Anapandikizwa embryo yaani kijusi baada ya mbegu ya mwanaume na yai la mwanamke kuunganishwa kwenye zile tubes za maabara kisha kijusi kutokea ndio wanachukua kifaa maalumu anaingizwa ukeni kisha kupandikizwa kile kijusi kwenye mji wa uzazi na mimba inatunga kama kawa.
Mtoto akitoka anakuwa na DNA za baba na mama yake wa asili huyu mwanamke anakuwa hafananii DNA hata chembe na mtoto. Na sharti ni moja mtoto akizaliwa anachukuliwa pale pale , haruhusiwi hata kumuona maana wengine huwa wanajikuta wanaumia kumuacha tena mtoto alietoka tumboni kwake ingawa si wake tena.
So huwa wanaamka tu na kukuta mtoto hayupo na hawaruhusiwi kumuona.
Ni maamuzi magumu sana mtu kuchukua.
Ukitaka kujua zaidi ingia online tafuta '"''Surrogacyc"''"