Raia wa Zanzibar wapigwe marufuku kupiga kura ya kumchagua Rais wa Tanganyika

Raia wa Zanzibar wapigwe marufuku kupiga kura ya kumchagua Rais wa Tanganyika

Kwa kawaida migambo TANZANIA wanamiliki virungu.
Pia migambo TANZANIA wana jezi zao.
Hao migambo wa Zanzibar wapo hivyo?
Kuna mfanano wowote kuanzia mavazi hadi siraha kati ya mgambo wa huku bara na hao wazanzibari?
Migambo kibao wana silaha!. Makampuni kibao, ya ulinzi wana silaha!.
P
 
Hilo litawekana kama tutakuwa na rais wa tanganyika na wa muungano. Au tubadili muundo, zanzibar na bara @ waongozwe na waziri mkuu na rais abaki wa muungano.

Sasa ni confusion
 
Bandiko hili ni kielelezo cha uhitaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa Watanzania wenzetu!. Watu wenye ufahamu na hili watamuona mleta mada kama ni lijinga fulani, kumbe huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania wenzetu, ni wajinga tuu kwa kutoelewa. Dawa ya mjinga ni kumuelimisha.
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina rais mmoja, rais wa JMT ambaye anachaguliwa na Watanzania wote.
2. Tanzania ina uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo Watanzania wote wana haki sawa ndani ya JMT, ikiwemo haki ya kupiga kura, na haki ya kugombea.
3. Tanzania ilitokana na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
4. Tanzania bara haina utawala wake wa ndani, hivyo rais wa JMT ndie rais wa nchi anayechaguliwa na wote, lakini Zanzibar inao utawala wake wa ndani, seclusion, na rais wake, rais wa Zanzibar ambapo ni Wanzanzibari wakaazi pekee ndio wenye haki ya kuchamchagua rais wa Zanzibar.
5. Baada ya muungano wetu adhimu, Tanganyika ilikufa na kugeuka Tanzania, ila Zanzibar iliendelea kubaki sio kama nchi bali ilibaki kama sehemu ya JMT inayojitegemea.

Hivyo Wanzanzibari wote ni Watanzania na wana haki zote za kumchagua rais wa JMT ila wenye haki ya kumchagua rais wa Zanzibar ni Wazanzibari pekee!.

P

Mkanganyiko wa namba 2 na 4 ndio unatufanya tulio na akili za nje ya ccm kuona hakuna muungano, bali uhuni wa wazi wa Nyerere.
 
Nawapongeza Zanzibar kwa kuwa na msimamo, huwezi kupiga kura ya kumchagua rais wa Zanzibar ikiwa wewe si mzanzibari.

Cha ajabu serikali ya Tanganyika inaingiliwa na Zanzibar, yaani raia wa nchi jirani (Zanzibar) wanapiga kura kuchagua Rais wa Tanganyika.

Jambo hilo lingekuwa na mantiki endapo nasisi Watanganyika tungeruhusiwa kushiriki kuwachagulia Rais watu wa Zanzibar. Kwakuwa hatuwaingilii kwenye uchaguzi wao, na wao wazuiliwe maramoja kutuchagulia Rais.
Ili hyo marufuku iwepo bas lazma uwepo wa tanganyika kwa mana serikali ya tanganyika na sio Tanzania.
 
Mtu ukiwa hujui kitu fulani, ni mjinga!, mtu kuwa mjinga sio kosa, kwasababu kutokujua kitu fulani sio kosa, ukiisha julishwa, ujinga unakutoka unakuwa mwerevu.

Ili nchi kuwa taifa, sio eneo, sio rais, sio bendera, sio wimbo wa taifa, nchi kuwa taifa ni kitu kinachoitwa sovereignty, dola!, Zanzibar haina sovereignty, sio dola!. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndio yenye sovereignty, yenye dola, yenye vyombo vya dola, yenye sarafu, Zanzibar ni jina tuu, la nchi lakini sio nchi, na rais wa Zanzibar ni rais jina tuu wa sehemu inayoitwa Zanzibar lakini kimataifa sio rais, rais ni mmoja tuu, rais wa JMT na nchi ni moja tuu, JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT!.
P
Kuna tofauti gani na wale wanaotaka serekali za majimbo? Maana siku zote ccm mkisikia sera za serekali za majimbo mnataka kuwehuka, wakati hilo la Zanzibar tayari ni Jimbo?
 
Na wazuiwe kumiliki ardhi Bara wakae huko huko hadi wakose nafasi walale wamesimama
 
Naendelea kusisitiza mtu ukiwa hujui kitu ni mjinga!, kuwa mjinga sio kosa, dawa yake ni kuelimishwa. Vatican ni nchi, a City State yenye sovereignty. Zanzibar haina sovereignty hivyo sio nchi!.
P

Tufanye uko sahihi kwa maelezo yako, lakini kiuhalisia hapo hakuna muungano wa watu wenye akili, bali wanaokubaliana na huo muungano kama mazombie.
 
Lengo la mwalimu 7likuwa zanzibar itambulike kama mkoa mmojawapo wa Tanzania lakini mchakato ukawa na upinzani wa chini kwa chini kwa wazanzibar kukataa nchi kuwa mkoa au jimbo

Lengo jingine ilikuwa ni kuimiliki sehemu kubwa ya bahari ya hindi iwe mali ya bara pia(hapa hadi sasa faida ipo nzuri tu)
 
Hilo litawekana kama tutakuwa na rais wa tanganyika na wa muungano. Au tubadili muundo, zanzibar na bara @ waongozwe na waziri mkuu na rais abaki wa muungano.

Sasa ni confusion
Hoja imeungwa mkono.
 
Bandiko hili ni kielelezo cha uhitaji mkubwa wa elimu ya uraia kwa Watanzania wenzetu!. Watu wenye ufahamu na hili watamuona mleta mada kama ni lijinga fulani, kumbe huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania wenzetu, ni wajinga tuu kwa kutoelewa. Dawa ya mjinga ni kumuelimisha.
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT, ina rais mmoja, rais wa JMT ambaye anachaguliwa na Watanzania wote.
2. Tanzania ina uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo Watanzania wote wana haki sawa ndani ya JMT, ikiwemo haki ya kupiga kura, na haki ya kugombea.
3. Tanzania ilitokana na muungano wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, na kuwa nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.
4. Tanzania bara haina utawala wake wa ndani, hivyo rais wa JMT ndie rais wa nchi anayechaguliwa na wote, lakini Zanzibar inao utawala wake wa ndani, seclusion, na rais wake, rais wa Zanzibar ambapo ni Wanzanzibari wakaazi pekee ndio wenye haki ya kuchamchagua rais wa Zanzibar.
5. Baada ya muungano wetu adhimu, Tanganyika ilikufa na kugeuka Tanzania, ila Zanzibar iliendelea kubaki sio kama nchi bali ilibaki kama sehemu ya JMT inayojitegemea.

Hivyo Wanzanzibari wote ni Watanzania na wana haki zote za kumchagua rais wa JMT ila wenye haki ya kumchagua rais wa Zanzibar ni Wazanzibari pekee!.

P
Safi sana mtaalam. Umeeleza hali ilivyo! Je unasemaje kuhusu haki za watanganyika ndani ya Tanzania!kwenye nchi sehemu ya Tanganyika na sehemu ya zanzibar? baada ya Tanganyika" kufa"?
 
Acha kuchekesha mkuu!

Zanzibar siyo nchi wakati ina raia wake, Bunge lake na mawaziri wake?

Zanzibar siyo nchi wakati ina wimbo wake wa Taifa?

Zanzibar siyo nchi wakati ina bendera yake?

Zanzibar siyo nchi wakati hata plate namba za magari ya huko ni tofauti na ya magari ya Tanganyika?

Zanzibar siyo nchi Mtanganyika hawezi kuvusha mzigo bila kutozwa Kodi "mpakani"?

Zanzibar siyo nchi wakati Mtanganyika hawezi kuendesha gari huko bila kibali maalum?

Zanzibar siyo nchi wakati Sheria zozote zitakazotungwa Tanganyika hazina mamlaka Zanzibar mpaka zitakaporidhiwa na Bunge la Zanzibar?

Zanzibar siyo nchi? How?

Wewe unaijua Zanzibar kuwazidi Wazanzibar ambao kote waendako wamekuwa wakijitambilisha kuwa nchi yao ni Zanzibar?
Zanzibar ina Katiba yake!
 
Back
Top Bottom