Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais nchini Kenya na kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anatarajiwa kuzungumza na Wakenya kupitia vyombo vya habari leo Jumanne, Agosti 16, 2022.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Dennis Onsarigo ambaye amekuwa msimamizi wa mawasiliano katika kampeni Raila Odinga, imeeleza kuwa hotuba hiyo inatarajiwa kufanyika majira ya saa nane mchana wa leo.
UPDATES
RAILA ODINGA, KIONGOZI WA MUUNGANO WA AZIMIO LA UMOJA
Your browser is not able to display this video.
Jana Agosti 15, demokrasia yetu ilikumbwa na msukosuko mkubwa.
Kutokana na hali hiyo, Kenya inakabiliwa na mzozo wa kisiasa kutokana na vitendo vya Wafula Chebukati
Sheria ya IEBC inaeleza kuwa isipokuwa uamuzi wa pamoja utaafikiwa, uamuzi kuhusu jambo lolote lililo mbele ya tume, utakuwa na wingi wa wajumbe waliohudhuria na kupiga kura
Takwimu zilizotangazwa na Bw. Chebukati ni batili na lazima zifutiliwe mbali na mahakama ya sheria
Kwa maoni yetu hakuna mshindi aliyetangazwa kihalali wala Rais mteule
Mimi na Azimio la Umoja na taifa kwa ujumla tulishangaa jana kujua kwamba Chebukati pekee ndiye aliamua kujitangaza kuwa ndiye aliyedaiwa kuwa Shujaa wa uchaguzi wa urais wa 2022
Tunakataa kabisa na bila kusita matokeo ya urais yaliyotangazwa jana
Tunafuata njia na michakato ya kikatiba na halali ili kubatilisha tamko haramu la Chebukati na lililo kinyume na katiba
Tunaelewa kuwa ni Chebukati pekee ndiye aliyeweza kujumlisha kura za urais
Aliyekuwa mgombea Urais wa Kenya, Raila Odinga atalihutubia Taifa leo saa 8 mchana.
Hatua hiyo inakuja kukiwa na mpasuko ndani ya tume ya uchaguzi baada ya maafisa wanne kukana kuyatambua matokeo yaliyompa ushindi William Ruto. https://t.co/T3pWW6R7Zd
Sisi kama wapwani tumempigia kura huyu mzee miaka nenda miaka rudi. Siku ya leo itabidi awe statesman na akubali matokeo. Kenya ni kubwa kumliko mtu mmoja.
Shukran baba, twakupenda, lakini kwa heshima na taadhima. Safiri salama na asante kwa kila kitu.
Huyu mwamba alikimbia presidential debate na Ruto Leo hii kashapigwa mitama anakimbilia Press Conference. Nani atamsikiliza? Dr Ruto ni Rais Mteule na tayari ameshapongezwa na Dunia nzima tayari anapata security briefings daily. Yeye anapata umbea toka kwa chawa wake daily.
Huyu mwamba alikimbia presidential debate na Ruto Leo hii kashapigwa mitama anakimbilia Press Conference. Nani atamsikiliza? Dr Ruto ni Risa Mteule tayari anapata security briefings daily. Yeye anapata umbra toka kwa chawa wake daily.
Sisi kama wapwani tumempigia kura huyu mzee miaka nenda miaka rudi. Siku ya leo itabidi awe statesman na akubali matokeo. Kenya ni kubwa kumliko mtu mmoja.
Shukran baba, twakupenda, lakini kwa heshima na taadhima. Safiri salama na asante kwa kila kitu.