Rafiki zangu wanapooa ukaribu wetu hupotea ghafla, nini kinawapata huko?

Mie naona hata kwa ma-Ex tunaowasiliana baada ya kuachana.

Wiki moja au hata mbili kabla ya harusi yake atakupigia mwenyewe mkaongea ila akiolewa tu ni kimya hata miezi sita.

Wakichokana huko ndani ndo anakutafuta tena.
 
Mwanamke ukimwoa anakuja na principle zake, kuna jamaazangu yani simu usipige kuanzia saa moja wakiwa home lazima ipite kwa wife alafu wife akiipitisha ndio jamaa anapokea hata kama mna deal la pesa , kuna jamaa mwaka jana ivo ivo nlikuwa na ishue nae ya hela nimepiga simu haipokelewi , kumbe simu anayo mwanamke me niajipanga nkatafuta mshikaji mwingine tukaenda kwenye ishue nikavuta m2 , kesho linakuja kuzinduka lina buku 5 mfukoni yule mwanamke anataka hela akaanza kupiga simu kama kichaaa, sijawah kuipokea hiyo simu, WANAWAKE WANABUGISHA MUDA MWINGINE AISEE ACHA KABISAA
 
Hii inafanana na wazazi wanapo chagua marafiki kwa watoto wao.

Lakini mtoto mwenyewe anajua mtu fulani ni msaada gani kwake ,hakuna urafiki usiokuwa na faida mtu anaweza kuwa muhuni ila unamuhitaji kama rafiki kwa kiasi fulani ana msaada wake.

Wanawake wengi haijalishi wapoje ila hawapendi wanaume zao wawe na marafiki wanaopenda kukaa maskani na kazi hawataki ,huu ndio ukweli wanawake wanapenda kuona mume anazunguka na kama ana marafiki wawe na faida kwake za kiuchumi kama kazini au kufanya biashara.
Vikundi vingine ni wale marafiki wa escort kwenda kweny starehe na kunywa pombe.
 
TUKO HAPA SIO!😀😀
 
Hujui kama maisha ya binadam yana dhama 4.
Dhama ya utoto
Dhama ya ujana
Dhama ya familia
Dhamaya uzee

Sasa wewe unataka kila dhama uwe na watu haohao haiwezekani..
Kwani ukiwa ktk zama/ "dhama" ya ujana huwezi kuwa na familia ? Wazee hawana familia?
 
Wamekatazwa na wake zao hivyo usife moyo maana wanawake ni wabinafsi sana.

Ila sisi wanaume tukisha kua na wanawake hatupotezeani maana tunajua kabisa lolote linaweza kutokea gafla, ila wavulana wakisha oa wanatupotezea kabisa nasiku ya kimkuta anaanza kuchanga karata ni namna gani ya kujirudisha kwa aibu ila hatunaga mbaya tunawapokea kijiweni kiroho safi maana tunajua wake zao ndiyo wamewakataza
 
Mwanamke hata aje na principle zake hatakiwi kukutoa kwenye msitari, lazima uwe mwanaume.. wanafeli
 
Ahahh kumbe! Basi nimeujua ukweli
 
Najaribu kuimagine jinsi anavyopigwa marufuku 🤣
Wawe wanatoa taarifa sasa😅
 
Mwanamke hata aje na principle zake hatakiwi kukutoa kwenye msitari, lazima uwe mwanaume.. wanafeli
Mkuu unapoengea nalo kihusu hii ishue anakuwa anasikiliza kwa makini lakin vitendo sasa ndio hamna kitu, kuna siku hivyo hivyo tumepiga ishue ambayo yeye ndio alikuwa front, tukapata M3 , bila aibu likanipa la mbili, laki nane kaenda kumtunza yule mwanamke wake kwenye birthday yan huku mimi naona, mtu kama huyu mbona ugonjwa wake hawez pona mkuu, mwanamke mimi hanibadilish msimamo wangu hata iweje…
 
Siyo wanaume tu, hata wanawake wakishaolewa wanakataa urafiki na rafiki yake kindaki ndaki, hata simu hapigi kisa kaolewa doooh!! Wanakosea sana [emoji13]
Kwa wanawake thats a big yes to me. Wanawake wengi maadui ni wanawake wenzenu tena wanaopenda kujifanya mashosti zenu wa kupika na kupakua. Hutaamini siku huyo rafiki yako asiyeolewa akianza kutembea na mume wako yani lazma roho ikutoke. Ila yapo yanatokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…