Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aiseee nadhani CCM walikuwa wanaomba Trump ashindweIla nadhani kwa watanzania ni bora trump ashinde ili bwana pompeo aendeleze harakati zake
Hesabu zikiwa hivyo hivyo,sioni Biden atachomokea wapi.Trump atashinda na Georgia Pia.Wisconsin, Michigan & Pennsylvania zinampa ushind View attachment 1619227View attachment 1619228View attachment 1619229View attachment 1619230
Unajua kwanin waliliita international forumSawa, kwa hiyo sisi huku Tanzania tufanyeje na maisha yetu, tusifanye kazi au kuwaza?
Tatizo Trump anakwenda kushinda majimbo yenye point nyingi. Trump anashinda. Mark my words.View attachment 1619213
Wanaendelea kuhesabu na mshindi anatakiwa kuwa na 270! 224( Biden) anahitaji 44, 213(Trump) anahitaji 57 ili ashinde
Ficha ujinga wako mkuu,watu 270!!!?Sio Marekani, sema ni wale watu 270 ndo wanateua raisi, majority vote wala hazihesabiki! Hakuna uchaguzi maigizo kama wa Marekani!
Kishashinda mark my words.Ni ndoto
Yaani wewe unajua kwa spidi kuliko hata wasimamizi wenyewe wa uchaguzi ambao wapo US!Kishashinda mark my words.
Pennsylvania,Michigan,Georgia,North Carolina..Kote huko Trump anakimbiza now...Tatizo Trump anakwenda kushinda majimbo yenye point nyingi. Trump anashinda. Mark my words.
Ni kwa sababu kule hakuna vyama vya upinzani vya kipumbavu kama huku kwenu. mwenyekiti analewa faru john unategemea nini?Huo uchaguzi hatujasikia watu wametekwa, kujeruhiwa wala kuuwawa wala kwamba zimepatikana kura feki.
Waafrika tulilaaniwa na tunajifanya kuigiza kufanya uchaguzi kimakosa kabisa wakati hatujui hata nini maana ya uchaguzi.
Marehemu Pieta Bother aliwahi kusema mwafrika hakuumbwa kutawala ila kutawaliwa tu. Today we're witnesses to what Bother said well over 40 years ago.
Nimepewa akili ya kung'amua logic.Yaani wewe unajua kwa spidi kuliko hata wasimamizi wenyewe wa uchaguzi ambao wapo US!
😂 😂
Trump analalamika wanataka kumuibia.Majimbo ya Wisconsin, Michigan na Pennsylvania itachukua hadi wiki moja kumaliza.
Hivyo hapa tutegemee ushindi wa taabu sana kwa mgombea yoyote kati ya Biden na Trump.
Hongera sana Dada yangu.Nimepewa akili ya kung'amua logic.
Namuelewa Sana huyu Mjuba...
Mtu mwenye historia ya Joe Biden kwa kiswahiliTrump, rais wa 45 wa Marekani anajivunia rikodi ya kuimarisha uchumi na kupunguza kwa kiwango kikubwa ukosefu wa ajira lakini anakosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia janga la virusi vya corona.
Biden, mwanasiasa anayegemea sera za wastani za mrengo wa shoto ameahidi kulinda haki ya wamarekani kupata huduma za afya, mafao kwa wazee na kutengeneza nafasi mpya za kazi kupitia sekta ya nishati jadidifu.
Mchuano ni mkali na wasiwasi umetanda juu ya kuzuka mabishano baada ya uchaguzi huu, baada ya Rais Trump kutishia kujitangazia ushindi hata kabla ya matokeo kukamilika.
=========================UPDATES====================
Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.
Mpaka sasa Joe Biden anaongoza kwa kura za wajumbe maalum 131 na Trump akiwa na idadi ya kura 98 za wajumbe maalum. Matokeo yanaendelea kutangazwa.
Wamarekani zaidi ya milioni Mia moja wamepiga kura ya kuamua iwapo watamrudisha madarakani Donald Trump au wataamua kuleta mabadiliko kwa kumchagua mgombea wa chama cha Demokratik Joe Biden, baada ya wanasiasa hao wawili kupambana vikali kwenye kampeni zao katika muktadha wa janga la maambukizi ya virusi vya corona.
Idadi hiyo inaashiria kwamba ushiriki wa wapiga kura utavunja rekodi ya karne. Washindani hao walikamilisha kampeni zao kwenye majimbo muhimu. Kura za maoni zinaonyesha kuwa Biden yuko mbele lakini kinyang'anyiro kinakwenda bega kwa bega katika majimbo yanayoweza kuamua mshindi.