Rafiki yangu anakaribia kuoa kimyakimya bila wazazi na ndugu zake kujua

Rafiki yangu anakaribia kuoa kimyakimya bila wazazi na ndugu zake kujua

Inategemea wanatoa sababu gani, mwingine unakuta hana sababu ya msingi anakwambia tu hapo usioe/usiolewe.
Ikumbukwe wazazi nao ni binadamu.
 
Baada ya wazazi wake kumkataa binti ambaye alikuwa ana mipango ya kumuoa kwa sababu wazazi wanazozijua wenyewe

Jamaa yangu sasa anakaribia kuoa kimya kimya bila wazazi na wala ndugu zake kuwashirikisha wala hawajui chochote kama anaowa na amefanya hivi sababu wazazi wake wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwake

Je hii imekaaje wakuuu

Kama una nafasi ya kumshauri mwambie atakuja kujuta Sana, anaweza Kuwa Na msimamo wa kuoa n kuwaalika wakatae, ila most of the time wanakujaribu , ukionyesha msimamo wanatulia.

Huwezi Fanya hiyo kitu bila Ndugu, Baba na Mama wakikataa una wajomba Na marafiki wanaweza kuwashauri, mambo marahisi Sana sema Vijana baada ya balee Na vitz za mikopo mnakuwa Na kiburi Sana.
 
Hapa ndipo watu weusi tunakwama sana.
Swala la kuoa ni swala mtambuka, na unapo oa haumuolei ndugu wala mzazi. Pia kukosea kuoa kupo tu hata ukiletewa mke na wazazi hii haijalishi kwamba huyo ndie mke bora. Minadhani swala la mke bora ni kumuomba Mungu kwa imani yako ili akuonyeshe yule alie bora.
 
Huyo jamaa yako wazazi wake walikataa walitoa sababu gani? Kuwa wazazi haimaanishi wako na busara sana ama wana maono ya mbali. Wangeweza pia toa baraka zao na bado ndoa ikaja kubuma ya mbele hayajulikani.
 
Hapa ndipo watu weusi tunakwama sana.
Swala la kuoa ni swala mtambuka, na unapo oa haumuolei ndugu wala mzazi. Pia kukosea kuoa kupo tu hata ukiletewa mke na wazazi hii haijalishi kwamba huyo ndie mke bora. Minadhani swala la mke bora ni kumuomba Mungu kwa imani yako ili akuonyeshe yule alie bora.
Sio tatizo bali ni mila za watu weusi na jamii nyingi pia duniani hasa Asia.

Kuna mwanafalsafa (Mbiki) anaelezea vizuri ktk kitabu chake kuwa "African mind is attached to past" yaani kila kitu kuheshimu wahenga na wazee wakiwamo wazazi. Hii kitu kwa jamii nyingi ya kanda ziwa watakuwa wanajua ikiwa wazee hawajabariki jambo ni ngumu kutoboa labda uwe umesimamia imara imani yako.

Ni vizuri kuwa huru kifikra na kuamua mwenyewe, lakini bado kiroho wazazi wanabakia kuwa miungu.

Tukitaka mind zetu ziwe oriented to future kama ilivyo kwa wana magharibi inatupasa kubadilika pakubwa sana
 
Mara nyingi wazazi huwa wanaona mbali japo mengine ni ya kizami but most of them huwa wanaona kitu at first wanapomuona bibie,
Haina shida hata ikitokea yamemwendea kombo akae kimya hivohivo
 
Ni muhimu kuoa unayempenda na kumchagua kuliko kuoa yule unayesukumiwa.

Ingawa ndoa inaingiliwa kwa kushauriwa pia sio kichwakichwa tu
Changamoto unaweza ukampenda mtu lakini akawa sio mwanamke wa kuoa sio kila mwanamke anafaa kuolewa,wengine wa kupiga na kusepa
 
Changamoto unaweza ukampenda mtu lakini akawa sio mwanamke wa kuoa sio kila mwanamke anafaa kuolewa,wengine wa kupiga na kusepa
Daah eeer bn huu ndio ukweli, maana kuna wanawake unawezapenda kwelikweli ila unajua kabisa nikiweka ndani hii mtu nitakua nimenunua ng'ombe moja kwa kutoa ng'ombe tano.

Ila na ww si ni mwanamke ndugu au ni avatar tu???
 
Ila wazaz saa ingine wanarusha steam sana, maisha ni yake acha mtu aoe anayemtaka afurahie maisha yake.. Maisha yenyewe mafupi haya halafu umpe mtu msongo wa kuishi na mtu asiye mpenda.. Kiufupi itakua hivi.. Mtaani pesa ngumu na nyumbani ndoa ngumu... Kwanin msikubaliane tu mkaweka muafaka mzuri maisha yakawa na amani na kesho mkasaidiana mambo mengine.. Sasa wazazi wanataka jamaa aforce mambo alafu arudi kunyenyekea kila kitu kama mtoto wa kambo kumbe ni mtoto wenu wa mkumzaa...
Nb: Mwambie jamaa ako hatuombei mabaya lakini shida zipo, ajiulize kesho akipata shida kubwa kama kufiwa, msiba ataufanya wapi... Akipata jibu arudi akakubaliane na wazee wake ndoa yake ifanyike kwa amani na maisha mengine yasonge mbele... Pole ndugu unataka kuingia kwenye mtihani mzito
 
Kuoa unatumia akili sio MOYO. Moyo unaweza kumuonea huruma mtu malaya, mfujaji wa mali, kiburi, asiye na heshia kwako nk. Lkn AKILI haiwezi kubeba huo ujinga. Hivyo fikiria hoja za wazazi kwa makini utagundua wako sahihi.

Wakati mwingine unalazimisha kuona Familia ambayo msingi wake una WACHAWI wengi hivyo kukupelekea ww na familia yako kujiingiza kwenye uchawi nk.

Ubishi wa kijinga haufai.
Yeye ndo kampenda muache amuoe...... Hao Wazazi awataenda kuish na huyo mke bali ni yeye muoaji

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Aachane na huyo mchanga atakuja kuuliwa na kuleta kizazi cha walevi
 
Wèeeeeee

Kibongo bongo mke ni wa wazazi wako...dada zako....kaka zako...wajomba zako na ukoo wako

As if wataishi nae vile

Khaaa!!!!
Hapa ndipo watu weusi tunakwama sana.
Swala la kuoa ni swala mtambuka, na unapo oa haumuolei ndugu wala mzazi. Pia kukosea kuoa kupo tu hata ukiletewa mke na wazazi hii haijalishi kwamba huyo ndie mke bora. Minadhani swala la mke bora ni kumuomba Mungu kwa imani yako ili akuonyeshe yule alie bora.
Halafu kila mtu ana haki ya kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa.

Wasipoendana kuna mahakama watatalikiana.

Kuna wengine wanakubalika na wazazi lakini kumbe ni vijinga vya moto!!!!
 
Daah eeer bn huu ndio ukweli, maana kuna wanawake unawezapenda kwelikweli ila unajua kabisa nikiweka ndani hii mtu nitakua nimenunua ng'ombe moja kwa kutoa ng'ombe tano.

Ila na ww si ni mwanamke ndugu au ni avatar tu???
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe ndo uyo jamaa unataka kuoa bila wazazi kuridhia

Wewe oa ila yatakayokupata wazazi watasema 'walikwambia'
 
Wèeeeeee

Kibongo bongo mke ni wa wazazi wako...dada zako....kaka zako...wajomba zako na ukoo wako

As if wataishi nae vile

Khaaa!!!!Halafu kila mtu ana haki ya kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa.

Wasipoendana kuna mahakama watatalikiana.

Kuna wengine wanakubalika na wazazi lakini kumbe ni vijinga vya moto!!!!
Kuna vitu ni ruhusa kukosea, ila sio kwenye swala la mwenzi (mke/mme)
 
Back
Top Bottom