Dunia yetu msingi wa Nyota zetu ni migongo ya wazazi wetu. Pamoja na utandawazi ila wazazi wanaona mbali mno kwenye masuala mazima ya Ndoa.
Binafsi mchumba ambaye wazazi walimkataa sikumuoa na hiyo ilinitokea mara mbili, nikifika home Bi mkubwa akanambia hapo hakuna ndoa piga chini huyo mwanamke hata iwe umempenda vipi, akinisisitiza nitumie akili zaidi kwenye kuchagua mke bora na sio MOYO.
Wa pili Dingi akanichana hapo unaoa JIWE hutopata maendeleo.
Nikatafuta pisi moja ya Kichaga, home ukawa Mziki sitokaa nisahau, kilichonisaidia ni ile mwanamke alishaamua kubadili dini na alikubaliana na mila zetu za Kimakonde. Wazazi wakaridhia, now life ni full furaha madogo wanachagua waende Moshi au Mtwara kupumzika na kote wanakuwa na furaha.
NB. Ukiona ndoa yako wazazi wanaikataa sana achana nayo utakuja kupata misala ambayo hutokaa ujue nini chanzo.