Rais anavyotembea na walinzi waliobeba mitutu anaonesha nini wananchi?

Rais anavyotembea na walinzi waliobeba mitutu anaonesha nini wananchi?

FourTwoNet

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2022
Posts
1,236
Reaction score
2,512
Mpaka hapo uzi kamili....

Nimeona mama yuko ziara, halafu majamaa yamepiga combat, na mitutu juu, halafu ziara yenyewe ni kaenda kuona wananchi wake.

Hii ina effect gani kisaikolojia kwa wananchi? Na inamaanisha nini? Maanake sio kwamba usalama wameshindwa kuweka usalama pasipo 'ku send message'....sijui kama naeleweka lakini.
 
Chief mimi huwa namkosoa mama kwenye mambo mengi tu lakini kwenye swala la usalama wa Rais bado hata huo uliouona hautoshi.Rais ni lazima alindwe mkuu.
tupo na maadui wengi wa nje na ndani.
Hata ujilinde na mamilioni ya Askari,siku wakiamua kukutoa wanatumika hao hao wa ndani na walinzi.

Uwe kama Nyerere tu. Ukiwa kawaida kwa wananchi hao. Unatenda yaliyo sawa kwa nchi. Keki ya Taifa inagawiwa sawa mpaka kwa wakulima masikini huko chini,hakika unaweza ukatembea bila hata mlinzi mmoja.

Lakini sio kama sasa mafisadi wachache wameikamata nchi. Wanaitafuna nchi kuanzia madini,mpaka gesi. Kuanzia Mali asali mpaka wanyama. Kuanzia ardhi mpaka tozo. Kuanzia madawa ya kulevya mpaka pesa yote wameficha. Hapo unategemea nini wakati wananchi wengi wananung'unika?.
 
Mpaka hapo uzi kamili....

Nimeona mama yuko ziara, halafu majamaa yamepiga combat, na mitutu juu, halafu ziara yenyewe ni kaenda kuona wananchi wake.

Hii ina effect gani kisaikolojia kwa wananchi? Na inamaanisha nini? Maanake sio kwamba usalama wameshindwa kuweka usalama pasipo 'ku send message'....sijui kama naeleweka lakini.
Weka picha weweee
 
Chief mimi huwa namkosoa mama kwenye mambo mengi tu lakini kwenye swala la usalama wa Rais bado hata huo uliouona hautoshi.Rais ni lazima alindwe mkuu.
tupo na maadui wengi wa nje na ndani.
Raisi ni raisi tu lazima alindwe hadi amalize muda wake kikatiba. Ingawa simkubali Mh.Samia toka anakuwa makamu wa raisi lakini hili la ulinzi mkubwa namuunga mkono tena aongezewe ulinzi mkubwa zaidi.
Mungu amjalie maisha marefu alee wajukuu zake.
 
Au wanaweza wakawa wanavaa kawaida tu lakini kwenye koti wanaweka mtutu.

Sio lazima ku display
 
Hamna picha, nimewah nkajua Kuna picha, Kumbe porojo tu za vijiweni
 
Mpaka hapo uzi kamili....

Nimeona mama yuko ziara, halafu majamaa yamepiga combat, na mitutu juu, halafu ziara yenyewe ni kaenda kuona wananchi wake.

Hii ina effect gani kisaikolojia kwa wananchi? Na inamaanisha nini? Maanake sio kwamba usalama wameshindwa kuweka usalama pasipo 'ku send message'....sijui kama naeleweka lakini.
Hicho hicho unachokiona
 
Mbona US wanatembea Hadi na nyau.

Tuwaache watu wafanye wajibu wao
 
Chief mimi huwa namkosoa mama kwenye mambo mengi tu lakini kwenye swala la usalama wa Rais bado hata huo uliouona hautoshi.Rais ni lazima alindwe mkuu.
tupo na maadui wengi wa nje na ndani.
Mkuu, kama umenisoma vizuri, sijasema asilindwe....ukiread between the lines utanielewa.
 
Maadui wetu ni ujinga, umasikini na maradhi. Nini kilimtoa mtangulizi wake, licha ya ulinzi kama kundi la ng'ombe?
Umenisoma eee! Yani ile inafanya hapo ni mesej ya kisaikolojia kwa umma... ni kama rais anaelewa hakubaliwi hivyo kutumia njia ya 'fear' na kutojali wananchi watajiskiaje wakiona raisi kazungukwa na ma himars utadhani kaenda ziara kwenye nchi ya kivita.
 
Rais ni icon ya nchi. Usalama wake ndio usalama wa nchi. Intelijensia inaliangalia hili kwa ukaribu sana, na kupanga safu ya ulinzi kwa Rais kwa kadiri wanavyoona inafaa kwa siku husika. Kwa hiyo, kumbe ulinzi wa Rais sio jambo lisilobadilika (kama tulivyozoea). Kumbuka tunakwenda na mabadiliko ya tekinolojia, ulinzi wa miaka ya 2000 hauwezi kutumika leo. We respond due to technological changes!
 
Back
Top Bottom