Hata ujilinde na mamilioni ya Askari,siku wakiamua kukutoa wanatumika hao hao wa ndani na walinzi.
Uwe kama Nyerere tu. Ukiwa kawaida kwa wananchi hao. Unatenda yaliyo sawa kwa nchi. Keki ya Taifa inagawiwa sawa mpaka kwa wakulima masikini huko chini,hakika unaweza ukatembea bila hata mlinzi mmoja.
Lakini sio kama sasa mafisadi wachache wameikamata nchi. Wanaitafuna nchi kuanzia madini,mpaka gesi. Kuanzia Mali asali mpaka wanyama. Kuanzia ardhi mpaka tozo. Kuanzia madawa ya kulevya mpaka pesa yote wameficha. Hapo unategemea nini wakati wananchi wengi wananung'unika?.