Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Q-Net na Forever Living zimenipotezea marafiki zangu wa karibu

Mimi binafsi mwaka jana walinipiga kwenye D9, Sitaki tena kusikia hizi longolongo za Qnet.Shemeji yangu yeye ndio kwanza ameingizwa huko na kaingiza hela zake, akanialika nikaenda kuwasikiliza na kuwasilikiza nikasema hawa wapuuzi kabisa yaani kwa tumaneno twao uto ndio niiingize mkwanja wangu!!!??? Hapa hata machungu ya D9 Hayajaisha. Hawanipati kabsaaaa.
Njia nzuri ya kuwaelimisha watu ni kuwaeleza ulishawishiwa vipi hadi ukawaamini, ulitoa kiasi gani, ulitegemea kupata nini baada ya wakati gani, ulichukua hatua gani n.k

Haijalishi hata kama watu watakukejeli lakini wengi watakuwa wameelimika.
 
Anaweza kuwa wa Qnet huyo. Au Network Marketing nyingine.

Kuna dem amenitafuta sana wiki ya pili hii simjui ila anapiga simu anasema tuonane kuna ishu ya maana tukajadili lakini hasemi ni nini.sasa namvutia upepo tu amesema weekend hii tukutane makumbusho.ila nazani ni hizi mambo
 
Huwa hawasemi mpaka ukifika... Ndo mi wanachoniudh. Ni utapel tapel tu.

Kuna kidem changu cha chuo kwasasa yupo likizo ila yupo bze sana namaswala ya pesa yn kama yupo ofis flan ivi zamichongo yapesa sasa leo ndo nimepata jibu mana juz kati alinitext "Habari Majan Samahani kesho kama hutojali naomba Uje ofcn Kwetu saa nane kuna program muhimu kwa wageni nakuomba nimekununulia ticket" ila kila nikimuuliza ofis zao zinahusika na nini hajawai kuniambia
 
K
Njia nzuri ya kuwaelimisha watu ni kuwaeleza ulishawishiwa vipi hadi ukawaamini, ulitoa kiasi gani, ulitegemea kupata nini baada ya wakati gani, ulichukua hatua gani n.k

Haijalishi hata kama watu watakukejeli lakini wengi watakuwa wameelimika.
Kweli mkuu
 
Kwa mtazamo wangu, na kwa wale wachache waliosoma na kuelewa na kukubali utafit wa Robert Kiyosaki kwny ktabu chake cha "rich dad poor dad" na "cash flow quadrant"., nakubali kua. .........only 10% of the people are operating from the I-quadrant.......... Me nadhan kwa nchi zetu za kiafrika hasa Tz...., this percentage is approaching to zero.
Ndo maana hata kw wale walio kweny "network martng" wanapata ugumu huo kutafuta watu weny uelewa wa aina hii ya biashara. Nashauri kwa wale wanaopenda kujiunga na aina hii ya biashara wasikurupuke tu.
Ni vema ukasoma vema, au hudhuria semina za kutosha za net.market tofauti tofauti, linganisha, harafu ndo ufanye maamuz ya kuingia. Binafs bado sipo huko. Ila wapo watu wamefanikiwa sana kupitia hizo.
Ni vema tukafanya utafiti wale walioshindwa, wameshindwa kwasababu gani.?
 
Mnanichekeshaga mnavofananisha FOREX na hizo mavitu zenu, forex yenyewe ni tofaut na story nyepes alizoleta Ontario. Inajumuisha kupoteza pesa nyingi, kutokulala kwa ajil ya kusoma PDF mbalimbali, vidonda vya tumbo Soko linavoenda against you.... Naomba watu wa jf msifananishe forex na vitu vya kijinga

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa yangu ni askari magereza, kila tukikaa kwenye vikao vya 'viti virefu' huwa haachi kugumia maumivu ya kupigwa 6 Mil za Qnet.... Wasiwasi wangu nadhani ipo siku atamfyatulia risasi mtu wa Qnet aliyemuunganisha.[emoji23]
 
Nina jamaa yangu daily haishi kunishawishi nijiunge na Qnet. Nishahudhuria hadi seminar zao lakini sikuwa na mpango wa kujiunga.
 
Kwa mtazamo wangu, na kwa wale wachache waliosoma na kuelewa na kukubali utafit wa Robert Kiyosaki kwny ktabu chake cha "rich dad poor dad" na "cash flow quadrant"., nakubali kua. .........only 10% of the people are operating from the I-quadrant.......... Me nadhan kwa nchi zetu za kiafrika hasa Tz...., this percentage is approaching to zero.
Ndo maana hata kw wale walio kweny "network martng" wanapata ugumu huo kutafuta watu weny uelewa wa aina hii ya biashara. Nashauri kwa wale wanaopenda kujiunga na aina hii ya biashara wasikurupuke tu.
Ni vema ukasoma vema, au hudhuria semina za kutosha za net.market tofauti tofauti, linganisha, harafu ndo ufanye maamuz ya kuingia. Binafs bado sipo huko. Ila wapo watu wamefanikiwa sana kupitia hizo.
Ni vema tukafanya utafiti wale walioshindwa, wameshindwa kwasababu gani.?
Umesema vyema..!
 
Kuna kidem changu cha chuo kwasasa yupo likizo ila yupo bze sana namaswala ya pesa yn kama yupo ofis flan ivi zamichongo yapesa sasa leo ndo nimepata jibu mana juz kati alinitext "Habari Majan Samahani kesho kama hutojali naomba Uje ofcn Kwetu saa nane kuna program muhimu kwa wageni nakuomba nimekununulia ticket" ila kila nikimuuliza ofis zao zinahusika na nini hajawai kuniambia
Sjui kwa nn mambo yao hua wanayaweka Siri Sana. Hata bidhaa zao ukiuliza bei longo longo kibao mara tuonane kwanza mara nn hadi ujue bei labda umbane Kweli. Pesa rahisi sijawahi kuzifikiria.
 
Qnet nawasifu sana kwa mbinu za kushawishi na kuwatoa watu ufahamu (brainwashing) hasa wanachama wao. Ukiwa na tamaa lazima upigwe, lakini ukitulia na akili zako timamu na ukijiuliza maswali ya msingi utajifunza jinsi watu wengi walivyokata tamaa za maisha, wanavyopenda kutafuta fedha na maisha bora kwa njia za mkato.

Kuna jamaa yangu mmoja namheshimu sana, siku moja aliniomba tuonane akisema kwamba 'ana jambo zuri angependa kunishirikisha', akisisitiza kwamba 'kizuri kula na mwenzio'. Tukakutana jioni moja mahali fulani tulivu akiwa na wenzake ofisini kwao waliponitambulisha Qnet, wakinipa ushawishi kwamba baada ya muda mfupi sitahitaji kufanya kazi tena, maana fedha zitakuwa zikitiririka kama maji. Ndani ya dakika tatno moyoni nilishafanya maamuzi kwamba sitajiunga nao kwenye biashara hii, lakini nikajiambia acha niwasilikize na niwaulize maswali maana sikuwa cha kupoteza, na huenda nikajifunza kitu. Yule jamaa yangu alionekana sio msemaji sana, inaonekana kazi yake ilikuwa kunishawishi nifike pale halafu kuna 'mkuu' fulani aliyepangiwa kuongea na mimi akiwa na uhakika kwamba nitaingia. Kwa nyakati tofauti niliwauliza swali moja tu ambalo hadi leo hakuna hata mmoja wao aliyenipa jibu si huyu 'mkuu' wala yule jamaa yangu. Niliwauliza kila mmoja wao anioneshe kwa mifano hai wamepata mafanikio gani kupitia Qnet, wakashindwa nami nikawaambia kwamba itakuwa vigumu kwangu kuingiza fedha mahali ambapo wewe mwenyewe unanishawishi sioni jinsi unavyofanikiwa. Nikamwambia jamaa yangu kwamba siku mambo yake yatakapokuwa mazuri anijulishe nami nitajiunga. Hadi leo mimi na yule jamaa yangu mawasiliano yamekatika.
 
Kuna mwalimu wangu wa A level nlikua namuheshimu kweli...mwezi uliopita akanipigia simu anasema tuonane . Me nikajua anataka nikafundishe kwenye tution center yake. Kufika pale wana mbwembwe balaaaaaaa yaan kama sio mtoto wa mjini unapigwa hivihivi
Ofisi yenyewe imechoka balaaa haina hata meza halafu ananishawishi nijiunge nao niwe nalipwa millioni 9 kwa wiki. Ila to my amazement nimekuta hadi vijana wa chuo wamezama kwenye huo upuuzii......NETWORK MARKETING NI PYRAMIDAL SCHEME KAMA ZILIVYO NYINGINE USIIBIWE KIJINGA
yah mkuu hiyo ndo pyramidic scheme, mnawanufaisha waleee wamwanzo ninyi namna uhakika wa kupata ama kurudisha hela, dahh haya mambo tunapigwa pigwa tuuu kishamba kwakutaka hela mtelezo
 
pole kaka nimempoteza rafiki kipenzi kwa sababu ya Qnet

Hata anipigie simu sipokei kwa sasa na bahat mbaya ukienda Qnet hta kama ni usiku utaambiwa Goodmorning

watu wana mashati yaliyochakaa na viatu vilivyoisha soli cha ajabu wanakuelezea return ya mamilioni!!!
 
Back
Top Bottom