Uchambuzi wako unatokana na chuki uliyonayo kwa Israel! Kulimlinganisha
Putin na Netanyahu kwa lengo la kumdharirisha Netanyahu sidhani kama uchambuzi wako uko fair...
Naona umekimbilia kuandika kiushabiki sana ili kumfichia aibu Netanyahu na nchi yake inayoshindwa kujisimamia yenyewe mpaka leo.
Unaposema et Netanyahu anapambana na nchi zenye utajiri wa mafuta alaf unataja nchi moja tu Iran unamaana gani? Mbona nchi zingine huzitaji? Maana hata hao Iran hawapambani na Israel moja kwa moja, bali ni kwa vitisho vya hapa na pale huku Iran ikiwa na vikwazo vikubwa vilivyowekwa na mabwana wa waisrael kwa zaidi ya miaka 50 bila nchi hiyo (Iran) kuomba poo.
Labda kama unamaanisha Hamas na Hezbullah ambazo sio nchi bali ni vikundi vya watu wachache wanaopigana na nchi yenye jeshi la zaidi ya wanajeshi laki 5 na uchafu.
Pili nimekuona hauna unalojua baada ya kuandika et Israel ina teknolojia kubwa kuzidi Russia. Sikushangai sana kwa sababu vijana wengi huwa mnamezeshwa maneno na kuyameza hivyo hivyo bila kutumia akili zenu kuyachuja ili muweze kufahamu ukweli wa yale mnayomezeshwa.
Hivi inakuaje nchi unayosema inaishinda urusi teknolojia na sayansi itegemee vitu vingi kutoka kwa wazungu. Urusi imesharusha satelite kibao kwenda angani huku Israel ikitegemea zaidi msaada wa wazungu kutengeneza japo kasatelite ki1 na yenyewe ikarushe.
Asilimia 90 ya silaha za Urusi inatengeneza yenyewe, huku asilimia 85 ya silaha za Israel zinatoka Marekani, Canada, UK, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi na nchi zingine za Ulaya.
Muda mungine ushabiki ukizidi sana unamfanya hata mtu mwenye kuonekana ana upeo aonekane mjinga.