rafiki yangu msabato akiri yapo mafundisho kinyume na Biblia yaliyoingizwa kanisani mwao analaumu kanisa katoliki lengo lao kuwavuruga kiimani

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Nilikuwa naongea na Msabato mmoja rafiki yangu kuhusu Kanisa kuruhusu baadhi ya mafundisho au Imani zinazoenda kinyume na Biblia

Katika mazungumzo yetu nilimtajia mambo mawili tu ambayo yameruhusiwa Kanisani karibuni kuwa ni kuruhusu wachungaji wanawake , idara ya wanawake pamoja na fundisho la holly trinity doctrine

Nilimwambia na kumpa ushahidi kuwa hayo hayakuwepo kabla na yameingizwa kimakosa kwenye Kanuni za Kanisa

Ndugu yangu Wala hakunibishia baada ya kumpa ushahidi ila Cha ajabu akidai kuwa hizo ni njama za wakatoliki kuharibu Kanisa lao.

Nilijaribu kumuomba anipe ushahidi alishindwa na aliendelea kutupa lawama kwa Kanisa hilo kuwa limeweka mapandikizi kuvuruga Kanisa

Sijaona logic kwenye madai yake kwani kwa mfano Kanisa Katoliki hawana huduma ya wachungaji wanawake

Naombeni mnishauri
Niwatakie Dominika njema
 
Mafundisho ya 'holy trinity' yalianzishwa na mhubiri aitwae Qintius Septimius Florens(tertullian) mwaka 213BK.Mafundisho haya yalikosoa mafundisho ya Praxeas mwaka 206BK yaliyohubiri Mungu mmoja asiyegawanyika.Nicean decree ya mwezi juni 325BK ndiyo iliyoingiza dynamic monarchianism(Mungu katika kiti cha enzi aliitwa baba,Mungu kavua utukufu wake na kuzaliwa na mwanadamu aitwa mwana na Mungu karudi kitini na kuachilia nguvuze aitwa roho mtakatifu) na huu ndiyo utatu mtakatifu.
 
ChatGPT ina majibu:
Screenshot_20250222_165441.jpg
Screenshot_20250222_165441.jpg
 
Wadau hamjamboni nyote?

Nilikuwa naongea na Msabato mmoja rafiki yangu kuhusu Kanisa kuruhusu baadhi ya mafundisho au Imani zinazoenda kinyume na Biblia

Katika mazungumzo yetu nilimtajia mambo mawili tu ambayo yameruhusiwa Kanisani karibuni kuwa ni kuruhusu wachungaji wanawake , idara ya wanawake pamoja na fundisho la holly trinity doctrine

Nilimwambia na kumpa ushahidi kuwa hayo hayakuwepo kabla na yameingizwa kimakosa kwenye Kanuni za Kanisa

Ndugu yangu Wala hakunibishia baada ya kumpa ushahidi ila Cha ajabu akidai kuwa hizo ni njama za wakatoliki kuharibu Kanisa lao.

Nilijaribu kumuomba anipe ushahidi alishindwa na aliendelea kutupa lawama kwa Kanisa hilo kuwa limeweka mapandikizi kuvuruga Kanisa

Sijaona logic kwenye madai yake kwani kwa mfano Kanisa Katoliki hawana huduma ya wachungaji wanawake

Naombeni mnishauri
Niwatakie Dominika njema
Yaani Sabato kushindana na katoliki ni sawa na Mashujaa kushindana na Yanga au Simba, levels zake ni Kengold, kimsingi levels za Sabato ni akina mwamposa, nk
 
Au nzi kukaa juu ya mgongo wa tembo🤣
 
Au nzi kukaa juu ya mgongo wa tembo🤣
Yaani kila wakihubiri, ooh Papa kafanya ivi, ooh 666 ! Ooh vatican, hawamtaji hata huyo muanzilishi wao Elen white wala nn, kuna rafk yangu ilikuwa kila tukikutana akiwa anatoka kanisani namuuliza leo mmesemaje kuhusu papa? Akawa anacheka tu hanijibu. Alafu uzuri mmoja huwezi kusikia hata siku moja kanisani katoliki wakiwa wanazungumzia Sabato, yaani wao wanaendelea na mambo yao tu
 
Back
Top Bottom