Putin na Kim Jong Un wakibishana nani kuwa wa kwanza kuingia kwenye gari

😁😁😁 Madikteta huwa wana maisha ya tabu sana
Kwahiyo wanaouwa watoto gaza, watu wasio na hatia na kuvuruga nchi za watu mfano libya, Syria, yemen, msumbiji, congo n.k sio madikteta! Obama na washirika wake wametuulia kiongozi wetu gadafi, je! Hao sio madikteta!
 
Ndio maana mnauliwa huko marekani na israel kazi kushobokea tu
 
Hiyo Yako ni ya Leo hiyo ya mleta mada ni ya Jana usiku alipokuwa akishuka airport wewe ndie umechanganya na kuweka ujuaji
Ujuaji gani nimeweka zaidi ya kupost picha inayowaonesha Putin na Kim wakiwa kwenye gari moja!?
kwahiyo unahisi mimi ni kipofu kiasi kwamba nishindwe kutofautisha picha iliyopigwa usiku na iliyopigwa mchana. Wabongo punguzeni ujuaji, maisha yenu hayafanani na ujuaji mnaojibebesha.
 
Umeshindwa kutofautidha ya usiku hawakupanda ya wazi na njia nzima hakukuwa na watu wa kuwapokea Wala wa kuapungia mikono.ilikuwa Giza Totoro njia nzima Hadi wanafika makazi ya ikulu
Wenzio tuliona usiku akiwasili.wewe baadabya kuchaji ndio ukakumbuka shuka wakati kumekucha unaleta picha kukiwa kumekucha



Hiyo Yako ya Leo
 
Poa Shoto, nimekubali Putin na Kim walikuwa wanabishana kuhusu nani aanze kupanda gari kwasababu wote ni madikteta, hakuna anayemuamini mwenzake!
 
Si kweli
 
Kwahiyo wanaouwa watoto gaza, watu wasio na hatia na kuvuruga nchi za watu mfano libya, Syria, yemen, msumbiji, congo n.k sio madikteta! Obama na washirika wake wametuulia kiongozi wetu gadafi, je! Hao sio madikteta!
Bila shaka itakuwa umekosea kunukuu mkuu. Kama sivyo basi una mihemko sana, uipunguze. Maana ulichokinukuu hakiendani kabisa na hayo unayojaribu kunilisha.

Sijawataja madikteta kwa majina na hakuna niliyemtaja kuwa si dikteta. Sijasema kuwa Putin na Kim wakiwa madikteta basi Obama na Macron hawawezi kuwa madikteta. Sijazungumzia kabisa habari za Gaza, Libya wala Yemen. Pia Sijazungumzia kabisa habari za akina Obama na akina Gaddafi.

Shida mkipenda ligi huwa mnadhani kila mmoja yupo kwenye hizo ligi zenu, na ana upande anaoushabikia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…