Raia wa Zanzibar wapigwe marufuku kupiga kura ya kumchagua Rais wa Tanganyika

Mleta mada siyo mjinga, ana uelewa kuwa Tanganyika imemezwa na Tanzania . Nia na lengo la mtoa mada ni kwanini Tanganyika haipewi haki ya kuchagua rais wao Kama Zanzibar ilivyo na haki ya kuchagua rais wao.
Ukirejea tume ya jaji marehemu Kisanga na tume ya rasimu ya katiba zote zilizungumzia kuhusu uwepo wa serikali tatu, tume ya Warioba ulienda mbali zaidi na kusema ni heri watanganyika wakapewa serikali yao kabla ya kuidai serikali yao.
Hayo maoni ni mwanzo mwishowe itafika wakati wataidai kwa nguvu hapo ndio utabiri wa tume ya Warioba utatumia.
 
Kwahiyo Uncle unataka kusema Zanzibar kimataifa inatambulika kama ilivyo mkoa tu wa Morogoro?

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
Yes, na sio kimataifa tuu, hata katiba ya JMT, rais wa Zanzibar ni almost nothing and nobody kwenye set up ya JMT, ili kumlindia hadhi, rais wa Zanzibar ni waziri asiye na wizara maalum ili aingie kwenye cabinet, baada ya Komandoo Dr. Salmin Amour kupitisha marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 kwa Zanzibar kujiita nchi, aligoma kuapishwa na kususia vikao vya cabinet yetu, na baada tuu ya kumaliza urais wa Zanzibar, he was grounded!, kama Jumbe!.
Kimataifa Zanzibar ni sawa tuu na mkoa!.
P
 
Naendelea kusisitiza mtu ukiwa hujui kitu ni mjinga!, kuwa mjinga sio kosa, dawa yake ni kuelimishwa. Vatican ni nchi, a City State yenye sovereignty. Zanzibar haina sovereignty hivyo sio nchi!.
P
Natamani siku moja JF waandae mdahalo kupitia zoom meeting mi nitalipia sina tatizo haswa usiku kuanzia saa 1 tupambane kwa hoja mkuu, nakutamani sn tufanye live.
 
Kwanza huu ni muungano wa hovyo ambao Zanzibar pekee ina nufaika wakati sisi watanganyika tunateseka.
 
Natamani siku moja JF waandae mdahalo kupitia zoom meeting mi nitalipia sina tatizo haswa usiku kuanzia saa 1 tupambane kwa hoja mkuu, nakutamani sn tufanye live.
Wewe tuu!, kwani if ni nani?, ni mimi na wewe, na yule na yeye, it's user generated content, ukitaka chochote, unaanzisha. Pendekeza tuu, mimi niko available all the time!.
P
 
Zanziba sio nchi,zanziba ni kama Palestine ni mamlaka ndani ya nchi mfano nijibu,Nani waziri wa Mambo ya nje wa zanziba? Je zanziba ana uwakilishi namba ngapi huko UN?
 
Nakuunga mkono mkuu.
Zanzibar ni state yenye sovereignty.
Hizo nyingine ni danganya toto.
 
Kabisa!
 
Ni mjinga tu ndo atabishia kuwa zanzibar sio nchi
 
Umemjibu kitaalam kabisa mkuu.

Angalia hata kwenye ubinafsishaji wa bandari!

Waziri aliyezibinafsisha za Tanganyika alithubutu kuzisogelea za Zanzibar?

Kuna Mtanganyika mwenye sauti juu ya bandari za Zanzibar?
 
katika huu Muungano ilitakiwa Tanganyika iwe na katiba na utawala wake hali kadhalika nayo Zanzibar.

Rais awe ni mmoja tu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ila Tanganyika na Zanzibar zinaweza kuwa na viongozi wao wakuu lkn si ma Rais.
 
Wakijibu unitag
 
Ni mtu MPUMBAVU,ZEZETA,TAHIRA,ZWAZWA &
MJINGA ambaye anasema Zanzibar siyo nchi,huwezi kusema Zanzibar siyo nchi kisa inakosa kitu inaitwa "SOVEREIGNTY".

Haya yanayoendelea kwasasa na tunayashuhudia kwa macho yetu kwenye huu muungano Uchwara unaweza simama kabisa na tumbo lako na kusema Zanzibar siyo nchi?

Hakuna mtanganyika mwenye akili timamu anaye ushadadia huu muungano Uchwara!,Ukiona mtu anasema Tanganyika ndiyo Tanzania basi atakuwa na tatizo la upungufu wa kiakili!.
 
Ni mjinga tu ndo atabishia kuwa zanzibar sio nchi
Naomba kuheshimu maoni yako, ujinga ni kutokujua, hivyo mtu yoyote anayedhani Zanzibar ni nchi, ni mjinga kwa kutokujua kuwa Zanzibar sio nchi kwasababu haina sovereignty na haina dola!. Wale majeshi yake ya KMKM, JKU na vikosi vya SMZ, sio majeshi!, wale ni migambo tuu!. Zanzibar haina polisi, haina jeshi, haina sarafu, haina sovereignty!. Sio nchi!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…