Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki

Pwani: Magari yagongana uso kwa uso, wanne wafariki

Wapumzike kwa amani ya Bwana, nishauri kitu kama huna uzoefu au uhakika wa safari ndefu tena usiku usijaribu,wapo madereva wengi wazoefu unaweza omba wakusaidie tupunguze ujuaji vitu vinavyoweza hatarisha maisha yetu
 
Bora upande yale madaladala yanayoendeshwa na wanywa viroba usiku?, bora utembee tu Mkuu

nimewahi kupanda daladala kutokea Buguruni kwenda Kawe, Dereva kama vile akili aliziacha buguruni usiku ule tukielekea Kawe, nilishuka Mkwajuni nikabadili daladala
Dereva daladala aliyekunywa viroba anaweza kuwa anaendesha vizuri gari kuliko madereva wengi sana wa maofisini ambao wamenunua leseni. Nina ndugu zangu wa SADC wakija Tanzania ndio wananunua leseni wakazitumie nchi zao, wana uzoefu wa kuendesha magari ila wakifanya test chances za kufeli kule kwao ni kubwa.

Kuna maelfu ya waendesha daladala jiji la Dar ila nadra kusikia daladala limeua watu wanne kwa ajari. Na yanakimbia kila usiku na kila alfajiri, na madereva wanakunywa wengine mida trafiki hamna, na wana fatigue kila siku, wanakuwa na usingizi kila siku. Uzoefu wao usiuchukulie kawaida.
 
Ndo akina msuya hawa??
Hujawaho kwenda kwenu..miaka na miaka..baba yenu anawaita njoo nyumbana niongee nanyi..mnajifanya busy..mnachofanya ni kumchukua mama yenu na kukaa nae mjin na baba anabaki kijijin akiwa hana msaada wowote huku AMEINAMISHA nafsi yake kwa sababu ya matendo yenu...linakuja kutokea tatizo kubwa pasipo kureconcile na baba yenu mnajibeba mnaenda.........
toa ubuyu wote sio nusu nusu
 
Yes mkuu,ujue watu wana-base kusema mama/bana hata awe kichaa ni baba/mama tu,No ni uongo,binafsi sipatani na mama mzazi kabisa,kaniacha mikononi mwa baba nikiwa na mwaka mmoja na miezi minne,baada ya mwaka mmoja kabeba mimba na kuzaa na mwanamme mwingine,bila ya kuja hata kuniona,I was to die,ila mungu akawa upande wangu.

Hadi sasa nikisikia mtu anasema nani kama mama huwa nakasirika sana,nafarijika sana nikisikia nani kama baba,
ATUKUZWE BABA
 
Mara nyingi usiku ma dreva wa kweli huwa wao wanalala na gari humuachia tingo wake nae aongeze ujuzi wa kuendesha! Sasa unakuta tingo anajifunza mwenyewe, maana Mwalimu wake ambae ndiyo dereva Mkuu kalala fofofoo!!
All in all wapumzike kwa Amani japo kuendesha gari usiku kama sio mzoefu ni risk sana bcoz mambo mengi yanafanyika usiku hasa tusisahau muda wenyewe ni mmbaya wenye barabara yao pia wapo kazini muda huo.
Risk nyingine ni kusafiri familia moja kwa pamoja kwenye gari bcoz ikitokea msiba unakuwa mzito zaidi kwa wanafamilia kwa ujumla
 
Ni kweli mkuu km50/h kama unaenda mbali ni changamoto ila mafuta yanaliwa sana ukiendesha above 119km/h. Ila 50-119km/h consumption ni nzuri. Speed nzuri ni 80km/h pale vibao vinaporuhusu.


Sahihi. Na hata kama una uzoefu, ni bora kuutumia badala ya kuupuuza ukaanza kukimbia hovyo.

Usingizi ni hatari. Hata mm imeshanitokea mara mbili sababu ya kujiona nina uzoefu. Sasa hivi nina adabu na barabara.
Yes kwa barabara zetu speed 80 - 100 sio mbaya sana, sema watu wqnaendeshea sifa, kama unataka kufika sehemu saa flani weka masaa 2 mengine ya ziada (mfano safari inachukua masaa 8 ondoka masaa 2 kabla ili uweze ku-balance speed in case barabarani kuna foleni etc.
 
Yes kwa barabara zetu speed 80 - 100 sio mbaya sana, sema watu wqnaendeshea sifa, kama unataka kufika sehemu saa flani weka masaa 2 mengine ya ziada (mfano safari inachukua masaa 8 ondoka masaa 2 kabla ili uweze ku-balance speed in case barabarani kuna foleni etc.
Sahvi watu wengi wanaendesha magari ovyo tu
Mtu anakimbiza gari bila sababu yoyote

Ova
 
We jamaa namna gani???
Huyu kama angekuwa dereva asingesinzia....wangapi wanafanya kazi mchana kutwa na usiku wanakesha.2.tairi linakatikaje??? Au wazungumzia ''BASTI'' 3.Kama ni ball joint au tire road end zilileta shida...alikagua gari kabla ya safari...kama ndio...ni garage ipi?...hapa tujifunze...je?macho ya dereva (prado}na taa za scania.....kwa nini apige scania asipige pori?????
PRADO MCHAGA zina tatizo la kukatika ball Joint bila kutarajia. Kwa ujumla prado siyo gari.
 
Back
Top Bottom