Mliojiunga JF miaka ya 2020 hamwezi kumfahamu huyu bwana. Naona alipunguza sana uchangiaji hapa jukwaani. Aliwahi kuleta simulizi moja nzuri sana ya vituko vya JKT ya miaka ile (siyo hii ya miezi 3).Yeah mwenyewe ni mgeni machoni na masikioni ila inatukumbusha kutojisahau sana...tunakufa bro..daah
Wakuu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.
Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.
Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.
Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Inaumiza sana mkuuLooh, pole sana kwa familia! Naikumbuka sana michango yake hapa jukwaani!
Mliojiunga JF miaka ya 2020 hamwezi kumfahamu huyu bwana. Naona alipunguza sana uchangiaji hapa jukwaani. Aliwahi kuleta simulizi moja nzuri sana ya vituko vya JKT ya miaka ile (siyo hii ya miezi 3).
Ni kweli, apumzike kwa amani mkwe wetu. Tuko hapa nyumbani kwenye kikao cha familia.Pole sana Max na wana JF.
Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".
Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.
Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.
Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.
Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
Mazishi yatakiwa siku ya jumapili. Ataagwa kanisa la sabato hapa Segerea saa saba, atazikiwa makaburi ya Kinondoni saa tisa jioni.Inabidi tubaki hapa kupata ratiba kamili ya mazishi, tukipata muda tuhudhurie
Poleni sanaNi kweli, apumzike kwa amani mkwe wetu. Tuko hapa nyumbani kwenye kikao cha familia.
R.I.P Mwamba mwenzetu JFs.Wakuu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.
Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.
Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.
Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Ahsante sana kwa taarifa hiiMazishi yatakiwa siku ya jumapili. Ataagwa kanisa la sabato hapa Segerea saa saba, atazikiwa makaburi ya Kinondoni saa tisa jioni.
Shocking news ! RIP Mtsimbe.Wakuu,