Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Raila Odinga: Polisi wa Tanzania kama Ulaya. Adai wanaweza kusubiri umalize kazi zako ndio wakukamate

Anajua akiivuruga Kenya atakimbilia Tanzania.

Police Force siku zote haina kubembelezana mpaka itakapo Kuwa Police Service.

Tanzania Kuna Aina kuu tatu za wahalifu wa Kwanza ni Wenye nafasi mbalimbali serikalini/ wafanyabiashara wakubwa HAO hawakamatiki. Polisi hushinda kwao kuomba misaada wanaitwa wadau

Kundi la Pili ni white collar criminal, wahalifu wanaoitwa Kwa Barua au simu hawakai Mahabusu hata wakiwa na kesi kubwa.

Kundi la tatu hili ni letu walala hoi huwa hata kuonana na Polisi hatutaki iwe tumefanya kosa au la kwasababu unaweza kukamatwa Kwa kosa A ukajikuta unashtakiwa na kosa B. Sisi ndiyo tunahusika na kukaa Mahabusu Kwa muda mrefu tunapokamatwa lazima tusimangwe au kupigwa.

Kwahiyo Polisi wa Tanzania wanafanya kazi kulingana na mtuhumiwa yupo kwenye kundi lipi.
 
Katika kuwaponda Polisi wa Kenya kuelwkea siku ya Maandamano Makubwa yanayoendelea , Mh Raila Odinga amedai kwamba Polisi wa Tanzania ni waungwana na werevu kama Polisi wa Ulaya , na kwamba wakitaka kukukamata wanasema "NDUGU TUNAOMBA TUKUKAMATE"

Hivi kweli jamani hiki alichokisema Odinga ndicho wanachofanya Polisi wa Tanzania ?

Toa maoni yako .
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ni sahihi kabisa, Sugu alikuwa anambishia afande tena very senior kule Mbeya alikwenda kumkamata, akaonbwa kwa upole kuwa alinde heshima yake. Kisha akakamatwa kwa heshima na taadhima 😎.
 
Kwa kuwalinganisha,polisi wa Tanzania hawafui dafu kwa wale wa Kenya kwa brutality.

Curfew ya COVID tu wakaidi walikula shaba na cases za polisi kubaka wanawake wakiwa kwenye operations zao ni kawaida tu kule Kenya.
 
Raila kaongeza sana chumvi 😀😀😀🙌. Ila kimaadili polisi wa Tanzania wana nafuu kuliko wa Kenya. Hao polisi wa Kenya ni wapenda rushwa na makatili kupindukia.

Polisi wa Tanzania hata akitaka rushwa lazima azunguke zunguke tofauti na wale wa Kenya ambao rushwa unawapa kama sadaka wakikukamata.

Kwa waendaji wa Nairobi kupitia Namanga huwa mkifika checkpoint ya kwanza tu baada ya kuvuka mpaka kama huna passport kuna hela unalipa unapita zako.

Ndiyo maana hawa waethiopia wengi hukamatiwa Tanzania au Zambia. Polisi wa DRC ndo wamewazidi ushenzi hao polisi wa Kenya.
 
Anajua akiivuruga Kenya atakimbilia Tanzania.
Police Force siku zote haina kubembelezana mpaka itakapo Kuwa Police Service...
Mkuu umeandika facts. Inaonekana ushakuwa victim wa vitendo vya police??
 
Raila kaongeza sana chumvi 😀😀😀🙌. Ila kimaadili polisi wa Tanzania wana nafuu kuliko wa Kenya. Hao polisi wa Kenya ni wapenda rushwa na makatili kupindukia...
Achaga toa siri za kambi
 
Back
Top Bottom