Marekani hakukimbia Vietnam kisa silaha, kilichomtoa huko ni hili kosa analolifanya Putin la kutaka kupigana na taifa lote wakiwemo wananchi. Marekani alijikuta anapigana na akina mabibi, mababu, watoto, n.k.
Yaani mnapita kijiji wakulima wanaojilimia hawana issue, ghafla mnashangaa hao wakulima wanageuka kuwa wapiganaji wanawafyatulia risasi za ghafla.
Wananchi wakishaaminishwa propaganda za kutosha na kupata mzuka, mbona utaomba poo maana hizo silaha zako watakua wanazikojolea, utaua wangapi, mamilioni ya watu kwenye nchi yao, vitongoji vyao, milima yao, mashamba yao, mito yao....