Quran imetaja tu mirathi kwa idadi ya sehemu na wanaostahili..hiyo yako hapo juu mgao wa milion ni yenu kwa hizi hesabu zenu za kubumba toka kwa mtu asiyejua lolote kuhusu mirathi ya kiislam..nilipoona umechanganya watoto na wazazi wa aliyeacha mali yaani babu na bibi wa hao watoto nikajua ni famba tu toka wachafuzi wa uislam kwa mambo wasiyoyajua..kwani inafahamika mgao unaanza kwa mke/mume na watoto..iwapo aliyeacha mali hakuwa na mke wala mtoto basi ndio wazazi wake wanaingia nao kama hawapo wanaingia kaka na dada zake yaani mambo yanaenda hivyo ngazi ngazi..acheni na hizo habari zenu za kuokoteza aya moja kwa wahuni wanaokashifu uislam kisha wanazipa tafsiri feki kwa sababu wanazojua wao
Dah! Mkuu kwanza punguza maneno makali pili mimi ni muislamu lakini hapa umeghafilika aya ya 4 surat nisaa inaelezea vizuri sana kwamba wazazi watarithi katika situations mbili kama kuna watoto na kama hakuna watoto pia watarithi kinachozidiana ni kiwango .
Tukirudi kwa muuliza swali kwa situation kama hii hukmu ya 'awl' (العَول) itabidi iingie na hii haipo kwenye quran moja kwa moja ila ni jambo ambalo swahaba walilifanya na ni pindi tu kiwango cha jumla baada ya mirathi kugawanywa kitazidi kiwango sahihi cha mirathi hesabu yake itakuwa hivi.
1. WARITHI
Mume amefariki na kuacha :
MKe
Binti wawili
Wazazi wake (baba na mama)
Urithi wa Shilingi Milioni 1 (TZS)
2. MGAWANYO KULINGANA NA QURAN
1. Mke → atapata 1/8 ya urithi (kwa sababu kuna watoto).
Chanzo: Qur’ani 4:12.
2. Binti wawili → watapata 2/3 kila mmoja (kwa sababu hakuna mtoto wa kiume ).
Chanzo: Qur’ani 4:11.
3. Wazazi:
Baba → atapata 1/6 (kwa sababu kuna watoto), na pia anaweza kupokea sehemu ya ziada.
Mama → atapata 1/6 (kwa sababu kuna watoto).
Chanzo: Qur’ani 4:11.
4. SEHEMU YA VIWANGO KULINGANA NA QURAN
Mke= 1/8
Binti wawili (kila mmoja atapata) = 2/3
Baba= 1/6
Mama=1/6
5. MAHESABU
Tutafute kigawanyo cha jumla .
unaweza kutumia LCM au prime factorization approach( hesabu za form 1 hizi hope sitomuacha mtu) nitatumia prime factorization kwa sababu kwangu naona ni nyepesi
Mke 1/8 = kigawanyo=8= 2³
Binti wawili (kila mmoja atapata) 2/3=kigawanyo=3¹
Baba na mama ( kila mmoja atapata) 1/6= kigawanyo=2¹ × 3¹
chukua jumla ya vigawanyo vikubwa na vipeo vyao kisha zidisha kwa pamoja
= 2³ × 3¹= 8×3=24
Hivyo kigawanyo cha jumla ni 24.
Tutafute kigawanyo cha jumla cha kila mrithi .
Mke 1/8 =1/8×3/3=3/24
Binti wote wawili 2/3=2/3×8/8=16/24, kwa mmoja atapata 8/24
Wazazi kila mmoja= 1/6×4/4=4/24
JUMLA YA VIGAWANYO= 3/24+16/24+4/24+4/24=27/24=1.125 , kiwango cha jumla ni kikubwa kuliko 1 bi maana kimezidi kiwango sahihi kama mtoa mada alivyoleta , sasa hapa ndipo awl inaingia pindi kiwango cha jumla baada ya mgawanyo kikiwa kikubwa kuliko kiwango sahihi hivyo itabidi kiwango cha jumla kigawanywe katika sehemu 27 sawa (ambayo ni idadi ya jumla ya vigawanyo tulivyopata hapo juu) kisha mgawanyo ufanyike kuanzia hapo kulingana na sehemu ya kila mrithi.
Hivyo 1,000,000/27=37,037.04 Tshs.
HIvyo mgawanyo mpya utakuwa .
1. Mke ana 3/24 ya kiwango cha jumla hivyo =3×37,037.04=1111,1111.12 Tshs.
2. Watoto wa kike wote wana 16/24 ya kiwango cha jumla hivyo =16/2 =8 idadi ya kila mmoja = 8×37,037.04= 296,296.32 Tshs.
3. Baba ana 4/24 ya kiwango cha jumla = 4×37,037.04= 148,148.16 Tshs.
4. Mama naye ana 4/24 ya kiwango cha jumoa =4×37,037.04=148,148.16 Tshs.
JUMLA MPYA BAADA YA 'Awl'=111,111.12 +296,296.32 + 148,148.16 + 148,148.16 + 296,296.32= 1,000,000/= Tshs
Allah ( The almighty) anajua zaidi.