PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

Sijui kama umesoma vizuri uzi hapo juu mkuu.

Jeshi la hitler liliwachinja waisrael kama vile mbuzi wanavyochinjwa kila siku pale Vingunguti machinjioni.

Jeshi la hitler lilivamia ufaransa, poland na nchi karibia zote wakateka miji na kufanya maangamizi makubwa.

Lakini jeshi hilo hilo la hitler lilishindwa vita na kuangamizwa vibaya na warusi hadi kupelekea kurudi nyuma na kupoteana.

So unapokuja kuandika kitu uwe na uhakika wa kujua unacho comment sio uandike tu kwa vile umelishwa propaganda za Israel na wenzako.

Israel bila Marekani, Ulaya na Nato ni sawa sawa na simba kibogoyo ambae hawezi kukamata windo na kulila.
io israel iliopigwa na hitler ilikuwa haina makao maalumu wala haikuwa na jeshi walikuwa wakimbizi nchi za ulaya na kwengine hata ivyo pamoja naukimbizi wao walikuwa ma milionea kuwazidi hata wazawa wenyewe apo ndo hitler alipo amua kuwamaliza
israel hii imeshaweka miziz kidiplomasia,kiteknolojia,kibailojia mpaka kijiografia ni ngumu sana mzee baba
 
Netanyahu ni mchumba tu wa USA na EU ukija kwa Putin a.k.a Bear killer, mpaka USA na NATO wanaujua mziki wake.

Wanasema Russia imeishiwa mpaka inatumia mapauro lakini haohao wanataka kupeleka jeshi likasaidie nguvu. Sasa nguvu waongeze ya nini wakati Russia anapigana kwa kitumia pauro 🤣🤣
 
2006 walipigana na hezbollah mpakani mwa lebanon uso kwa uso fuatilia nini kilitokea pamoja na kupewa silahazote kali na washirika wake waliishia kuaibika hadi marekani kaenda kuomba ceasefire umoja wa mataifa, na badala ya hapo mkuu wa majeshi wa israel akajiuzulu
Sasa Israel imefutika? Kinachomshinda Allah na waislam wote kuifuta taifa teule takatifu ni nini?
 
Putin alisema hakuna mtu wa kuingilia vita yake na Ukraine lakini Dunia haikumtii. Hadi nchi kama Poland zinatuma Silaha wazi wazi na Putin hafanyi chochote.Netanyau kasema hakuna mtu wa kusogeza Pua yake Gaza na dunia imetii kabisa.
Kwahiyo kumbe mpaka Poland na yeye ashatuma silaha zake lakini zote zimeshindwa kulitoa jeshi la Russia nchi Ukraine. Hakika Putin anatisha sana.

Sio tu Gaza, bali hezbulla anapiga kabisa ndan ya Israel. Na kibaya analenga mpaka kambi za jeshi za Israel kila siku, na hakuna ambacho Netanyahu ashafanya kuhakikisha jeshi lake na raia wake waliopo mipakani kwake wako salama.

Hivyo Netanyahu bado mchumba tu kwa Putin. Silaha anazopewa na magharibi kila siku zimeshindwa kumsaidia kutokomeza uasi unaoendeshwa na hezbulla.

Putin anatumia silaha zake dhidi ya nchi zaidi ya 10 na bado wameshindwa kumtoa katika maeneo aliyoteka.
 
Kumlinganisha Putin na Natenyahu ni kimvunjia heshima Putin.

Netanyahu ana nini kama yeye kila kitu anafanyiwa na Marekani na Ulaya anapewa pesa anapewa silaha.

putin anapigana vita na Nato na Ulaya na Marekani.

Netanyahu anapigana vita na watoto na wagonjwa leo unaenda mwezi wa 8 hawajui mateka wao walipo Gaza yenyewe ni ndogo kuliko Kigamboni.
Putin vita ya miaka 3 kila kitu Urusi ni made in China na India , ebu tuache ushabiki wa kitoto
 
Netanyahu huwa anaishi kwa kujificha ficha akiogopa kuangushwa na maadui zake. Ila Putin anaenda popote anapopataka yeye bila kumhofia mtu wala nchi yoyote.

Hivi nje ya Marekani ni nchi gani nyingine ambayo Netanyahu ashawahi kutembelea? Hebu nikumbushe mkuu, maana jamaa anajifungia sana.
Netanyahu anaishi kama digidigi, kuingia US huwa hajiamini kabisa.

Putin anakuja hadi Africa, Putin ana maadui wenye nguvu na teknolojia kubwa lakini haogopi mtu, jamaa ni namba.
 
io israel iliopigwa na hitler ilikuwa haina makao maalumu wala haikuwa na jeshi walikuwa wakimbizi nchi za ulaya na kwengine hata ivyo pamoja naukimbizi wao walikuwa ma milionea kuwazidi hata wazawa wenyewe apo ndo hitler alipo amua kuwamaliza
israel hii imeshaweka miziz kidiplomasia,kiteknolojia,kibailojia mpaka kijiografia ni ngumu sana mzee baba
Unazungumzia Israel hii hii ambayo mpaka leo inategemea kila kitu kutoka Marekani, UK, Ufaransa, Ujerumani, NATO ndo ipambane na Russia nchi ambayo yenyewe ndo inategemewa na nchi zingine izisaidie silaha za kujilinda.

Israel hii hii ambayo imekuwa ikipokea misaada ya silaha kutoka katika nchi zaidi ya 5 za magharibi lakini inahenyeshwa na hezbulla wenye silaha chache mno.

Israel isipopewa misaada ya silaha na mabwana zao haiwezi kusavaivu hata miaka miwili.
 
Putin vita ya miaka 3 kila kitu Urusi ni made in China na India , ebu tuache ushabiki wa kitoto
Kuandika tu madai yako bila kuambatanisha na fact, wengi watachukulia kama umeandika tu mipasho badala ya hoja yenye mashiko.
 
Sasa Israel imefutika. Kinachowashinda Allah na waislam wote kuifuta ni nini?
lengo halikuwa kuifuta israel lengo ni kuikomboa palestina na kuitaka israel ikae kwa kuheshimu mikataba ya kimataifa na kiheshimu haki za wapalestina
Kama leo israel anavyohangaika na kutaka kikundi cha mgambo tu kukifuta matokeo yake hadj leo amegeuka kama mwendawazimu mbele ya international community
Gallant simlaumu sana maana siku zote amekuwa akimwambia netanyahu ambaye amekuwa akitaka kubaki madarakani kwa namna yoyote na kiwategemea right wing kama strimogvic na beghvir ambaye last week gallant aliitisha vyombo vya habari na kutoa ujumbe pua kwa netanyahu kwamba hatuwezi kupigana kila siku ,tumepigana inaenda miezi minane only for hamas to go and regroup and come back stronger we need to havr clear plan on post war solution na kumaliza hii vita ambaye inatugharimu
Week later icc inataka kuwakamata
Nato ally france,belgium na norway wameahidi kuheshimu maamuzi ya icc yami kuwakamata netanyahu na gallant
Norway, ireland na spain wamerecornise palestine state
5 senior us state department members akiwemo mwanamama muisrael ambae ana ushawishi mkubwa Aipac na alishiriki kumuweka biden na hariss madarakani wameresign kupinga sera za marekani na israel dhidi ya wapalestina na vita vinavyoendelea
Netanyahu anaiangamiza israel ,na ehud barak alionya kuhusu kuaibika kwa israel kwenye uso wa dunia since january na yote yanatokea kwa haraka sana
 
Niaje waungwana

Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.

Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.

Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.

1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.

Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?

I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.

Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.

Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.

Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.

Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.

2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.

Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.

Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?

Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.

Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.

So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.

Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.

Karibuni sana...
Netanyahu he has backup, while Putin he always standing himself.
 
Kwahiyo kumbe mpaka Poland na yeye ashatuma silaha zake lakini zote zimeshindwa kulitoa jeshi la Russia nchi Ukraine. Hakika Putin anatisha sana.

Sio tu Gaza, bali hezbulla anapiga kabisa ndan ya Israel. Na kibaya analenga mpaka kambi za jeshi za Israel kila siku, na hakuna ambacho Netanyahu ashafanya kuhakikisha jeshi lake na raia wake waliopo mipakani kwake wako salama.

Hivyo Netanyahu bado mchumba tu kwa Putin. Silaha anazopewa na magharibi kila siku zimeshindwa kumsaidia kutokomeza uasi unaoendeshwa na hezbulla.

Putin anatumia silaha zake dhidi ya nchi zaidi ya 10 na bado wameshindwa kumtoa katika maeneo aliyoteka.
Ushabiki huondoa hata akili ndogo iliyokuwepo.
 
Kijana sijui umezaliwa baada ya mwaka 2016, au umeanza kufuatilia international news miaka hii miwili iliyopita.

Hebu soma hizo taarifa zilizotolewa na FBI wenyewe nchini Marekani.
Unachekesha
 
Hana anachojua huyu kazi yake kusoma habari leo na kusikiliza millard ayo atajua wapi habari kama hizi, angekuwa mfuatiliaji wa masuala ya kimataifa asingeweza kubisha vitu obvious kama hivi
Kwamba Trump aliwekwa na Warusi ?
 
Back
Top Bottom