Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Zanzibar haina dola, yale sio majeshi ni mitambo!.Kwa kuongezea tu, Zanzibar ina Rais wake, Jeshi lake, mkuu wa majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake.
Migambo kibao wana silaha!. Makampuni kibao, ya ulinzi wana silaha!.Kwa kawaida migambo TANZANIA wanamiliki virungu.
Pia migambo TANZANIA wana jezi zao.
Hao migambo wa Zanzibar wapo hivyo?
Kuna mfanano wowote kuanzia mavazi hadi siraha kati ya mgambo wa huku bara na hao wazanzibari?
Mkuu Mayalla! Mbona wewe ni mwanasheria? Unashindwaje kuelewa mambo yaliyo wazi hivyo?Zanzibar haina dola, yale sio majeshi ni mitambo!.
Amri Jeshi Mkuu ni mmoja tuu!, rais wa JMT!.
P
Bandiko hili ni kielelezo cha uhitaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa Watanzania wenzetu!. Watu wenye ufahamu na hili watamuona mleta mada kama ni lijinga fulani, kumbe huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania wenzetu, ni wajinga tuu kwa kutoelewa. Dawa ya mjinga ni kumuelimisha.
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina rais mmoja, rais wa JMT ambaye anachaguliwa na Watanzania wote.
2. Tanzania ina uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo Watanzania wote wana haki sawa ndani ya JMT, ikiwemo haki ya kupiga kura, na haki ya kugombea.
3. Tanzania ilitokana na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
4. Tanzania bara haina utawala wake wa ndani, hivyo rais wa JMT ndie rais wa nchi anayechaguliwa na wote, lakini Zanzibar inao utawala wake wa ndani, seclusion, na rais wake, rais wa Zanzibar ambapo ni Wanzanzibari wakaazi pekee ndio wenye haki ya kuchamchagua rais wa Zanzibar.
5. Baada ya muungano wetu adhimu, Tanganyika ilikufa na kugeuka Tanzania, ila Zanzibar iliendelea kubaki sio kama nchi bali ilibaki kama sehemu ya JMT inayojitegemea.
Hivyo Wanzanzibari wote ni Watanzania na wana haki zote za kumchagua rais wa JMT ila wenye haki ya kumchagua rais wa Zanzibar ni Wazanzibari pekee!.
P
Ili hyo marufuku iwepo bas lazma uwepo wa tanganyika kwa mana serikali ya tanganyika na sio Tanzania.Nawapongeza Zanzibar kwa kuwa na msimamo, huwezi kupiga kura ya kumchagua rais wa Zanzibar ikiwa wewe si mzanzibari.
Cha ajabu serikali ya Tanganyika inaingiliwa na Zanzibar, yaani raia wa nchi jirani (Zanzibar) wanapiga kura kuchagua Rais wa Tanganyika.
Jambo hilo lingekuwa na mantiki endapo nasisi Watanganyika tungeruhusiwa kushiriki kuwachagulia Rais watu wa Zanzibar. Kwakuwa hatuwaingilii kwenye uchaguzi wao, na wao wazuiliwe maramoja kutuchagulia Rais.
Kuna tofauti gani na wale wanaotaka serekali za majimbo? Maana siku zote ccm mkisikia sera za serekali za majimbo mnataka kuwehuka, wakati hilo la Zanzibar tayari ni Jimbo?Mtu ukiwa hujui kitu fulani, ni mjinga!, mtu kuwa mjinga sio kosa, kwasababu kutokujua kitu fulani sio kosa, ukiisha julishwa, ujinga unakutoka unakuwa mwerevu.
Ili nchi kuwa taifa, sio eneo, sio rais, sio bendera, sio wimbo wa taifa, nchi kuwa taifa ni kitu kinachoitwa sovereignty, dola!, Zanzibar haina sovereignty, sio dola!. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndio yenye sovereignty, yenye dola, yenye vyombo vya dola, yenye sarafu, Zanzibar ni jina tuu, la nchi lakini sio nchi, na rais wa Zanzibar ni rais jina tuu wa sehemu inayoitwa Zanzibar lakini kimataifa sio rais, rais ni mmoja tuu, rais wa JMT na nchi ni moja tuu, JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT!.
P
Zanzibar haina jeshi, bali ina jeshi usu, ambao ni migambo tuu!, sio jeshi.Hili siyo Jeshi?
Labda uniambie unawasilisha ujumbe wako kwa "code", vinginevyo utaonekana kituko kusema Zanzibar haina Jeshi wakati iko wazi kabisa kuwa Zanzibar ina Jeshi lake na mkuu wake wa majeshi na Amiri Jeshi Mkuu.
Jifunze tofauti ya jeshi na jeshi usu!. Zanzibar haina polisi, haina jeshi!. KMKM, JKU na Vikosi vya SMZ wote ni jeshi usu.Mkuu Mayalla! Mbona wewe ni mwanasheria? Unashindwaje kuelewa mambo yaliyo wazi hivyo?
Wanchagua raisi wa Tanzania sio wa Tanganyika.Cha ajabu serikali ya Tanganyika inaingiliwa na Zanzibar, yaani raia wa nchi jirani (Zanzibar) wanapiga kura kuchagua Rais wa Tanganyika
Cheo cha Meja kinakopatikana wapi?Zanzibar haina jeshi, bali ina jeshi usu, ambao ni migambo tuu!, sio jeshi.
P
Naendelea kusisitiza mtu ukiwa hujui kitu ni mjinga!, kuwa mjinga sio kosa, dawa yake ni kuelimishwa. Vatican ni nchi, a City State yenye sovereignty. Zanzibar haina sovereignty hivyo sio nchi!.
P
Nini utofauti wa Jeshi na hao unaowaita mgambo?Jifunze tofauti ya jeshi na jeshi usu!. Zanzibar haina polisi, haina jeshi!. KMKM, JKU na Vikosi vya SMZ wote ni jeshi usu.
P
Hoja imeungwa mkono.Hilo litawekana kama tutakuwa na rais wa tanganyika na wa muungano. Au tubadili muundo, zanzibar na bara @ waongozwe na waziri mkuu na rais abaki wa muungano.
Sasa ni confusion
Safi sana mtaalam. Umeeleza hali ilivyo! Je unasemaje kuhusu haki za watanganyika ndani ya Tanzania!kwenye nchi sehemu ya Tanganyika na sehemu ya zanzibar? baada ya Tanganyika" kufa"?Bandiko hili ni kielelezo cha uhitaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa Watanzania wenzetu!. Watu wenye ufahamu na hili watamuona mleta mada kama ni lijinga fulani, kumbe huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania wenzetu, ni wajinga tuu kwa kutoelewa. Dawa ya mjinga ni kumuelimisha.
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina rais mmoja, rais wa JMT ambaye anachaguliwa na Watanzania wote.
2. Tanzania ina uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo Watanzania wote wana haki sawa ndani ya JMT, ikiwemo haki ya kupiga kura, na haki ya kugombea.
3. Tanzania ilitokana na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
4. Tanzania bara haina utawala wake wa ndani, hivyo rais wa JMT ndie rais wa nchi anayechaguliwa na wote, lakini Zanzibar inao utawala wake wa ndani, seclusion, na rais wake, rais wa Zanzibar ambapo ni Wanzanzibari wakaazi pekee ndio wenye haki ya kuchamchagua rais wa Zanzibar.
5. Baada ya muungano wetu adhimu, Tanganyika ilikufa na kugeuka Tanzania, ila Zanzibar iliendelea kubaki sio kama nchi bali ilibaki kama sehemu ya JMT inayojitegemea.
Hivyo Wanzanzibari wote ni Watanzania na wana haki zote za kumchagua rais wa JMT ila wenye haki ya kumchagua rais wa Zanzibar ni Wazanzibari pekee!.
P
Zanzibar ina Katiba yake!Acha kuchekesha mkuu!
Zanzibar siyo nchi wakati ina raia wake, Bunge lake na mawaziri wake?
Zanzibar siyo nchi wakati ina wimbo wake wa Taifa?
Zanzibar siyo nchi wakati ina bendera yake?
Zanzibar siyo nchi wakati hata plate namba za magari ya huko ni tofauti na ya magari ya Tanganyika?
Zanzibar siyo nchi Mtanganyika hawezi kuvusha mzigo bila kutozwa Kodi "mpakani"?
Zanzibar siyo nchi wakati Mtanganyika hawezi kuendesha gari huko bila kibali maalum?
Zanzibar siyo nchi wakati Sheria zozote zitakazotungwa Tanganyika hazina mamlaka Zanzibar mpaka zitakaporidhiwa na Bunge la Zanzibar?
Zanzibar siyo nchi? How?
Wewe unaijua Zanzibar kuwazidi Wazanzibar ambao kote waendako wamekuwa wakijitambilisha kuwa nchi yao ni Zanzibar?
Na ina nguvu kuliko ile inayoitwa ya JMT. Ndiyo maana ili ya JMT itumike Zanzibar, sharti lipate kibali cha Bunge la Zanzibar.Zanzibar ina Katiba yake!