Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Mtoto mdogo aki testify uongo inajulikana.
Mtoto chini ya miaka kumi muulizi kitu zaidi ya mara tano ukiona mara ya tatu anatoa taarifa inayopishana na ya kwanza, basi jua cha kwanza ni uongo.
Ukimuuliza mara ya sita ashasahau yale aliyolishwa atautapika ukweli wooteee.
Hii mbinu mahakama ya mirathi Chang'ombe Temeke nimeiona.
 
1. Usiingilie yasiyokuhusu.
Hiyo NI Kanuni Namba Moja.

2. Ikiwa utaingilia, Basi kuwa mwangalifu, chukua tahadhari na Work smart.

Sikuona sababu ya Mtoto kuteseka Miaka nenda Rudi alafu kumbe NI Mtoto WA Mshikaji wako.
Ulishindwa nini kumwambia mapema kama kweli ninyi NI marafiki?

Siku zote mnapoonana mnazungumzia mambo gàni ya maana?

Alafu unampaje shemeji zawadi Kwa Mtoto asiye wake, Kosa.
Unampaje Zawadi shemeji àmbaye tayari ushajua anaroho Mbaya?

Kama wanauwezo wa kumnunulia nguo na Viatu huyo Mtoto na hawajamnunulia, ulikuwa na uhakika gani nguo utakazopeleka huyo Mwanamke angempa azivae?

Ninyi mnasema Wanawake NI wabaya lakini ubaya wa Mwanamke mara nyingi hutokana na uzembe wa Mwanaume.
Mfano huyo Mwanamke kama ungekuwa smart Sana Wala huyo ràfiki yako msingegombana.

NI aidha ungemwambia Mshikaji pekeake, au Siku uende ukamchane live wakiwa wôte wawili ili shemeji asipate Nafasi ya kuongea uongo.
Akibisha unamwambia Dogo aitwe aulizwe.

Maana huyo ràfiki yako ungeweza kumwambia mapema lakini akitoka akaenda kumuuliza Mkewe akapewa tàarifa potofu na Hali ikawa kama ya Sasa.

Siku ñyiñgine kama Huna best solutions NI Bora usiingilie Kesi za Watu.
Wengi wamekufa Kwa sababu hizohizo
 
ulikosea, kabla ya kununua hizo nguo ungeongea na jamaa na kumpa full story kuhusu mateso ya mtoto wake. Badala ya kumkabidhi nguo huyo mama wa kambo.
 
Ok mkuu
 
Umetoa mfano mzuri mkuu. Nahisi uliemwambia amekuelewa.
 
ulikosea, kabla ya kununua hizo nguo ungeongea na jamaa na kumpa full story kuhusu mateso ya mtoto wake. Badala ya kumkabidhi nguo huyo mama wa kambo.
Sikutegemea wala kufikiria kama haya yangetokea mkuu. Najilaumu sana.
 
Umetoa mfano mzuri mkuu. Nahisi uliemwambia amekuelewa.
Nimehudhuria kesi za familia mara kadhaa mahakama ya Chang'ombe.
Dogo alikua kamezeshwa uongo dhidi ya babaake alooo!!
Dogo kaulizwa mara ya pili ya tatu kakanganya maelezo,wakamshusha pembeni apumzike sakata lilivyoendelea kafunguka yote mama aibu mahakamani.
Huwa wanashindwa ku recall yale waliyomezeshwa.
 
Ni kweli mkuu 🤣🤣🤣
 
Waswahili walikuwa na msemo kwamba "tenda Wema uende zako"
Kakosea wapi jirani hapo? Mbona mara nyingi amekua anatenda WEMA na anaenda zake, au mi ndio sijaelewa? Mtoto amekua anapewa chakula, pesa za kununua vitu vidogo vidogo na baadae kaamua kumnunulia nguo; hajawahi kutangaza popote (according to the story ) isipokua baada ya kukutwa na hi!
 
Learn to mind yout own business
We mtoto wa mjini lakini inakuwaje kufatilia mambo ya watu,utakuja kufungwa siku kwa uzembe wako,dunia ya kibepari hii,bora ungeripoti kwenye mamlaka husika sio kumnunulia mtoto nguo,big mistake
Kwahiyo ile slogan ya "mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako" kwa watoto wa mjini waachane nayo?
 
Makosa ni yako mwenyewe, katika khali ya kawaida haiingii akilini kumnunulia mtoto wa mwenzako nguo bila sababu ya msingi.
Ulichotakiwa kufanya ni kukusanya ushahidi na kumuonesha baba mtoto changamoto alizokuwa anapitia mtoto na siyo kumnunulia nguo utafikiri baba yake aneshindwa kufanya hivyo.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi, nina imani uliem quote kakuelewa vizuri sana 🙏
 
Jirani alikuwa anatenda Wema lakini akaishia kulipwa ubaya

Ndiyo maana nimesema "tenda Wema nenda zako"
 
Huyo shemeji mkongo ana kalio la maana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…