Rafiki yangu anakaribia kuoa kimyakimya bila wazazi na ndugu zake kujua

Rafiki yangu anakaribia kuoa kimyakimya bila wazazi na ndugu zake kujua

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,217
Reaction score
3,694
Baada ya wazazi wake kumkataa binti ambaye alikuwa ana mipango ya kumuoa kwa sababu wazazi wanazozijua wenyewe.

Jamaa yangu sasa anakaribia kuoa kimya kimya bila wazazi na wala ndugu zake kuwashirikisha wala hawajui chochote kama anaowa na amefanya hivi sababu wazazi wake wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwake.

Je, hii imekaaje wakuu?
 
Ni muhimu kuoa unayempenda na kumchagua kuliko kuoa yule unayesukumiwa.

Ingawa ndoa inaingiliwa kwa kushauriwa pia sio kichwakichwa tu
 
Dunia yetu msingi wa Nyota zetu ni migongo ya wazazi wetu. Pamoja na utandawazi ila wazazi wanaona mbali mno kwenye masuala mazima ya Ndoa.

Binafsi mchumba ambaye wazazi walimkataa sikumuoa na hiyo ilinitokea mara mbili, nikifika home Bi mkubwa akanambia hapo hakuna ndoa piga chini huyo mwanamke hata iwe umempenda vipi, akinisisitiza nitumie akili zaidi kwenye kuchagua mke bora na sio MOYO.

Wa pili Dingi akanichana hapo unaoa JIWE hutopata maendeleo.

Nikatafuta pisi moja ya Kichaga, home ukawa Mziki sitokaa nisahau, kilichonisaidia ni ile mwanamke alishaamua kubadili dini na alikubaliana na mila zetu za Kimakonde. Wazazi wakaridhia, now life ni full furaha madogo wanachagua waende Moshi au Mtwara kupumzika na kote wanakuwa na furaha.

NB. Ukiona ndoa yako wazazi wanaikataa sana achana nayo utakuja kupata misala ambayo hutokaa ujue nini chanzo.
 
Atakuja kujuta mwambie aache wenge wazee wanaona mbali kuliko yeye siku yakimfika ndo atajua hajui.
 
Muache aoe mtu alompenda yeye sio walompenda Wazazi

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Kuoa unatumia akili sio MOYO. Moyo unaweza kumuonea huruma mtu malaya, mfujaji wa mali, kiburi, asiye na heshia kwako nk. Lkn AKILI haiwezi kubeba huo ujinga. Hivyo fikiria hoja za wazazi kwa makini utagundua wako sahihi.

Wakati mwingine unalazimisha kuona Familia ambayo msingi wake una WACHAWI wengi hivyo kukupelekea ww na familia yako kujiingiza kwenye uchawi nk.

Ubishi wa kijinga haufai.
 
Labda nitoe kisa kimoja kwa ufupi
Kuna demu nilipata namba zake kutoka sehemu nikamcheki. Kiujumla demu ni mzuri sana hivyo nikaliendeleza nione mwisho wake. Baada ya siku 3 za mawasiliano ikawa imefika jmosi ambayo tulitoka usiku baada ya kufanya mazoezi ya jioni pamoja. Huo usiku tulikaa mahali na usiku uliposonga akaomba twende club. Hiyo siku sikuomba utelezi maana kwa jinsi alivyo nikajua aliomba twende club may be alikuwa anatamani ila anakosa wa kwenda nae so kwakuwa tulishazoeana sana ndani muda mchache hivyo aliniamini.

Kisa chenyewe ni baada ya siku kama 4 nikaomba utelezi ili nijue muafaka kabla sijachana mkeka ila yule demu aliniambia ANATAKA LAKI 1 nikamwambia kiutani hadi mimi unaniuzia hakujibu. Nikamwambia mm nina 30k round 1 akaniambia baki na dau lako.

Jana nikagundua kumbe ni mke wa mtu na wana mtoto mmoja ila inavyoonesha jamaa anajua mke anafanya biashara katika mkoa niliko kumbe mkewe anajiuza kwa dau kubwa

Ushauri: suala la ndoa lisiamuliwe kwa kuangalia utakapokuwa unachomeka, wazazi huwa wanaliona hili japo hawawezi kusema direct bali watakueleza kwa njia nyingine. Ikumbukwe ndoa ni taasisi ambayo ukikosea basi kizazi na maisha yako yatakuwa ya majuto.
 
Acheni kutisha watu Kwani wasabi ndo wako sahihi Kwa kila jambo mm walinikatalia nikao na kukawa na watu kama nyie leo mwaka wa12 nipo tu fresh kimaisha sijatoboa sana ila. Niko kwenye kundi la 2%
Atakuja kujuta mwambie aache wenge wazee wanaona mbali kuliko yeye siku yakimfika ndo ataju
 
Japo wazazi wetu wanatutakia heri lakini ikumbukwe kuwa wazazi pia si wakamilifu mara zote kuwa sahihi,

Itakua ngumu kutoa ushauri sahihi kupitia maelezo hapo juu, zaidi itakua ni betting ambayo timu wazazi wanauwezekano mkubwa kushinda japo mpira ni dk 90 na chochote kinaweza tokea.
 
Tutumie point zile zile tu maarufu;

1: Lack of Capital
2: Un skilled labour
3: Poor infrastructure
4: Low technological advancement
5: Poor working facilities

Conclusion: Muache aoe tu asiwajulishe ndg zake
 
Back
Top Bottom