Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Niliitwa na jamaa yangu mmoja....akawa ananiambia kuna siku ataniita nije nione ujasiriamali aufanyao. Nikawa najaribu kudadisi nijue anajihusisha na nini katika biashara yake mpya? Jamaa akawa hataki kusema, akidai nitajua tu siku nikienda.

Kichwani nikaanza kujiuliza inawezekanaje kama mtu amefungua biashara na hataki watu waijue? Hapo tayari nikachezwa chale.siku ikawadia akanipigia simu jioni akanielekeza, nikafika ofisini.

Kwa nje inaonekana ni nyumba tu ya kuishi watu, kumbe ndani ni ofisi. Nikapokelewa na zile goodmorning etc...kuona mabango tayari nikawa nimewatambua. Qnet.

Kwenye semina nikasikiliza stori za mamilioni...then nikauliza swali kuwa toka nimeingia humo kwao sijaona Certificate of incorporation ya kampuni yao, sijaona TIN ya kampuni, sijaona leseni ya biashara n.k ktk mazingira hayo nawezaje kuwekeza kwenye entity ambayo haitambuliki?

Wakaanza kujikanyaga, mara walionyeshwa kwenye taarifa ya habari, mara waziri alikuja kuzindua ofisi yao, mara sijui gazeti liliwaripoti,...tayari nikahitimisha kuwa these people are after my hard earned money. Nilipoondoka sikurudi kwa semina ya pili.
 



oyaaaaaaaaa si wslikupeleka kuleeee mikocheni b kwenye ki chochoro Chao???? ?
 
ngoja tuendelee kupigwa labda tutashituka huko mbeleni
 
Ahahaha am global walikuta na vitu vyangu kichwan halafu nilitoka kutapeliwa kilo SITASAHAU ILE SIKU
 
Hawa jmaa wanatapeliwa alafu na wao wanafundishwa kutapeli wengine. Process zao ni moja. Watakuambia njoo oficn kuna semina unafika unakuta wamejipanga kuanza kukutapeli wewe.
 
Kuna dem amenitafuta sana wiki ya pili hii simjui ila anapiga simu anasema tuonane kuna ishu ya maana tukajadili lakini hasemi ni nini.sasa namvutia upepo tu amesema weekend hii tukutane makumbusho.ila nazani ni hizi mambo
Kma ni makumbusho usiende[emoji23][emoji23]ndo ofisi zao zilipo.kuna mxkaji alitumiwa msg na dem flani anasoma ardhi akaambiwa kuna kazi inahusu mambo ya health.anahitaji vijana wanne.mxkaji wangu akanitonya mm na wana wengne watatu,tumetoka IFM na mvua kubwa kishenzi adi makumbusho,kufika makumbusho tumelowa mana alituelekeza twende kwenye crdb ss sisi tukaenda millenium tower branch ya crdb kumbe alimaanisha ATM ya crdb iliokuwepo makumbusho stand pale.tulivyokutana nae tushalowa vibaya sana af ndo katupandisha ofisini kwao pale juu akaanza kutuambia huo upuuzi.
 
HAO BHANA NAWAOGOPA HAO TOKA WAMSABABISHIE MAANANGU MMOJA CHUO ALE ADA HADI LEO WAMESHIKILIA CHETI CHAKE SHENZI HAWA AFU MMOJA WA HAWA MADADA NI CLASS MATE WETU CHUO FLANI HVI..... BACK IN DAYS
 
Unanikumbusha GNLD mwaka 2011 kipindi nipo A level kuna best yangu alitumia pesa yote ya kupiga mapindi tuition kwa mudi physics kisa kujiunga na GNLD

Alikua anajisifia mafanikio ya maisha bora na mkwanja mrefu wakati kiuhalisia tulikua tunasota kwa kushindia mihogo na maji kandoro ya miamia kwa mgosi mwisho alikuja kukiri alitapeliwa tuliporudi shule baada ya likizo kuisha na kudai kazi ilikua ngumu sana mana ni kujenga network ya watu

Alijitahidi kunishawishi kinoma ili namimi nijiunge but sikuwa interest ukizingatia shule ya PCB A level ilivyo kuwa ngumu sikutaka kuchanganya madesa
 
Sipati Picha, hahahaha
 
Wanajiita upcoming billionaires hahahaha dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…