Kenya 2022 Raila Odinga anatapatapa: Ameibuka na hoja tofauti, sasa anadai Ruto hakufikisha kura 50% + 1

Kenya 2022 General Election
Lengo la Raila ni kuivuruga kenya. sababu ya uchu na uroho wa uongozi.
 
Lengo la Raila ni kuivuruga kenya. sababu ya uchu na uroho wa uongozi.
Raila ana haki ya kupeleka malalamiko yake mahakamani. Anaitumia haki hiyo. Mahakama itaamua kama hakuna kesi basi ombi lake litatupwa vinginevyo kesi itaendeshwa. Tusubiri tuone, lakini Raila ni mjenzi mkuu wa demokrasia na utawala bora Kenya. Ashinde asishinde kuna mafunzo yatakayo patikana hapo ambayo yata tumika 2027. Tuache inyeshe tujue wapi panavuja.
 
Yanatuhusu?
Yanatuhusu sana, kwanza ni kwa sababu kuna kitu cha kujifunza hapo! Yale mazuri tunaiga na yale mabaya tunaona namna ya kuyaepuka! Dunia ni kama kijiji kimoja, kinachotokea upande mmoja huwa na athari katika sehemu nyingine. Nitashangaa kama haulijui hilo!
 
Na ww n mahakama ya high court au sio
 
wewe unajua ana ushahidi gani? keep patience
 
anaitumia haki hiyo vibaya sana! anazidi kupoteza resources za wakenya bure!!
naamini mahakama itatupilia mbali huu upuuzi wenye lengo la kupowapotezea muda wa maendeleo wananchi.
 
Mahakama ya juu itatupilia mbali hii petition kwa sababu ina nyima/kuchelewesha haki za wakenya walio amua 9/8
zaidi ya wakenya 6million waliamua kuwa Ruto ndiye Rais wao lazima waheshimiwe.
 
Huyu mzee safari hii anaenda kupata aibu mahakamani
 
Mwenzio amebeba mzigo wa makaratasi amepeleka mahakamani, wewe unasema anatapatapa tena kwa kigezo cha matokeo ya Chebukati anayelalamikiwa na Odinga na timu yake.
Inamaana pamoja na RO kuwa team deep state, bado wamem-outsmart? Si ajabu sasa wafuasi wake na viongozi wenzake wanaahamia kwa president-elect kwa spidi ya 5G
 
Hii ndo demokrasia isiyo na mipaka. 1% inapelekea kutumia tena mamilioni ya uchaguzi. Kama mm ndo raisi natumia udikteta natoa maamuzi msumbufu namfanyia figisu.
 
Why not the other way round? Usikute team Raila waliweka mategemeo ambayo hayakuzaa matunda, so wanaishi katika ulimwengu wa ndoto za Alinacha.
 
Umesoma ripoti ya wale waasi 4 wa IEBC?
 
Umepita mulemule, mkuu. Raila hawezi kukubali matokeo yoyote ya uchaguzi, hata akishinda yeye.

Correction: 0.01%, and not 0.1% kama ulivyoandika. Hizi namba zina wenyewe ujue. Hahahaha
 
Mmeshageuka mahakama, nyie time yenu haishitakiwi ndio maana mnaumia.mtu akienda kudai haki yake mahakamani
2017 pamoja na mapungufu yote, kilichosababisha hasa Supreme Court kubatilisha matokeo ni OPACITY (OPAQUENESS ama OPAQUE NATURE, kama aandikavyo Ms J. ChererrorπŸ™‚). Remember servers za Msando?

Sasa hilo tatizo limeshughulikiwa katika uchaguzi huu. Ruto anaapishwa tarehe 5 Septemba!
 
2017 alikimbia uchaguzi wa marudio. Sasa asitegemee kabisa kusikilizwa hahaha
 
anaitumia haki hiyo vibaya sana! anazidi kupoteza resources za wakenya bure!!
naamini mahakama itatupilia mbali huu upuuzi wenye lengo la kupowapotezea muda wa maendeleo wananchi.
Mawakili wake 54 je?
 
Huwezi kutegemea fact moja katika civil complaint kutengeneza kesi yako mara nyingi unaweka fact nyingi ili moja ikidondoka nyingine inasimama. Sasa huyo ngumbaru aliyetengeneza mada hii kanyofoa ka fact kamoja ili tuamini kuwa kesi yake ndiko pekee ilipolalia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…