Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Yawezekana ni protokali za kijeshi mkuu.
 
Muombolezaji naye anazingua,akaenda mazima barabarani,kit u ambacho kinahatarisha hata kibarua cha huyo askari,maana angegongwa na gari ya msafara,sidhani kama askari angebaki na kibarua.Pole kwa mpigwaji.
 
Very nice comment. Angefanya hivyo lingekuwa jambo la busara. Hili tukio limeniuma sana.
Mkuu wakati mwingine hata sisi raia tunakuwa wajinga. Kilichotokea wakati wa kifo cha Magufuli kilinifanya nifikirie mara mbili kuhusu mazishi ya viongozi. Wale waliokufa kwa kukanyagana walikuwa wengi kweli kweli lakini serikali ikadanganya idadi. Kuna jamaa alikwenda kumcheki ndugu yake vyumba vya maiti vya hospital za Muhimbili na Amana akasema kulikuwa na maiti nyingi sana. Na serikali haikujali hata kidogo ilifanya kama ni mbwa wamekufa. Imefika wakati kwa raia kuacha kujipanga au kwenda kwenye mazishi ya hawa viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…