Haya kumekucha tena, kumekuwa na trend ya members humu jamvini ya kuzungumzia Qur'an kimasihara kuhusu habari za vita ya huko palestine, wakati nakuandalia majibu hapa, nikushauri
Mhaya ukasome uzi umeanzishwa na
Bams kuhusu mambo haya haya na ameshaukimbia uzi wake.
pili, israeli iliyotajwa kwenye Qur'an ni nabii yaaqub mtoto wa ishaqa mtoto wa ibrahiym amani iwe juu yao wote, huyu jina lake ni israeli, na israeli kwa kiarabu maana yake ni abdullah, yaani mja wa allah kwa kiswahili.
"
Kila chakula kilikuwa halali kwa wana wa israeli isipokuwa alichojiharamishia israeli mwenyewe kabla haijateremshwa torati, sema: Leteni torati muisome ikiwa nyinyi mnasema kweli."
Qur'an 3:93
Utaona hapo Allah amemtaja nabii yaaqub ambaye ndiye baba wa watoto 12 ambao ndio chimbuko la koo zote za wana wa israeli, kwahiyo kwa ufahamu wako nchi inakula sio? taifa la israeli limeanzishwa mwaka 1948 hata babu yangu amesharudi kutoka vita ya pili ya dunia.
Mahali pengine ukikuta imetajwa banii-israeli basi wakusudiwa ni watoto wa yaaqub na kizazi chake, na pamechimbuka mitume wengi kati yao, kama yuusuf, mussa, yoshua mwana wa nuun, haarun, daudi, sulaymaan na wengineo.
Kwa kumalizia naona umetaja ahadi Allah alizochukua kwa wana wa israeli, mbona haunukuu muendelezo kuwa wao walizivunja ahadi hizo? tizama mfano:
"
Na kwa hakika alikujieni musa na hoja zilizo waziwazi, kisha mkajifanyia ndama (kumfanya muabudiwa wenu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu."
"Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): yashikeni kwa nguvu haya tuliyokupeni na msikie, wakasema: "Tumesikia na tumekataa!" na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya kumuabudu) mwana ndama kwa ukafiri wao, sema: Ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu mkiwa ninyi ni wenye kuamini."
Qur'an 2:92-93
Kwa ufupi Qur'an imewasema vibaya sana wana wa israeli kwa ukafiri wao na kiburi chao cha hali ya juu, mara nyingine uzungumzie mambo unayoyajua kwani ardhi ya palestine ndio imetajwa kwenye Qur'an mara kadhaa na ardhi ya israeli haijatajwa hata moja kwani hakukuwa na jambo kama hilo katu.
"
Enyi watu wangu! ingieni katika ardhi takatifu ambayo Allah amewaandikieni, wala msirudi nyuma ya visigino vyenu, msije mkawa ni wenye kupata hasara."
Qur'an 5:21
"
Ninamtakasa kumtakasa yule aliyemchukua mja wake sehemu katika usiku kutoka msikiti mtukufu wa makkah mpaka msikiti wa aqswa, ambao tumevibariki vilivyouzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya alama zetu, hakika yeye ni msikivu, mwenye kuona."
Qur'an 17:1
Hizo aya zimetaja ardhi ya palestine, ambayo Allah ndio aliwaandikia wana wa israeli wakati wa musa wakavunja ahadi na wakatolewa tena, sasa kuja hapa kutupigia kelele kuwa israeli imetajwa mara 36 basi jua hapo anakusudiwa yaaqub amani iwe juu yake au wanawe, ama ardhi ya palestine ardhi ya quds, msikiti wa aqswa vimetajwa katika Qur'an mara kadhaa.