DOKEZO Raia wa Rwanda wanapenyaje hadi kujazana nchini?

DOKEZO Raia wa Rwanda wanapenyaje hadi kujazana nchini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kigoma imekuwa chaka lao!
Sijajua Taifa langu eidha limeamua kuacha uhamiaji holela au mamlaka zimeshindwa kupambana na wimbi la wahamiaji MI

Warundi na Wanyaru ni wengi sana Kigoma, in fact wao ndio cheap Labor huko kigoma

Kwahiyo Rwanda iliyoendelea, inayotuma ma spy na kuhatarisha usalama wenu ndo wamekua cheap labor wenu? Info wanazopata kijasusi haziwasaidii 😂
 
Watanzania tuna wivu wa kipumbavu sana,mleta mada akiwa miongoni mwa haa wapumbavu ni ujinga na upumbavu kwa taifa kubwa kama taifa kulihofia taifa dogo kama Rwanda.

Hakuna watu waoga hii East Africa kama Watanzania.

Word.
 
Mkui acha ujinga basi, nchi zote duniani zina athirika na uhamiaji harama,sio nchi tajiri wala za uchumi wa kati.
Nchi kama USA,UK,Germany,Denmark,Norway,Sweden na nyingi za Ulaya zipo well off kiuchumi zaidi lakini zinaathurika na uhamiji vipi Tanzania nchi maskini.
Kuwa na wahamiaji wengi katika nchi ina disturb uchumi wa nchi na mbaya zaidi unasababisha matatizo ya kijamii.
Mfano nchi za Ulaya ongezeko la uhalifu linatokana na wahamiaji haramu.

Mtu kuongea Kinyarwanda hiyo tu inatosha kumfanya mtu kuwa mhamiaji haramu? Hayo ndo madai ya mleta uzi.

Mimi nikiongea Kiswahili London downtown, does that make me an illegal immigrant?

Umewahi kusikia malalamiko ya wabongo against wamalawi, wacongo, wazambia nk zaidi ya kelele against Rwanda na Kenya?
 
Nadhani serikali na Jeshi la Uhamiaji waingie kazini, kama kipindi cha Kikwete wengi waliogopa na kurudi kwao
Ushachelewa mpaka aje rais mwenye akili hio ila kwa kupitia Mapinduzi ya Chama hakuna rais atakaefanya hivyo
 
Topic zote zilizopo humu zinapinga uhamiaji Haram na sio ushindani wa ajira na ni ajira ipi hapa bongo mrwanda anaweza shindana na mtanganyika akashinda?

Kuhusu DP Haina uhusiano wowote na wahamiaji Haram wanyarwanda Ina uhusiano na kagame na kwakuwa najiamini ninaweza kumkubali kagame lakini nakapinga vikali wahamiaji Haram bila kujali ni mrwanda au mrundi sema inferiority complex ndo inakufanya uone sisi kukipinga uhamiaji Haram kama tunawaonea

Kama unajua hawawezi pewa kazi nchini nini kinakuuma? Kwanini uliamini maneno ya CDF ambayo hadi leo hayana proof?

Unajua mrwanda au mgeni yeyote akiwa naturalized ana haki zote kama raia wengine?

Wabongo walio wengi including wewe na mleta uzi mkisia warwanda au wakenya mnaloa tepe tepe bila sababu za msingi.
 
Hujajibu swali langu, Nimekuuliza hayo makabila ni raia wa nchi zipi kwa sababu hata historia huelewi unaposema Watusi "waliruhusiwa" kuingia Congo usijue kwamba kuna Watusi wamekuwepo Congo ya leo tangu karne 18 wakati ambapo hata hilo taifa la Congo lililotengenezwa na Wakoloni Wabelgiji halikuwepo.
Jussa kasha wahi sema "Watanganyika hawaijui historia"
 
Watusi wanamiliki ardhi ya kutisha hapo Kahama.Kuna kijiji kinaitwa Nuja walijimilikisha nusu ardhi ya kijiji na hakuna wa kuwafanya chochote.Shukrani kwa jeshi la Magereza kulitwaa lile eneo kwa mikong'oto na virungu vya ugoko.
Tabora nako maporini yamejificha majamaa na ng'ombe,ujambazi yamejimilikisha na uchumi na maelfu ya ardhi .Miswahili imekuwa manamba na mitumwa ya hawa pua ndefu kama filimbi.Tuamke.
Hii haina tofauti na Watanzania ambao ni manamba kwenye viwanda vya wahindi na waarabu
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Huyo mbulula alieanzisha uzi kaukimbia...
Mibongo asilimia 90 ni mipumbavu
Elimu mbovu, Mahospitali hakuna huduma, maji na umeme bado ni ndoto...
Wamebaki na ule ujinga wa enzi za nyerere, kuogopeshwa na wageni ni hatari kwa usalama wa taifa
Wakati hapo Kenya wanajielewa kuwa ukosefu wa huduma za jamii ndio kuhatarisha usalama wa taifa ndio maana wanajua kukiwasha......huku kwetu mizobwe ni ujingaujinga mwingi.....
 
Tuko Dodoma tunasosomola akina Doto Magari, Diamond, Zuchu nk.

Hayo mambo yenu magumumagumu hayatuhusu.
 
Zamani ilikuwa ni kawaida Kwa sisi watu wa wa mkoa wa Kagera kuishi na Wanyarwanda na wamesoma hapa Tanzania na Sasa wana kazi kubwa serikalini na likizo Huwa wanaenda kwao Rwanda kusherehekea na ndugu zao huku, na likizo zikiisha hurejea Tanzania katika ajira za serikali kabisa

Wanyarwanda wameingia kinyemera Kwa kuhonga kupata kitambulisho cha mpiga kura,
Wengine wamesoma hadi vyuo vikuu na mikopo wa elimu ya juu wamepata, yàani raia wa kigeni anasomeshwa na Kodi zetu na vijana wetu wanakosa mkopo.

Vyombo vya usalama kwanini hamfanyi operation za mara Kwa mara kubaini wahamiaji haramu.

Wanyarwanda sio wageni wazuri kuingia kwenye Taifa letu bila taratibu na vibali au kujulikana,

kila siku serikali za Congo, Burundi Uganda na Msumbiji zinawalalamikia sana kusababisha maafa, mauaji na kipenyeza vikundi vya waasi wanaokesesha raia amani

Nilishituka Kuna kipindi Niko zangu Tandahimba huko Niko bar napata safari lager, nikasikia mabinti wahudumu wanazungumza Kinyarwanda, wao walidhani sijui kumbe me natokea Ngara ni jirani Yao.
Hii ilinishtua yaani mtu kavuka Rwanda mpaka na kutembea zaidi ya km 2000 na hajakamatwa

Hii ni hatari Kwa usalama wa Taifa letu, watu kuingia nchini bila kutambuliwa na vibali maalumu au passport

Wanyarwanda wamejaa hapa nchini, hadi wanapenya na kupata nafasai nyeti serikalini

Nadhani serikali na Jeshi la Uhamiaji waingie kazini, kama kipindi cha Kikwete wengi waliogopa na kurudi kwao
Afrika ni nchi moja. Hata hivyo, tuna waafrika wabaya kama vile Wanigeria na matapeli wengine wnaaaotaka riziki bila kufanya kazi halali. Ukienda Mara wamejaa Wajaluo, wakisii na wengine toka Kenya. Ukienda Kigoma ndo usiseme. Wamejaa wakongomani wengi tu wanaojiita wamanyema ambao nao wakiwa Kigoma wanajiita wazaramo. Kimsingi, Tanzania hakuna utaratibu wa maana wa uraia zaidi ya kuwa na roho mbaya kwa watanzania wanaotwaa uraia wa kigeni hasa kwenye nchi za ulaya. Kuna wanyasa wengi toka Malawi wanaofanya kazi Masaki na kwingineko kwa wenye nazo. Mie, naona tuunganishe Afrika Mashariki na kuwa na nchi moja ili kuondoa ujinga huu.
 
Watu weusi ndio namba moja kwa ubaguzi so hiyo mikopo waliyopewa kusoma chuo ndio ilikuzuia wewe kupata PhD yako ama?
 
Wabongo wengi hawawapendi sana raia wageni wa Kenya na Rwanda, nafikiri kuna hali fulani ya wivu mbaya dhidi ya hizi nchi. Kila wakati utakapozungumziwa uhamiaji haramu reference kubwa zaidi ni Wanyarwanda na Wakenya.
Kabisa mkuu sasa sijui ni chuki au uelewa hawa wanyarwanda washakuwa wakimbizi sasa kuwepo mpaka leo kuna ajabu gani, kuna watanzania kibao Kenya wa halali na wasio halali.
 
Wana uzi wao humu JF niliingia nikawauliza wanaongea lugha gani? Nikashangaa nimechezea ban. Hii ilinifanya nitafakari sana juu usalama wa taifa na raia wake.
 
Back
Top Bottom