Kenya 2022 Raila Odinga akataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa Rais
Kenya 2022 General Election

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais nchini Kenya na kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anatarajiwa kuzungumza na Wakenya kupitia vyombo vya habari leo Jumanne, Agosti 16, 2022.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Dennis Onsarigo ambaye amekuwa msimamizi wa mawasiliano katika kampeni Raila Odinga, imeeleza kuwa hotuba hiyo inatarajiwa kufanyika majira ya saa nane mchana wa leo.

Onsarigo.PNG


UPDATES

RAILA ODINGA, KIONGOZI WA MUUNGANO WA AZIMIO LA UMOJA



Jana Agosti 15, demokrasia yetu ilikumbwa na msukosuko mkubwa.

Kutokana na hali hiyo, Kenya inakabiliwa na mzozo wa kisiasa kutokana na vitendo vya Wafula Chebukati

Sheria ya IEBC inaeleza kuwa isipokuwa uamuzi wa pamoja utaafikiwa, uamuzi kuhusu jambo lolote lililo mbele ya tume, utakuwa na wingi wa wajumbe waliohudhuria na kupiga kura

Takwimu zilizotangazwa na Bw. Chebukati ni batili na lazima zifutiliwe mbali na mahakama ya sheria

Kwa maoni yetu hakuna mshindi aliyetangazwa kihalali wala Rais mteule

Mimi na Azimio la Umoja na taifa kwa ujumla tulishangaa jana kujua kwamba Chebukati pekee ndiye aliamua kujitangaza kuwa ndiye aliyedaiwa kuwa Shujaa wa uchaguzi wa urais wa 2022

Tunakataa kabisa na bila kusita matokeo ya urais yaliyotangazwa jana

Tunafuata njia na michakato ya kikatiba na halali ili kubatilisha tamko haramu la Chebukati na lililo kinyume na katiba

Tunaelewa kuwa ni Chebukati pekee ndiye aliyeweza kujumlisha kura za urais

Aliwazuia makamishna wote kupata taarifa za kura
 
Itakuwa Vyema Akikubali Matokeo Mambo Mengine Yaendelee.
 
Asante kwa taarifa,ngoja tusikie atasemaje maana ndiye aliyeshika mustakabali wa amani ya Kenya
 
Aliyekuwa mgombea Urais wa Kenya, Raila Odinga atalihutubia Taifa leo saa 8 mchana.

Hatua hiyo inakuja kukiwa na mpasuko ndani ya tume ya uchaguzi baada ya maafisa wanne kukana kuyatambua matokeo yaliyompa ushindi William Ruto. https://t.co/T3pWW6R7Zd

20220816_135304.jpg
 
Anapoteza muda bureee!

Anatakiwa ampongeze Ruto kwa kushinda kiti cha Urais.

Asiye kubali kushindwa sio mshindani, wakenya tayari wamesha amua na dunia imesha zisikia sauti za wakenya wengi kuwa kipenzi chao ni Ruto.
 
Sisi kama wapwani tumempigia kura huyu mzee miaka nenda miaka rudi. Siku ya leo itabidi awe statesman na akubali matokeo. Kenya ni kubwa kumliko mtu mmoja.

Shukran baba, twakupenda, lakini kwa heshima na taadhima. Safiri salama na asante kwa kila kitu.
 
Huyu mzee anahangaika sana, angefuata nyayo za baba yake tu ambaye naye alitoka kapa kwenye urais.......ni swala la kukubaliana na hali ya mambo.
 
Huyu mwamba alikimbia presidential debate na Ruto Leo hii kashapigwa mitama anakimbilia Press Conference. Nani atamsikiliza? Dr Ruto ni Rais Mteule na tayari ameshapongezwa na Dunia nzima tayari anapata security briefings daily. Yeye anapata umbea toka kwa chawa wake daily.
 
Huyu mwamba alikimbia presidential debate na Ruto Leo hii kashapigwa mitama anakimbilia Press Conference. Nani atamsikiliza? Dr Ruto ni Risa Mteule tayari anapata security briefings daily. Yeye anapata umbra toka kwa chawa wake daily.
Babu Hana hamu na hustler
 
anapoteza muda bureee!
anatakiwa ampongeze Ruto kwa kushinda kiti cha Urais.

Asiye kubali kushindwa sio mshindani, wakenya tayari wamesha amua na dunia imesha zisikia sauti za wakenya wengi kuwa kipenzi chao ni Ruto.
Halazimiki kumpongeza Mheshimiwa.
 
Sisi kama wapwani tumempigia kura huyu mzee miaka nenda miaka rudi. Siku ya leo itabidi awe statesman na akubali matokeo. Kenya ni kubwa kumliko mtu mmoja.

Shukran baba, twakupenda, lakini kwa heshima na taadhima. Safiri salama na asante kwa kila kitu.
Mzee anapambana mpaka mwisho
 
Huyu mzee anahangaika sana, angefuata nyayo za baba yake tu ambaye naye alitoka kapa kwenye urais.......ni swala la kukubaliana na hali ya mambo.
Na huu mfano pia hapa kwetu tunapaswa kuuiga,maana haijawahi tokea upinzani ukakubali matokeo ya Urais.
 
Back
Top Bottom