Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

C396CD1E-CB78-432B-98C9-1BF19FFFAD43.jpeg

====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
 
Huyu akipelekwa ubaoni hachomoki especially hilo kosa la matumizi mabaya ya madaraka watamdaka mapema mno maana alikuwa anasumbua watu then mwishoni hakuna kinachotokea zaidi ya kuwapakazia watu Mambo ambayo amekosa ushahidi.
 
Kosa linaloitwa matumizi mabaya ya madaraka ni gumu kulitolea ushahidi mbele mahakama ya haki bila kuonyesha kuwa alitumia madaraka hayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Akitumia madaraka hayo kukutisha linaweza liswe kosa la jinai bila viongezi vingine.
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Saabaya.

View attachment 2010778
Jenerali Ulimwengu ameamua rasmi hili gazeti liwe tabloid sasa kama ya Shigongo. Hakuna tena zile makala za kiuchambuzi mtu unasoma unaridhika. Sad!
 
Back
Top Bottom