina maanisha kupumzika sawa si kwa kiasi hicho unachosema Wewe, Mfano una machine ya kusaga na wafanyakazi10 wanakula Milo mitatu ya nguvu!Wapumzike siku 2Kwako ni Faida??Acha mawazo ya kivivu.Chukua likizo .
Kupumzika Ijumaa ni siku 2?? Serikali ina mashine ya kusaga?? Kupumzika analazimishwa mtu?? Kwani hiyo December 26, madaktari na Police hawaendi kazini??
 
Kwa wafanyakazi wengine hasa wa serikali siku huyo ya ijumaatrh 27 itakuwa na maudhurio hafifu
Wengine hawatokwenda kazini kwa kigezo Cha ugonjwa au dharura za kifamilia
 
Watumishi wa umma ni asilimia ndogo sana kati ya mamilioni ya Watanzania.
Na hizo amri za kupumzika haziwahusu sekta binafsi, hivyo anayejisikia kupumzika ijumaa anaweza kujipumzikia bila busara ya Mkuu wa nchi.
Lakini pia tunaona siku za mapumziko zinapokuwa mfululizo baadhi ya taasisi kama mabenki huamua kufanya kazi ili kutoa huduma kwa wananchi, hata kama kuna ruhusa kwa busara za Mkuu.
Kwa hiyo ni wewe tu ukiamua kula bata wiki nzima, byee!
 
Ijumaa itakuwa siku ya kazi kinadharia ila kiuhalisia hakuna cha maana kitakachofanyika. Utaenda ofisi za serikali utakuta huduma unayotaka utapata nusu, na nusu nyingine utaambiwa njoo jumatatu, kwa sababu mmojawapo wa wahusika ambao wangehudumia jambo lako hayupo amesafiri. File lako liko kwa boss lakini amesafiri
 
Absolutely 💯 right. That's my great concern.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…