Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa. Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie. Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Hapo ni muda wa kujipima pia imani... usifanye maamuzi yyte ya kumdhuru mkeo au rfk ako
Mwanamke ndio anaweza kua chanzo kikubwa cha yeye kutongozwa..... Kwa hyo fanya na tafakali kabla ujaamua chchte
 
We jamaa unasema unaendelea kukusanya ushahidi, hiv hujui maana ya mtu anapokwambia amevumilia mpka amechoka! Ina maana yeye ameshindwa hyo vita amekuachia wewe mumewe kwahyo na ww ukiendelea kusubiri hvyo ndo unampa jamaa ushindi na ataliwa we subiri hvyohvyo
Mbona akitongozwa na wngine halalamiki?hamuwajui wanawake nyie
 
JAMAA MWENYEWE MLEVI

HANA PESA, UMEMWAMBIA NIPO HAPA

PESA YENYEWE YOTE ATALEWEA
 
Usiniongezee machungu nitamfanya mbaya sana
Usiwe na hofu mkuu angekuwa ameshakula mwanamke asingethubutu kukwambia hizo habari.

Ushauri wangu: Mwambie kama umeshajua na mwambie aache hiyo tabia, kwa kusema hivyo tu atakata mguu kabisa maana ni aibu, wanaume huwa tunafadhaika sana tunapokataliwa na wanawake tunaowaheshimu. Usithubutu kabisa kumtega usimwambie mke wako aigize kumkubalia ufumanie yote hayo ya nini? Unaweza kufanya hivyo ukajikuta mke wako akavutiwa na jamaa anampa bila kukwambia.
 
Hivi nyie vijana mliooa hua mnakua na ujasiri gani wa kuwakaribisha marafiki zenu tena mabachela kwa wake zenu?
Hivi hamjui kua mashemeji hua wana ladha special kuliko mademu wengine?
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbona akitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
Dah kweli asee hapo changanya na akili yako
 
Nilikua namtongoza mke wa jamaa angu sana...yule mwanamke hakunikataa kabisa ila kumbe akamwambia jamaa...
Jamaa alinipigia simu akanichana live ...tokea siku hiyo nikamuacha yule mwanamke na jamaa ni best yangu ile mbaya....

Cha ajabu sasa yule mwanamke ndio ananifanyia visa mi namuogopa yaani anazidisha ukaribu hatari...
Nimeamua nimkwepe... kwa hiyo fanya kama jamaa alivyonifanyia....!
 
Kwa ushauri tu
Kwanza lazima umwambie wife asije akakuambia ujinga huo kuwa flani kanitongoza

Kwa sababu utagombana na kuwachukia wangapi kama yeye kila amtongozae atakuambia

Mwambie ajitetee mwenyewe na ajibu mapigo kama yeye bila kukushirikisha la sivyo atakufanya ufe upesi
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa. Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie. Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipigia simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Rafiki yako usimwambie chochote kwakua hajafanya mapenzi na mkeo,wangefanya mapenzi wala mkeo asinge kwambia kama anatongozwa
 
Kwa ushauri tu
Kwanza lazima umwambie wife asije akakuambia ujinga huo kuwa flani kanitongoza

Kwa sababu utagombana na kuwachukia wangapi kama yeye kila amtongozae atakuambia

Mwambie ajitetee mwenyewe na ajibu mapigo kama yeye bila kukushirikisha la sivyo atakufanya ufe upesi
Kwa kawaida ni rahisi kuwakataa wale wanaume ambao hawana uhusiano na mume wako (ndugu au rafiki).

Lakini hawa wanaojifanya marafiki inakuwa ni ngumu sana, wengine hata ukimwambia awache na akome bado atakuganda kama kupe mpaka neno litoke kwa rafiki yake ndiyo akome.
 
Nikiamua siwezi kudelay nitakuwa na chat na mke wangu kila hatua wanayopiga, mpaka watakuta tumelipia chumba kabisa. Kazi yake kutuambia namba ngapi tu basi
Kama hiyo stori sio ya kutunga basi ichukulie kwa mawazo mapana...wanawake huwa wanapenda kuwini kama wako perfect au waaminifu kwa ishu kama hizo.Kuna mambo ya kujiuliza kabla ya kutenda,jee huyo ni mwanaume pekee aliyemtongoza toka muwe pamoja au na wengine wanaomtokea huwa anakuambia au kaona ni rafiki yako???Pili upate ushahidi wa mtongozo kutoka kwake ili kujiridhisha.Kama ukajiridhisha basi unaweza kumfuata na kumueleza kwa evidence kuwa aache hiyo ishu.
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa. Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie. Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipigia simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Muite mpe kichwa kimoja!harafu mwambie akae mbali na wife wako,si kwa vile una wivu ni kujaribu kuweka mipaka,
Ningekuwa Mimi namchapa makomde huyo rafiki,kwa sababu ameingilia himaya yangu,na kunivunjia heshima.
Mfano ikitokea kumbe wife ameishamzimia jamaa,na wanataka wawe pamoja,Wala sifanyi fujo,namwambia wife tuachane vzr,hata mchango wa harusi naweza wapa.
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa. Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie. Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipigia simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Mwambie tena kwa meseji tu
 
Back
Top Bottom