Ndugu binaadam wenzangu, kumbe kuacha Kupiga punyeto ni jambo linalowezakana lakin sio kirahisi sana. mimi nimefanikiwa kuacha kabisa punyeto.
Mimi nilidumu katika punyeto kwa miaka 7.
Nilianza kupiga punyeto tangu mwaka 2006 nikiwa na miaka 15 mpaka mwaka jana 2013 nikiwa na miaka 22. Lakini nakumbuka ilikuwa mwezi July mwaka jana nilikaa mwenyewe na nikajiapiza kutofanya tena punyeto.
Nashukuru sasa ni zaidi ya mwaka mmoja sijafanya punyeto, na nina mpenzi wangu tunafurahia vyema mahusiano yetu.
Jamani ukiwa serious na kama una nia ya dhati ya kuacha punyeto, basi ni jambo linalowezekana.