Rafiki Yangu above 30 Hana Nguo za Heshima, Kabati Lake Limejaa Jeans!

Gentleman,
kwani harusini hawaruhusu uvaaji wa t-shirt na jeans au ni athari ya dhana iliyojengeka miongoni mwa fikra za wengi?

halafu,
kwani jeans sio vazi la heshima?🐒
Zari the boss lady aliwafukuza wote walio vaa t-shirt na jeans kwenye jambo lake, juzi tu hapa alidai sio heshima kwenda kwenye hafla na hayo mavazi ya kuendea disco
 
Hiyo sherehe mlienda kule Siha?
Itakuwa Bukoba hiyo, Nina jeans nyingi hata idadi sijui, Nina suti pia. Bahati nzuri kazi zangu sehemu kubwa ilikuwa field hivyo suti zinasubiri matukio makubwa lakini nyingi zinaishia kuvaliwa mara moja au kutovaa kabisa. Kwangu jeans ni vazi la heshima kabisa.Mwenzangu mmoja alifariki, wakati najipanga kwenda kuaga nikaona tangazo wanaume wote mvae suti.
 
Mwenyewe haoni shida..muache avae anavyojisikia...aibu utaona wewe...
 
Aisee mimi from monday to monday ni mwendo wa jinsi na tshirt ndio mavazi navaa kazini. Suruali za kitambaa ninazo sijui tatu na mpaka nivae ni shughuli....

Anyway for a gentleman muhimu kuwa na nguo kwa ajili ya matukio flani flani. Koti, suruali ya kitambaa, kadeti, moka mchongoko....
Ila kwenda harusini na jeans mbona fresh tu.

Mimi classmate wangu mmoja alikuja kwenye harusi yangu na jezi ya arsenal na jeans😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…