Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi hizi kauli not yet uhuru, au kama ndugu zetu wa chadema wanavyosema wanataka kuikomboa nchi, huwa naona wanadownplay jitihada za wazee walipigania uhuru. Nadhani bora watafute lugha nyingine ya kuhamasisha watu...
Ana haki ya kuhoji matokeo. Tatizo la Waafrika, ukimchukia mtu, unachukia na hoja zake hata kama ni za maana. Kwa mfano, Raila anasema kuna vituo ambavyo kura zimekuwa nyingi kuliko watu waliojiandikisha! Tena basi, si kituo kimoja! NI zaidi ya vituo 10. Mawakala wake walitolewa nje. Kura zilijumlishwa na kutangazwa matokeo wakiwa hawakushirikishwa. Je, kukubali upuuzi wa aina hiyo ndiyo kuimarika kwa demokrasia? Ushindi wa hila si ushindi.
Hii ndiyo laana ya Afrika. Hatuheshim matakwa ya raia wala misingi ya utawala tunaojiwekea. Ilikuwaje System mpya, iliyogharim mabillion, ikafa ghafla? Kibaki ndiye mwenye vyombo vya dola,mtu aliye na uchu madaraka wa kupindukia , aliyeapishwa usiku, hawezi kushindwa kutumia machinery kuchakachua matokeo.
Wazungu ndio maana wanatudharau sana. Siku zote wanatuchukulia kama watu wenye taahila ya akili na mtindio wa ubongo. Afrika pamoja na kuwa na watu zaidi ya milioni 600 lakini haina nguvu UN, haina VETO UN wala haiaminiki. ipo ipo tu na biashara hii ya kuchakachua matokeo, kukuza umasikini na kutukuza upumbavu. hakuna maendeleo ya teknolojia, elimu inazidi kushuka chini. Kwasababu ya watu wake kukata tamaa wana-resort kwenye ngono. Hivyo afrika linabakia kuwa bara lililo duni sana lakini lenye kipaji cha ngono.
kwa biashara hii ya ukabila na uchakachuaji, kenya haiwezi kuwa na heshima hata kidogo na wala haiwezi kuaminika. Hii zana ya East Africa community itakufa tu. Kama Mkikuyu hawezi kuwaheshimu wakenya wengine awezaje kuwaheshim waganda na watanzania?
Hilo sio Tatizo, tatizo hapa ni kwamba huyu jamaa Bw. Odinga ndio mkubwa wa Serikali, na sio mpinzani, mimi sijawahi kusikia ktk historia ya Dunia hii kwamba Serikali inalalamika kuibiwa kura, angekuwa mpinzani sawa angalau ungesema Serikali kwa kutumia machinery yake imeamuibia, lkn ni mkubwa Serikali na Mgombea mwenza wake Bw. Musyoka ni Makamu wa Raisi wa Serikali hiyo hiyo sasa, anamlalamikia nani, haswa?
I don't think if it will work out!
Asema uchaguzi umefanyika "KIENYEJI"...
Kenya imekabidhiwa kwa watu wa ajabu kweli kweli, time will tell na haitachukua muda president na makamu wake kukorofishana wakati wa kugawana madaraka.
wacha arekebishe demokrasia...
Mimi hizi kauli not yet uhuru, au kama ndugu zetu wa chadema wanavyosema wanataka kuikomboa nchi, huwa naona wanadownplay jitihada za wazee walipigania uhuru. Nadhani bora watafute lugha nyingine ya kuhamasisha watu...
uchaguzi uliendeshwa na tume HURU, siyo serikali ya Kenya
You know nothing about Literature,
You know nothing about interpretations.
Kaa kimya hujui kitu.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Mkuu njoo Kenya ujifunze sio kubwabwaja mashudu.Sio kweli, Tume iko Huru lkn, Lakini ni jukumu la Serikali kuisimamia na kuhahakisha kwamba inafwata Sheria za nchi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba kura haziibiwi, kuilipa hiyo tume na ndio maana tume inafanya kazi na Jeshi la Polisi watu wa Usalama n.k ambao ni Serikali!
Mkuu njoo Kenya ujifunze sio kubwabwaja mashudu.
*Hii ni tume huru na mipaka ya kenya na haipaswi kuingiliwa utendaji wake na serikali, inafanyakazi katika mazingira kama ya kimahakama.
Na kama inaweza kuingiliwa basi wa kwanza kufanya hivyo atakuwa ni Rais Kibaki ambaye ni Uhuru supporter.
*Ni kweli katika uhalisia wa matokeo Raila kashindwa lakini kama kuna kasoro kadhaa ambazo zinampa nguvu kuhoji matokeo hayo kisheria na ikibidi kubadilisha mwenendo wa matokeo ya uchaguzi, basi hapo yuko sahihi kabisa.
*Japokuwa mimi sio supporter wa siasa za Kenya hususani siasa za Raila Udinga, lakini mambo haya yanayosemwa yanatia mashaka pia kama demokrasia ilifuata mkondo wako
1/Kuna vituo kadhaa vya uchaguzi ambavyo idadi ya kura ilizidi watu waliojiandikisha!!
2/Sheria ya sasa inataka kura zihesabiwe kwa Electronic machine lakini utaratibu ulibadilishwa ili zihesabiwe kwa mikono kwa sababu mitambo ilishindwa!!
3/Wakati wa kuhesabu kura kwa mitambo Zaidi ya kura laki tatu zilikuwa zimeharibika kabla hata kura zote hazijahesabiwa, zoezi la kuhesabu lilipobadilishwa na kuwa kwa mikono kura zilizoharibika zilipungua na kuwa chini ya laki moja!!!
4/Mitambo ya kuhesabu kura iliweza kuzidisha kura zilizoharibika hadi mara 8 zaidi, na sheria inataka kura zote zihesabiwe kwa mitambo!!!