Badala ya kuamua kupiga punyeto ili kuzima tamaa za ngono, jitahidi kukuza sifa ya kujizuia. (
1 Wathesalonike 4:4, 5) Ili ufaulu, kwanza kabisa Biblia inapendekeza ujiepushe na hali zinazoweza kuamsha tamaa ya ngono. (
Methali 5:8, 9) Namna gani ikiwa umekuwa mtumwa wa zoea la kupiga punyeto? Labda umejaribu kuacha lakini hujafanikiwa. Ni rahisi kukata kauli kwamba huwezi kubadilika, na kwamba huwezi kuishi kulingana na viwango vya Mungu.
Kwa hiyo, jaribu kuwa na usawaziko. Kupiga punyeto ni uchafu. Mazoea hayo yanaweza kukufanya uwe ‘mtumwa wa tamaa na raha za namna mbalimbali' na kukufanya uwe na maoni yasiyofaa. (
Tito 3:3) Hata hivyo, kupiga punyeto si upotovu wa kingono, kama vile uasherati. (
Yuda 7) Ikiwa una tatizo la kupiga punyeto, usikate kauli kwamba umefanya dhambi isiyoweza kusamehewa. Siri ni kupinga tamaa ya kufanya hivyo na
kutokubali kamwe kushindwa!
Chunguza burudani yako. Je, wewe hutazama sinema au programu za televisheni au hutembelea vituo vya Intaneti vyenye kusisimua kingono? Kwa hekima, mtunga-zaburi alisali kwa Mungu: "Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa."
*-
Zaburi 119:37.