Rais mbabe na mmiliki wa mkanda mweusi wa judo katangaza kuanza kuuza gas yake kwa zile nchi alizoziita unfriendly kwa sarafu ya rubble badala ya dollar & euro na katoa wiki moja kwa bank kuu ya Urus kukamilisha utaratibu wa kupokea mauzo ya gas kupitia rubble
Kwahiyo kuanzia wiki moja toka Leo nchi za ulaya zitaanza kukimbizana huku na kule kusaka rubble
=====
Putin Wants ‘Hostile’ States to Pay for Russia Gas in Rubles
Sign up here to get the latest updates on the Russian invasion of Ukraine. You can also follow us on Telegram here.
Russia will demand that “unfriendly” countries pay for natural gas in rubles, President Vladimir Putin said Wednesday, causing European futures to jump.
“I have taken a decision to switch to ruble payments for our natural gas supplies to the so-called hostile states,” Putin said at a meeting with government officials, according to a transcript published on the Kremlin website. “Stop using the compromised currencies in such transactions.”
Benchmark European gas prices rose as much as 21% in Amsterdam amid concerns that Russia’s requirement could exacerbate the energy supply crunch on the continent. The ruble
strengthened.
State gas exporter
Gazprom PJSC’s press office declined to comment on whether its long-term supply agreements allow a switch to ruble payments.
Within a Week
Putin ordered Russia’s central bank to develop a mechanism enabling such payments within a week, according to the transcript. Earlier in March, Russia’s government announced a list of
48 states deemed hostile. They included the U.S., Japan, all European Union members, Switzerland and Norway. As a result, the bulk of Russian gas exports now go to “unfriendly” nations.
Some 58% of Gazprom’s gross gas sales abroad were in euros as of the third quarter of last year, according to the producer’s most recent bond prospectus. Another 39% were in U.S. dollars.
“At the same time, I want to emphasize that Russia will definitely continue to supply natural gas in line with the volumes and prices and pricing mechanisms set forth in the existing contracts,” Putin said.
In the first 15 days of March, Gazprom
exported an average of 500 million cubic meters per day to countries outside the former Soviet Union, including those in the EU, China and Turkey. Of the total, flows toward Europe averaged 384 million cubic meters per day, the producer’s data showed.
Putin also said it makes no sense to export goods to the U.S. or EU in dollars or euros
Na Lilian Mtono | saa (0) nyuma
[
https://res]
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesisitiza kupinga vikali hatua ya kususia bidhaa za nishati kutoka Urusi na kusema hatua zaidi zitaibua hatari ya matokeo mabaya katika uchumi wa Ulaya.
Kansela Olaf Scholz amesema vikwazo ambavyo tayari vimewekwa dhidi ya taifa hilo vina athari kubwa. Scholz amesisitiza hayo katika wakati ambapo kuna mashaka kwamba hatua zaidi zitaibua hatari ya matokeo mabaya katika uchumi wa Ulaya.
Kansela Scholz amesema hayo wakati kukiwa na miito kwa mataifa ya magharibi kususia kabisa bidhaa zote za nishati kutoka Urusi baada ya kuivamia Ukraine. Scholz amesema ni lazima wawe wazi katika hilo kwa kuwa linaweza kuibua mzozo wa muda mrefu, na mataifa hayo yote yanapaswa kuungana.
Msimamo wa Ujerumani katika hili haubadiliki. Kwa bahati mbaya hili lina ukweli kwa wanachama wengine wengi tu wanaotegemea zaidi makaa, gesi na mafuta, kuliko hata Ujerumani. Na katika hili, hakuna yoyote atakayeachwa nje, alisema Scholz.
Marekani na washirika wake wa magharibi wanaangazia iwapo Urusi inaweza kusalia katika kundi la mataifa yenye nguvu kiuchumi la G20, baada ya uvamizi huo hii ikiwa ni kulingana na chanzo kilichohusika kwenye majadiliano kuhusu hatua hiyo, kilichozungumza na shirika la habari la Reuters siku ya jana.
[
https://res]
Mkutano wa G20 unatarajiwa kufanyika nchini Indonesia, lakini kukiwa na wasiwasi wa baadhi ya wanachama kutoshiriki
Chanzo hicho kimesema kufuatia uwezekano kwamba jaribio la kuitenga Urusi mara moja huenda likapigiwa kura ya turufu na wajumbe wengine wa kundi hilo ambao ni pamoja na China, India, Saudi Arabia na wengine, kuna mashaka kwa upande mwingine kwamba baadhi ya mataifa pia hayatahudhuria baadhi ya mikutano ya G20 kwa mwaka huu.
Kundi hilo la G20 pamoja na kundi dogo la mataifa saba ambayo ni Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Canada, Japan na Uingereza ndio hasa waratibu wa kimataifa katika kila jambo kuanzia hatua kuelekea mabadiliko ya tabianchi hadi deni la kimataifa.
Wakati mataifa hayo ya magharibi yakifikiria kuiengua Urusi kutoka G20, balozi wa Urusi nchini Indonesia amesema mapema leo kwamba, rais Vladimir Putin anapanga kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi hilo utakaofanyika Indonesia baadae mwaka huu.
[
https://res]
rais Joe Biden wa Marekani atazuru Ulaya kwa nia ya kuimarisha mahusiano na washirika wake wa magharibi
Rais Joe Biden, kuzuru Ulaya kuimarisha uhusiano.
Rais Joe Biden wa Marekani kwa upande wake anaondoka hii leo kuelekea Ulaya akiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano na washirika wake wa magharibi, kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi lakini pia likiwa ni jaribio la kuhujumu mzani wa nguvu za kijeshi wa baada ya enzi za vita baridi.
Kesho Alhamisi, Biden atahudhuria mikutano ya kilele ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO na ule wa mataifa yaliyostawi zaidi kiuchumi ulimwenguni, G7. Biden pia atahudhuria mkutano wa Baraza la Ulaya. Siku ya Ijumaa, atakwenda Poland inayopakana na Ukraine, siku ya Jumamosi akitarajiwa kukutana na rais Andrej Duda.
Huku hayo yakitarajiwa, Umoja wa Mataifa hii leo linajadili maazimio matatu kuhusiana na kuzorota kwa hali ya kibinaadamu nchini Ukraine baada ya Urusi kuamua kuitisha kura kuhusu azimio lake kwenya baraza la usalama, ambalo halitaji mashambulizi yake dhidi ya jirani yake Ukraine. Baraza kuu la Umoja huo limeanza kuangazia maazimio ya wapinzani hao wawili mapema leo, moja linaloungwa mkono na Ukraine na mataifa ya magharibi kwamba Urusi inahusika na kusambaa kwa mzozo wa kibinaadamu na lingine lililodhaminiwa na Afrika Kusini, ambalo haliitaji Urusi.