Qatar ilipata utajiri kutokana na gesi. Kwanini Tanzania ilizuia miradi ya gesi?

Qatar ilipata utajiri kutokana na gesi. Kwanini Tanzania ilizuia miradi ya gesi?

Magufuli alikuwa serikalini kipindi mikataba hiyo inapitishwa na hakupinga chochote, kwa nini sasa?
Upinge kitu wakubwa wameamua wewe kama nani ? Muulize yule aliyesalimu amri ! Utaishia kusema nimekosa mimi nimekosa sana! Na haitasaidia kitu ! Ndio maana Katiba mpya ni muhimu !!
 
Mfano wako haupo relevant mkuu kuicompare Qatar na nchi za kiafrica Tena Tanzania.

Sisi ngozi nyeusi hatuwezi kuzisimamia Mali zetu, tumejaa ufisadi. Angola ilitabiriwa uchumi ungepaa na maisha ya wananchi yangekuwa mazuri Kama ulaya baada ya kuanza kuuza mafuta lakini mambo yakaenda tofauti na matarajio ya wengi, nchi bado Ni masikini Hadi leo. Msumbiji wameanza kuuza gesi yao, wacha tusubiri Kama uchumi wao utabadilika.

Hakuna kukata tamaa kwani hao watu weupe walipitia mambo kama ya kwetu!
Una kumbuka Libya? Sasa hivi walibya wamekuwa omba omba, hilo ni fundisho kwa nchi nyingi sana!
Ombea nchi yako, ipende nchi yako, walahi tutafika!
IMG_5518.jpg
 
Kwa kifupi kabisa, Tanzania inahitaji Reformation ya hali ya juu sana.

No sacrifice, No Liberation.
Ni lazima Watanzania angalau hata 500000 kati ya Watanzania wote 60,000,000 wajitoe sadaka kwa ajili ya kuikomboa Nchi hii kutoka kwenye Wimbi la uharibifu.
Matatizo yanayopelekea Nchi hii kuendelea kuwa maskini ni pamoja na:-
(1) Ufisadi, Rushwa, Ubadhirifu, Wizi wa mali za umma na Ubinafsi.

(2) Uzembe makazini na kuogopana au kuoneana haya.

(3) Mihimili ya Serikali kutokuwa huru na hivyo kutofanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu zake.

Kwa hiyo, bila kujilipua kwa lengo la kuondoa MAKANDOKANDO haya, Tanzania itaendelea tu kuwa maskini.
 
Ukimwondoa Nyerere, hakuna hata wa kumkaribia JPM kwa utendaji kazi mzuri kama Rais.
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Tukiachana na siasa na maneno ya majukwaani, Maamuzi ya mwenyekiti na raisi wa awamu iliyopita ya kuachana na gesi yalipata baraka za chama na watanzania walikubali mbadala uliopendekezwa.

Mafanikio ya hii nchi yanatokana na chama cha mapinduzi, makosa yalikipa chama changamoto mpya na malalamiko yalifanyiwa kazi na chama.

Pamoja na yote, CCM ni chama pekee chenye uwezo wa kupewa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi hii.
 
Thinking yenu huwa siielewi kabisa, mmekaa kimihemko na ushabiki sana, hamjui kufikiria vizuri kabisa, kwenu ni bora siku ipite kwa kumtaja Magufuli, ili mkila ugali upite vizuri kwenye koo.

Wewe unaamini tatizo la umasikini/poor decision nchi hii lililetwa na Magufuli, wala huoni kama ni la kimfumo, sasa mbona lilishakuwepo hata kabla ya ujio wa Magufuli?

Mbona hujiulizi, licha ya madini tuliyonayo, ikiwemo Tanzanite, yanayopatikana Tanzania pekee bado tuko nyuma kimaendeleo, kwanini uamini hiyo gesi inayopatikana maeneo mengi duniani ingetutoa kwenye umasikini? kwa usimamizi gani? wa CCM hii hii?!

Umasikini wa akili ndiyo umasikini mbaya zaidi kupata kutokea duniani. Namuunga mkono Mwal. J. K. Nyerere.

Halafu la pili, tujitahidi kuelimishana kizazi hiki na kijacho kwamba CCM si Tanzania. Tujaribu kuitenganisha Nchi yetu Tanzania na CCM. Pia Tanzania si CCM. Kuna watu wanajaribu kuonesha kwamba hakuna tofauti kati ya Tanzania na CCM. Wanajifanya kwamba wana machungu na CCM ambayo ni sawa sawa kuwa na mapenzi na Tanzania. Kitu ambacho ni uongo, uchunguzi unaonesha kwamba watu wengi wananufaika na keki ya taifa na rasilimali za Tanzania kwa kupitia CCM. Huwezi kuneemeka na mema ya nchi hii kiujanja ujanja, bila ya kupitia CCM. Hivyo CCM inatumika kama kichaka cha kupora mema ya nchi yetu. Naweza kusema kwamba, hujuma za nchi hii zinaanzia huko.
 
Ktk mfumo wa nchii hii ulojengwa,ni ngumu sana kutenganisha hili genge na nchi
Umasikini wa akili ndiyo umasikini mbaya zaidi kupata kutokea duniani. Namuunga mkono Mwal. J. K. Nyerere.

Halafu la pili, tujitahidi kuelimishana kizazi hiki na kijacho kwamba CCM si Tanzania. Tujaribu kuitenganisha Nchi yetu Tanzania na CCM. Pia Tanzania si CCM. Kuna watu wanajaribu kuonesha kwamba hakuna tofauti kati ya Tanzania na CCM. Wanajifanya kwamba wana machungu na CCM ambayo ni sawa sawa kuwa na mapenzi na Tanzania. Kitu ambacho ni uongo, uchunguzi unaonesha kwamba watu wengi wananufaika na keki ya taifa na rasilimali za Tanzania kwa kupitia CCM. Huwezi kuneemeka na mema ya nchi hii kiujanja ujanja, bila ya kupitia CCM. Hivyo CCM inatumika kama kichaka cha kupora mema ya nchi yetu. Naweza kusema kwamba, hujuma za nchi hii zinaanzia huko.
 
Kwani Magufuli si alisema yeye ni kiboko ya mabeberu? Kwa nini alikubali gesi yetu ikauzwa bure alipokuwa serikalini kisha aje kulaumu?
Na kwa nini asiingie mikataba mizuri alipokuwa Rais?
Samahani mkuu unajua maana ya Ministerial responsibility?
 
Upinge kitu wakubwa wameamua wewe kama nani ? Muulize yule aliyesalimu amri ! Utaishia kusema nimekosa mimi nimekosa sana! Na haitasaidia kitu ! Ndio maana Katiba mpya ni muhimu !!
Si ndio uzalendo huo? Magufuli hakuwa mzalendo?
 
Samahani mkuu unajua maana ya Ministerial responsibility?
Abgejiuzulu, kama alikuwa mzalendo na akaona nchi inapigwa vibaya na wewe unajua na hupingi wala kujitenga nao, wewe pia ni fisadi papa
 
Samahani mkuu unajua maana ya Ministerial responsibility?
Abgejiuzulu, kama alikuwa mzalendo na akaona nchi inapigwa vibaya na wewe unajua na hupingi wala kujitenga nao, wewe pia ni fisadi papa
 
Ktk mfumo wa nchii hii ulojengwa,ndi ngumu sana kutenganisha hili genge na nchi

Hakuna ubishi hapo, hiyo ni kazi ngumu sana. lkn lazima tufikirie namna bora ya kutenganisha dora na chama chao.
 
Back
Top Bottom