Kb Ulayaulaya
JF-Expert Member
- Jan 5, 2023
- 727
- 1,059
Mkuu mbona inakuwa mkali!.mleta MADA anahitaji umtajie faida ya muungano.Bandiko hili ni kielelezo cha uhitaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa Watanzania wenzetu!. Watu wenye ufahamu na hili watamuona mleta mada kama ni lijinga fulani, kumbe huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania wenzetu, ni wajinga tuu kwa kutoelewa. Dawa ya mjinga ni kumuelimisha.
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina rais mmoja, rais wa JMT ambaye anachaguliwa na Watanzania wote.
2. Tanzania ina uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo Watanzania wote wana haki sawa ndani ya JMT, ikiwemo haki ya kupiga kura, na haki ya kugombea.
3. Tanzania ilitokana na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
4. Tanzania bara haina utawala wake wa ndani, hivyo rais wa JMT ndie rais wa nchi anayechaguliwa na wote, lakini Zanzibar inao utawala wake wa ndani, seclusion, na rais wake, rais wa Zanzibar ambapo ni Wanzanzibari wakaazi pekee ndio wenye haki ya kuchamchagua rais wa Zanzibar.
5. Baada ya muungano wetu adhimu, Tanganyika ilikufa na kugeuka Tanzania, ila Zanzibar iliendelea kubaki sio kama nchi bali ilibaki kama sehemu ya JMT inayojitegemea.
Hivyo Wanzanzibari wote ni Watanzania na wana haki zote za kumchagua rais wa JMT ila wenye haki ya kumchagua rais wa Zanzibar ni Wazanzibari pekee!.
P
Maswala ya kuungana anajua historia yake.Faida yake nn.
Zanzibar Bado ni Nchi yenye Serikali mfumo mzima wa kiongozi wanao.Why Serikali ya Tanganyika ife,irihali JMT ni muungano wa Nchi mbili?.
Nchi ya Kwanza ni Zanzibar,na Nchi ya Pili ni ipi Kwa Sasa?.
Mzanzibari ana haki bara,ila wa bara hana haki Zanzibar,mbona nnajizima DATA wakubwa,mnakuwa na kigugumizi Cha Nini hasa.
Au Zanzibar kivingine no Koloni letu ama!.
Hapo ntaitwa mchochezi,ila kiukweli Mtanganyika Yuko wapi maana Mzanzibari yupo.Watanzania pia wapo.
Tupeni faida Kwanza,afu elimu ya uraia Kwa sisi wajinga itafata.