Rafiki Yangu above 30 Hana Nguo za Heshima, Kabati Lake Limejaa Jeans!

Rafiki Yangu above 30 Hana Nguo za Heshima, Kabati Lake Limejaa Jeans!

Itakuwa Bukoba hiyo, Nina jeans nyingi hata idadi sijui, Nina suti pia. Bahati nzuri kazi zangu sehemu kubwa ilikuwa field hivyo suti zinasubiri matukio makubwa lakini nyingi zinaishia kuvaliwa mara moja au kutovaa kabisa. Kwangu jeans ni vazi la heshima kabisa.Mwenzangu mmoja alifariki, wakati najipanga kwenda kuaga nikaona tangazo wanaume wote mvae suti.
Kwa hiyo ukashindwa kumuaga rafiki yako kisa umevaa jinsi 😂
 
Suti haimfanyi mtu kua wa heshima bali mtu ndiye anayeifanya suti kua ya heshima.
At times huwa unaongea Madini sana

Ulichosema ni kweli Sheikh, sio eti Mtu anavaa suti halafu anenda kupanda baiskeli au anakula maembe from hand to mouth bila kuyakata ni kuivua heshima suit.
 
Kwani yeye ndio anaoa.!?

Mtu uko pembeni unashuhudia watu.. Na hatokuja peke yake shida nini hata akivaa bukta
 
Mimi huwa napendelea kadeti, na shirt mikono mirefu. Suti labda niwe kamati kabisa
 
Halafu naona kama kaunda zimetulia kuliko suti ila kwa wale wembamba sio wale vifutu
Kaunda ndio bado sijazielewa.
Mimi ni mpenzi wa english suit. Koti na suruali tofauti.
Tai yangu safii.
NIna jeans na cardet pia za kutosha, za aina tofauti. Ngumu na kitambaa chepesi. So sometimes nakula jeans kitambaa lain na koti ya suti ndani tshirt nyepes popote pale unaingia hata church.
Raba, buti Moka hiz zote lazima kama sio muhimu uwe navyo kwenye cabinet yako
 
Kaunda ndio bado sijazielewa.
Mimi ni mpenzi wa english suit. Koti na suruali tofauti.
Tai yangu safii.
NIna jeans na cardet pia za kutosha, za aina tofauti. Ngumu na kitambaa chepesi. So sometimes nakula jeans kitambaa lain na koti ya suti ndani tshirt nyepes popote pale unaingia hata church.
Raba, buti Moka hiz zote lazima kama sio muhimu uwe navyo kwenye cabinet yako
Kuna kaunda suti ni kali sana bwashee suti naona kama kila mtu anavaa imezoeleka mno🤔
 
mimi navaa vazi lolote, kokote ilmradi ni safi, ila koti la kuwapumbaza kidogo nipo nalo standby kokote & in office.
But kamwe siwezi kuumiza kichwa kuhusu kuvaa au mwingine kavaaje 🐒
Noma. Sana 😁
 
Nimepata mwaliko wa harusi ya rafiki yangu iliyoko mkoa mwingine.

Nikasema, ngoja nimtafute rafiki yangu mwengine anayeishi huko ili twende pamoja, tupige story na kufurahia sherehe. Si unajua kwenda harusi peke yako vibe linapoa !

Nikamcheki nikamwambia, Bro, nina harusi ya rafiki yangu hapa kwenu, twende pamoja. Jiandae tupendeze!

Jamaa akasema, Hakuna shida

Lakini nilipomuuliza kuhusu mavazi, ndipo nilipoanza kuona giza! 😭🤣

Kumbe miaka yote hii jamaa hajabadilika hata kidogo! Kabati lake limejaa jeans, T-shirt na sneakers. Suti hakuna, shati la heshima hakuna, hata blazer ya kujifanya mjumbe wa kamati haipo!

Nikajiuliza, huyu mtu anaenda harusini au anakwenda kwenye miaka 30 ya bongo fleva ?

Cha kushangaza zaidi, jamaa ana miaka zaidi ya 30, lakini kabati lake unahisi bado yuko kidato cha pili!

Sasa nimebaki njia panda. Nimwambie atafute suti ya kuazima, au akodishe
Shida ni nini! Hizo nguo hazikuamkia?
 
Back
Top Bottom